International beer day

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
18,075
Reaction score
25,179
Leo, Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa nane, ni siku ya kimataifa ya kinywaji kijulikanacho kama beer; iliasisiwa mwaka 2007 tu. Kama hujawahi kuonja beer, tumia siku ya leo kufanya hivyo lakini usizidishe - unaweza kuona kama ni chachu sana na haina utamu wowote. Na kwa wale maveterani, kila la heri na sikukukuu!! Tukutane ofisini salama jumatatu ijayo saa mbili kamili bila kuchelewa.

...............he was a wise man who inveted beer!
 
Hivi hata spirit Kama K Vant ni beer au Vipi?

Mimi nipo na K Vant yangu baridi kabisa sitaki bugudha.
Spirits zote ikiwa na pamoja na gongo, konyagi, chang'aa, kachasu, kill-me-quick siyo beer. Tafuta Lager, Stout, Light au Bitter beer uweze kujumuika na wenzio kabla sikukuu haijaisha.
 
Ngoja ni update kule kwenye mada yetu
 
kwan beer haileti ulevi ??? usijikaze sana mkuu ? fikiri zaidi
Pombe zote pamoja na madawa fulani yana kilevi ndani yake; kuzitumia haina maana ya kuwa ni ulevi ingawa unaweza kulewa. Ulevi ni tabia mbaya za kuzidi kipimo mara zote, na watu hao ndio wanaoitwa walevi. Wakati Obama anakunywa beer hapa, haikuwa na maana kuwa ni mlevi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…