ingekuwa wewe ungefanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ingekuwa wewe ungefanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Joyceline, Jun 15, 2009.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nina rafiki yangu, alitegemea kufunga ndoa dec thisyear,
  Jana amemuacha mchumba wake waliyekaa 5 years tangu urafiki hadi uchumba.

  huyo mchumba wake katoka arusha kaamia hapa dar huko maeneo ya kimara kwa biashara zake.
  Hapo kwake kuna kisima cha maji , kwa hiyo majirani wanakuja kuchota akiwepo au asipokuwepo.

  mwezo 1 uliopita jioni alienda bar moja kunywa, amekaa kidogo akaja dada mmoja yeye anmfahamu anamuona akija kuchota maji,
  Akamwambia kaka naomba nikae hapa namsubiri jamaa yangu akamwambia kaa tu usijali, wanaongea ongea yule jamaa kanywa kachoka akataka kuondoka kwenda kwake, yule msichana akamwambia hata mimi jamaa yangu naona kanidanganya nipe lifti, akamwambia twende,
  Kwa mujibu wa yule jamaa mpaka hapo hajui kilichoendelea amekuja kushtuka saa saba usiku yuko kitandani na yule msichana kama walivyozaliwa hajitambui.
  akaanza kumuuliza imekuwaje akamwambia mimi nakupenda siku nyingi sikuwa na njia ya kukuingia, jamaa kachhanganyikiwa msichana kavaa nguo zake kaondoka usiku huohuo,
  Yule jamaa asubuhi kamuita mpenzi wake akamuelezea tukio lilivyokuwa basi kukatokea kutokuelewana hadi wazazi wakaitwa wakawasuluhisha sana vikao kibao yakaisha.

  Sasa juzi yule bibie kaja kasema anamimba ya yule kijana na anataka amuoe yeye hawezi kulea mtoto peke yake.
  Binti kaja na shangazi zake na mama yake ni wazaramo wamemkalia kijana kooni wanasema lazima amuoe mtoto wao amemuharibia masiha.
  Sasa huyu rafiki yangu alivyojua hivyo kamuacha mchumba wake bila kusikiliza maelezo wala utetezi wowote tena seriously ikiwa ni pamoja na kurudisha kila kitu hadi pete ya uchumba kavua karudisha,

  Ila kijana kawapa shua kwamba hamuoi, sababu hampendi na alilala naye bila kujujua na hiyo mimba labda aliitegesha, kama mtoto ni wake kweli atamtunza akiwa mkubwa atamchukua.
  Sasa huu uamuzi aliouchukua shost ni hasira, wivu, au ametumia busara,
  au yuko sahihi kufanya hivyo.
   
 2. S

  Salehe Ndanda Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  First of all Thank you jamiiforum and God bless you.Ningekuwa mimi kwanza yule mwanaume alivyofanya sawa sawa namuungamkono KUSEMA UKWELI ukikutana na mambo usioyaelewa matukio mabaya usio YAPENDA ujawahi kukutana nayo nivizuri kumwambia mtu wa karibu yako.
  Yule MCHUMBA alivyofanya sio sahihi, HASIRA HASARA wherever you go, amekurupuka ' think before you rip' sasa ukipata mchumba anayesema 'UKWELI USHUKURU MUNGU' kwa vijana wa sasa, je yule kaka asingesema ukweli harafu akaendelea naye yule dada kimapenzi ndio angekuwa anampenda mchumba wake? au alivyosema ndio ameonyesha ANAMPENDA MCHUMBA WAKE KULIKO ANGEFICHA?
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Unajua yule dada, anashidwa kuelewa maana mlinzi anasema waliingia ndani wanaongea na yule msichana, sasa anahoji, iweje alikuwa anaongea huku hajitambui au ndo mambo ya ushirikina?
   
 4. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwanza aache pombe. Hiyo yote sababu ya ulevi.

  Majaribu mengi yanatukuta kwa sababu tunayafuata huko yaliko.

  Tujiepushe na majaribu, hata Mungu atatusimamia pale tunapokumbwa na majaribu.

  Nawapa pole wachumba.
  Lakini wasilaumu sana pengine ndoa haikubarikiwa ifungwe.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mke/mume mwema hutoka kwa BWANA! Ukitumia akili yako ndio hayo yatakukuta. Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa, sasa usipomwomba akupe mwenza wa kufanana naye, what do u expect? Halafu ukiachwa na mchumba usilalamike, labda Mungu kakuepusha na baya zaidi. Wewe mtegemee Mungu utapata furaha ya kweli. Halafu ujue mchumba sio mke/mume, just a fiance`. Mwisho: SIKU YA KUFANIKIWA, UFURAHI, SIKU YA KUPATWA NA MABAYA UFIKIRI!
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ingekuwa mwanamke ndio kafanyiwa hivyo ningesema mambo ya "spanish fly" SPANISH FLY APHRODISIAC,

  lakini kwa mwanaume mnh... lifti mpaka kitandani kwake? akishapima UKIMWI aache pombe!
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  uchumba unasuluhishwa? jamani mtumie zana jamani, huyo dada ashikilie msimamo huo huo.
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa mara ya kwanza maishani I feel pity kwa huyo mkaka!!

