WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
msichana na familia yake hawajatumia busara kwa kweli....warudiane na wavute subira mtoto akizaliwa akapimwe DNA kama wa jamaa asimtelekeze lakini kama sio wake amshitaki huyo mchota maji...
Mimi nina mawazo tofauti... ajali hii ingetokea baada ya wawili hawa kufunga ndoa basi ningeunga mkono kabisa kitendo cha kusameheana.Na mara nyingi wanaume hutafuta kisingizio cha kututendea yale yaliyo kinyume na mara zote tunawasamehe.Kwa vile kulikuwa hakuna mkataba/makubaliano ya kuwafunga kindoa basi siyo sahihi kuwasuluhisha.Ni vema ndoa ikaanza bila historia za ajabuajabu.Hii ni kwa manufaa ya huyo mke mtarajiwa zaidi.Akiendekeza basi atakuwa yeye ni wa kuletewa hadithi za ajabu katika ndoa yake na hatakuwa na jinsi.
Unajua yule dada, anashidwa kuelewa maana mlinzi anasema waliingia ndani wanaongea na yule msichana, sasa anahoji, iweje alikuwa anaongea huku hajitambui au ndo mambo ya ushirikina?
Kuchotachota maji pale, utakuta mdada alikuwa anamlia timing siku nyingi na siku hiyo akatimiza ndoto yake kwa kutumia udhaifu wa mkaka huyo.Inaelekea huyo mkaka naye mhhhhh....
uchumba unasuluhishwa? jamani mtumie zana jamani, huyo dada ashikilie msimamo huo huo.
Asante NY,
Ukishasuluhisha uchumba ujue kusuluhisha ndoa itakuwa ni kama kupiga chafya.Itakuwa haina maana.
NDIYO HAPO USHANGAE.Ni vipi ukimwi utaisha?Unajua kuwa zaidi ya nusu ya wanaume wa Tanzania waliopima DNA wanalea watoto sio wao kulingana na wanawake wao kulengesha?
Huyu dada ashukuru kuwa hiki kitu kimetokea kabla ya ndoa.Huyo hakuwa mume wake toka mwanzo.Asonge mbele.