Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Kuna miti ya huzuni, ya majuto, ya kushindwa, na ya hofu iliyoota kwa miaka mingi ndani ya nafsi yako. Lakini leo, ujumbe wangu kwako ni huu, kata mti, panda mti.
Kata mti wa kukata tamaa, panda mti wa tumaini. Kata mti wa uchungu wa jana, panda mti wa furaha ya kesho. Kata mti wa lawama zisizokoma, panda mti wa msamaha unaoponya.
Kata mti wa hofu inayokufunga, panda mti wa imani inayokuinua.
Usiogope kuchukua shoka ya maamuzi. Najua sio rahisi kukata mti wa mazoea au wa uoga, lakini kumbuka, hakuna lenye mwanzo lisilo na Mwisho. Ukikata mti, panda. Usiache ardhi tupu, maana moyo usiopandwa huota magugu tena.
Mungu wetu si Mungu wa kukata tamaa, bali ni Mungu wa kuumba upya. Alisema hivii, “Tazama, nafanya mambo mapya” Isaya 43:19. Panda mti wa maisha mapya. Panda ndoto zako tena. Panda imani yako tena. Panda upendo tena. Halafu muache Mungu akunyeshee mvua.
Kata mti, panda mti na utavuna msitu wa baraka.
Wimbo Ulio Bora Media