Instagram kuna siri gani?

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
8,116
Reaction score
5,370
heshima kwenu wanajamvi.
mi ni member wa insta ila si mdau sana,nilianza kutumia insta mwaka jana ili nione ikoje,sasa kuna mambo naomba mnifafanulie kuhusu instagram:
1.ukiachilia mbali swala la kutangaza biashara, nini faida nyingine ya kuwa na followers wengi? maana naona watu wanabembeleza tuwafollow.

2.nini hasa hufanya mtu amfollow mtu mwingine ambaye wala accaunt yake haina mvuto insta? mfano kila siku huwa nakuta follow requests lakini ac yangu inapost 12 tu na zote zakawaida sana tena wala sijawahi kupost picha yangu hata sura tu.

3. kuna watu wanaomba sana tu-like picha zao wanazopost,sasa je picha ikiwa na likes nyingi yeye anafaidika nini?

4. hivi nikiamua kum-unfollow mtu fulani je yeye huko atajua kuwa nimemu-unfollow?

==>tafadhali naomba mnijulishe hayo maana naona ni kama siielewi vile insta...naona ni kama watumiaji wengi washamba kwa kupost tu mapicha hovyo,kama sio hivyo basi mi ndio mshamba kwa kuwashangaa wao.
 
Wewe ndio mshamba kwa kujiunga na instagram halafu hakuna uwekacho....

Ni sawasawa na mtu anayenunua antena au dish wakati hana TV...
 
Wewe ndio mshamba kwa kujiunga na instagram halafu hakuna uwekacho....

Ni sawasawa na mtu anayenunua antena au dish wakati hana TV...

sasa mkuu kuna wadau huko kila siku wanapost tu picha zao asubuhi mchana jioni hata usiku... wala hawaandiki CAPTION yoyote... je hapo wanafaidika nini... binafsi huwa naona ni kama kuuza sura tu
 
Vijana tunapenda attention ni hAli ya kawaida tu,

sawa mkuu, sasa naomba unisaidie hivi nim-unfollow mtu fulani je naye atajua kuwa nimemu-unfollow?

nataka ni punguze watu wanaopost picha za hovyo huko.
 
sasa mkuu kuna wadau huko kila siku wanapost tu picha zao asubuhi mchana jioni hata usiku... wala hawaandiki CAPTION yoyote... je hapo wanafaidika nini... binafsi huwa naona ni kama kuuza sura tu

Hahaha...

Ndio kazi ya hiyo mitandao ndugu, kuweka matukio ya maisha kwa njia ya picha...
 
>>>>>Kuna wengine wenye followers wengi wakifika kipindi fulani wanauza account kwa kiasi fulani cha pesa na watu wananunua kwa ajili ya kutangaza biashara...

>>>>>Then ukiwa na followers wengi wenye biashara wanaomba uwapostie tangazo wanakulipa kiasi fulani cha pesa....

>>>>Pia kama kuna mtu atahitaji kupewa "shout out" kwenye account ya mwenye followers wengi atalipa pesa pia....So kafaida kapo...
Kwa mfano kuna jamaa(mmarekani) nilimuomba "shout out"
kwenye account yake akanambia nimlipe 25$...sasa piga mahesabu kwa mwezi anaingiza kiasi gani kama anatoa "shout out" angalau mbili kila siku..25$×60..
Dollar 1500$ si haba sana na usikute anapost picha za nyumba au magari au pikipiki n.k...
>>>Na kuna visababu vingine vinawafanya watafute followers wengi....

So mambo yanaenda hivyo mkuu....
japo kuna wengine wanahitaji kuuza sura tu...
 
sawa mkuu, sasa naomba unisaidie hivi nim-unfollow mtu fulani je naye atajua kuwa nimemu-unfollow?

nataka ni punguze watu wanaopost picha za hovyo huko.

Akiamua kuangalia atajua, ila watu hawana time hizo mtu anamamia ya follower kama sio maelfu, huo mda wa kumuangalia mtu mmoja baada ya mwengine atakuwa hana

Ila kama mtu ana follower watatu tu then ukajitoa wakabaki wawili hapo ataahtuka😃
 
Kuna apps kibao za kujua kama mtu ameku unfollow, kama unfollowgram na nyinginezo.. Kuhusu likes na followers ni life style ya mtu.. Ila mara nyingi what people post sio maisha yao halisi..
 

aisee kumbe watu wanapiga hela kirahisi hivyoo
 
Kuna apps kibao za kujua kama mtu ameku unfollow, kama unfollowgram na nyinginezo.. Kuhusu likes na followers ni life style ya mtu.. Ila mara nyingi what people post sio maisha yao halisi..

kumbe mpaka atumie apps nyingine...hapo sawa maana kuna watu nafahamiana nao ila tuna interests tofauti so nataka niwa unfollow kwa amani tu ila wasishtuke mapema wasije wakaona ni kwama nawadharau vile
 
Insta sijui fb wala sina mpango wa kuwa na acount huko, JF INATOSHA SANA!
 
Mitandao ya kijamii inabuniwa kujazia pengo lililopo.
Kama hujui maana ya mtandao fulani ni bora uulize.
Kila mtandao wa kijamii una maana yake, anzia twitter, facebook, snapchat, pininterests, jamiiforums etc.
Instagram ni mtandao wa kushare matukio kwa njia ya picha, kuna watu wapenzi wa picha na hawana muda wa kusoma maneno mengi.
 
Watu wengi hawana shughuli maalum ndio maana wanaishia kushinda mitandaoni 24/7 insta, fb, n.k
 
huwa naona huko mtu kapost picha mwingine anacomment "follow me @ fulanifulani....
Yeah wanajipromote...but sijui jamaa hasa wa ulaya wanatumia njia gan..
kwa sababu unaeza kuta jamaa anafollowers 2m idadi ambayo...hata msanii wa bongo hana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…