  - Kitendo cha yeye kumweleza mchumba wake juu ya tukio lile kinadhihirisha wazi kuwa anampenda kwa dhati na ni mwaminifu kwake. Inatupasa tuamini kuwa mauza uza siku hizi yapo hasa ukizingatia idadi ya waganga wa mapenzi inazidi kuongezeka. Kama huyo mchotamaji alikiri kuwa alikuwa anampenda siku nyingi kitu gani kingemzuia kutafuta miziziology ya kumpumbaza huyo mkaka hata akajikuta kalala naye?

  - Kitendo cha shostito wako kuvunja uchumba sikioni kama ni cha busara unless aniambie kuwa baada ya hiyo skendo ya kwanza mchumba wake aliwahi kulala tena na huyo mwanamke. Ila kama mimba hiyo ni mazao ya huo usiku mmoja wa mauza uza sidhani kama mkaka anastahili kuadhibiwa kiasihicho. Ningekuwa ni mimi nafikiri ningekuwa bega kwa kiuno na huyo kaka kiasi cha kuwa huyo mchotamaji hakuna rangi angeacha iona kwa kitimutimu ambacho ningemfanyia .... na harusi tungeifunga kesho yake baada ya yeye kuja na kina shangaziye.

  Ni wazi kuw akatumwa huyo!!

  Eti kaharibiwa maisha mtu anajua hadi kubaka ataharibiwaje maisha!!?
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mh! yule dada alijirengesha!! huyo rafiki yako alitakiwa asamehe tu, ile ni mitego tu ya kidunia tena ukute hata hiyo mimba siyo ya jamaa ni ya mtu mwingine kabisa!
  Sema shemeji yako kondom yeye hazijui kabisa!!?
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jun 16, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unajua kuwa zaidi ya nusu ya wanaume wa Tanzania waliopima DNA wanalea watoto sio wao kulingana na wanawake wao kulengesha?
   
 11. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ukimwi je?
   
 12. s

  sinani Member

  #12
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  dah wanaJF hili ni bonge la mkasa..kwa mawazo yangu jamaa anampenda mchumba wake ndo mana akaamua kumwambia kitendo kilivyotokea hakupaswa kuadhibiwa kiasi hicho,msichana na familia yake hawajatumia busara kwa kweli....warudiane na wavute subira mtoto akizaliwa akapimwe DNA kama wa jamaa asimtelekeze lakini kama sio wake amshitaki huyo mchota maji...
   
 13. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mimi naona huyu binti (mchumba) uamuzi aliofanya ni sahihi kabisa. Kwanini? Kwasababu kama huyu kijana ameweza kufanyishwa tendo la ndoa kwa ushirikina ina maana kuwa kama atamuoa huyo mchumba wake iko siku hao wachawi watamtoa roho au kumfanyia mambo mengine ya kumharibia maisha yake kwa ujumla huyu binti. Kwani kwa maelezo yako Joyceline inaonekana hawa wachumba hawajaookoka (Hawajampokea YESU kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao-maana mwanaume ni mlevi) kwahiyo hawana ulinzi wa MUNGU (Zaburi 34:7, Hesabu 23:23) dhidi ya wachawi. Kwahiyo ni bora huyu mdada akimbie mapema kabla umauti au utaahira haujamkumba toka kwa hao washirikina.
   
 14. fundiaminy

  fundiaminy JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 358
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  rmashauri,niwie radhi pale ntakosea.je? hakijasema kitabu kwamba mke anaweza kumuokoa mume wake katika janga na kwamba anaeolewa na mume ambae hajaokoka basi asimwache bali kwa ukarimu wake anaweza kumgeuza mumewe?kitu kama hicho ila nikipata aya kamili nitakupa.naona si vyema binti amtoroke huyo jamaa.ni maoni tu.
   
 15. M

  Misana Member

  #15
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BUCHANAN - Ni kweli hata takwimu kutoka kwenye kifaa pale muhimbili asilia 47% kati ya 100% ni wanaume wanalea watoto wasio wao, ambao wengi wapo kwenye ndoa.

  Kaka aliebakwa - abaki na msimamo wala asimuoe huyo jini.
  Mchumba - aache ujinga na ang'ang'anie kwa jamaa ukimkosa hutakaa umpate hata wakukwambia shogaako akimtaka.
   
 16. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,460
  Trophy Points: 280
  Joyceline hii siyo story yako ila unatafuta kama maamuzi uliyochukuwa ni sahihi au laa??/
   
 17. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hapana siyo mimi, ni rafiki yangu wa karibu sana , mi ningesema tu kwani nini?
   
 18. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hata mimi nilimshauri asimuache lakini wapi? Jamaa anamuomba sana ametuma hadi wazazi wake, Mama wa kijana kaenda hadi kwa binti mwenye mimba kawapa shua kwamba kijana wake hamuoi huyo msichana, kama ni mimba wataitunza na matunzo yote atayachukua kwake yeye mama siyo kijana, akate mawasiliano na kijana wake, mtoto akizaliwa watapima kama ni wao watamchukua
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Mhh una mastory kweli ya rafiki zako, nakumbuka wewe ndiye muasisi wa mambo ya tiGo .....
   
 20. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #20
  Jun 19, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  daa...jamaa lkn alifwaudu..sasa huyo dada antafute na mie nipate miraha hiyo.
   
Loading...