Insha 3 za Mwal. Nyerere

muddymrisho

New Member
Dec 14, 2016
4
45
Insha 3 za Mwl. Nyerere. Kitabu nilichokipenda zaidi kwa Mwaka huu unaoyoyoma.... Mwl. anasema.....

"Kwa hiyo katika utaratibu wa kibepari na kikabaila chama cha wafanyakazi si chombo cha kuondoa unyonyaji, bali ni chombo cha kupunguza makali ya unyonyaji. Si chombo cha kukata mirija ya wanyonyaji: bali ni chombo cha kuwawezesha wafanyakazi kuikabili mirija ya wanyonyaji na kuipunguzia nguvu zake.
Ukabaila unaweza kuzaa maendeleo, lakini pia unazaa chuki, kwa sababu msingi wake ni dhuluma. Hakuna jambo jema kwa binadamu kama kusaidiana: maana kusaidiana na kushirikiana ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli na msingi wa kupendana.
Kwa ajili hiyo hakuna jambo baya kwa Binadamu kama kudhulumiana. Mtu kumnyonya mtu, au kumdhulumu mtu ni unyama, ni ushenzi. Ushenzi huu ndio asili ya maafa yote, kama vile baina ya raia wa nchi ile ile: au baina ya nchi mbalimbali: na ndiyo sababu hasa ya ukoloni.
Kitu peke yake kinachoweza kuondoa balaa ya unyonyaji katika maendeleo ya binadamu ni sharti letu la tatu la Maisha ya Kijamaa -kufanya kazi pamoja kwa faida ya pamoja. Kutakuwa na maendeleo makubwa ya vitu na watu.
Maendeleo ya kikwelikweli, ambayo hayana unyonyaji na hayana chuki, lazima yatokane na Utawala kamili wa mfanyakazi (note:mfanyakazi, si mwajiriwa).
Lazima mfanyakazi mwenyewe katika ushirika kamili na wafanyakazi (si waajiriwa) wenzake atawale mali yote ya kijiji au nchi yake. Kila tone la jasho lake lazima limsaidie kwa kutimiza mahitaji yake katika umma."

Katika insha hizi 3, Mwalimu amefundisha kifalsafa juu ya USAWA WA WATU, KAZI na KUISHI PAMOJA. amefafanua umuhimu wa kazi katika maisha ya mwanadamu. Ameonyesha Usawa na Utofauti wa Binadamu.
Unaweza kuchanganyikiwa usipokuwa makini kuelewa anachokizungumza. Lakini unapofikia hitimisho lake, unaishiwa hoja ya kupingana naye isipokuwa kukiri Ukweli na usahihi wa hoja zake alizojenga kwa mifano mahiri yenye misingi ya ukweli na mantiki.
Anasema Binadamu wote ni sawa katika ubinadamu wao, lakini anasema pia kwamba kwa 'nafsi' yangu mimi ni tofauti kabisa na binadamu wengine. Kwamba, NAFSI ndicho kitu peke yake ambacho Binadamu hashirikiani na Binadamu mwingine yeyote! Kwamba, thamani ya nafsi ni thamani ya pekee: ndio thamani inayomfanya kila binadamu awe yeye asiwe binadamu mwingine yeyote.

Ni falsafa rahisi na halisi kwa Maisha na Mahusiano ya kijamii.
Naam, Nyerere anaishi!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom