Inspekta wa polisi auawa kwa kudhaniwa mwizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inspekta wa polisi auawa kwa kudhaniwa mwizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Inspekta wa polisi auawa kwa kudhaniwa mwizi[​IMG]Na Suzy Butondo, Shinyanga

  INSPEKTA mkaguzi wa polisi, George Libenti, 36, ameshambuliwa kwa kipigo na wananchi wenye hasira kali kwa kudhaniwa kuwa ni mwizi na kusababishiwa maumivu makali na baadaye kufariki siku iliyofuata.

  Tukio hilo lilitokea Novemba 13, majira ya saa 1.30 usiku katika eneo la Ndembezi lililo kwenye manispaa ya Shinyanga baada ya askari huyo kudaiwa ingia kwenye makazi ya watu kwa nguvu na kulazimisha kuingia ndani ya nyumba.

  Kuona hivyo, wakazi hao walianza kupiga kelele za kuomba msaada na ndipo watu walipokusanyika na kuanza kumshambulia kabla ya kutoa taarifa polisi za kuomba msaada. Polisi walifika eneo hilo muda mfupi baadaye.

  Kamanda wa polisi wa mkoani hapa, Daudi Siasi alisema kuwa askari walivyopigiwa simu, walienda eneo la tukio lakini walipofika waligundua kuwa mtu aliyedhaniwa kuwa mwizi ni inspekta wa polisi ambaye walimkuta akiwa amelewa na kumpeleka kituoni.

  Kamanda Siasi alisema inspekta huyo alikuwa na matatizo ya akili na kwamba alikuwa hapangiwa kazi za kipolisi kutokana na matatizo hayo ingawa alikuwa akiendelea kutambuliwa kuwa mfanyakazi wa jeshi hilo. Alisema chanzo cha kifo cha Inspekta huyo bado kinautata kama kilitokana na maumivu aliyoyapata kutokana na kipigo cha wananchi ama ni matatizo mengine. Tayari mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika leo.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Poleni wafiwa na poleni geshi ra poris!!!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe

  .R.I.P..GL
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280

  Duh hayo Mambo INSPEKTA mkaguzi wa polisi apata kipigo Heavy bongo kweli hii ni bongo hata Ma INSPEKTA mkaguzi wa polisi wanakula vipigo hiyo kweli Bongoland hahahahahahahah Poleni sana ndugu wafiwa na Ndugu wana usalama poleni sana
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Duh!.....
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280

  Nina wasiwasi alikitetea chadema;wacha inspekta unamkumbuka

  R.I.P GENERAL KOMBE?
   
Loading...