Injinia Hers na Kugombea urais wa Yanga.

Nkondo 2

Senior Member
Oct 10, 2016
163
127
Zimekuwepo taarifa kutoka kwa mashabiki na wanachama wa club ya Yanga wakishawishi na kutaka sana ndugu Hers agombee urais wa Yanga.

Nafikiria hivi hawaoni mgongano mkubwa wa kimaslahi iwapo kweli Injinia Hersi akiamua Kugombea na akawa Rais!!?
Kvp!!? Hers ni sehemu ya wafadhili wa sasa wa Yanga ambao wanatarajiwa kuwa wawekezaji kwenye mfumo mpya ambao club ya Yanga inauendea, sasa unampaje urais mtu ambae anahitaji kuja kuwa mwekezaji!! Atajisimamia vipi? Je wawekezaji wengine watatendewa fair kweli??

Makosa ya mihemko kama hii ndo waliifanya Simba halafu leo wanalalamika et Mwekezaji amepewa mamlaka yote na mwenyekiti wa club hana lolote zaidi ya kufungua na kufunga vikao. Kipindi wanapitisha katiba ilipelekwa kishabiki sasa akili zimeanza kutumika mianya ya udhaifu wameanza kuiona. Yanga nao nawaona wanataka kuyapeleka mambo kihisia zaid kitu ambacho baadae kitaibua migogoro isiyoisha.

Nawasilisha.....
 
Kwani rais wa Real Madrid na Berceloma sifa yao kubwa si ni kuwa na hisa nyingi kwenye club!
 
Tatizo vilabu vyetu havitaki wanachama, ili upate uanachama kwenye vilabu vya Simba na Yanga basi connection yako ni ndefu.
Binafsi sioni Kwanza umuhimu WA michango Ile wakati timu zina wafadhili. Faida ya wafadhili ni nn sasa Kama clubs zinapitisha mabakuli kila siku.
 
Urais wa mpira anatakiwa mtu mwenye ufahamu na mambo ya mpira. Mtu atakaye leta Mabadiliko halisi kwenye klabu ya mpira.
 
Back
Top Bottom