Ingekukuta hii......

bombu

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,127
542
Ingekukuta hii......

Uko ndani ya "mkoko" boomba kabisa, unamwona binti mzuuuri, unaamua kumpa lifti. Akiwa ndani ya gari binti anapoteza fahamu, unaamua kumkimbiza hospitali, wakati ukisubiri nje unamwona nesi anayemhudumia akija uelekeo wako. Anakupa hongera kwa kuwa binti ni mjamazito. Unamwelewesha kuwa wewe si muhusika, lakini kwa msahangao yule binti anasema kuwa mimba ni yako. Unaomba kupima vinasaba, ambapo kwa mshangao zaidi baada ya vipimo Doctor anakwambia kuwa mbegu zako hazina uwezo wa kutungisha mimba. Unahamaki kwani una mke na watoto watatu.

Je, ungechukua hatua gani?
 
Nakubali mimba ya mrembo na nyumbani sirudi tena,huyu kapenda mimi niwe baba wa huyo mtoto akijuwa sihusiki lakini kule nyumbani afadhali nisirudi naweza kusababisha mauaji,naanza upya.
 
unampa lifti hamfahamiani ghafla mimba yako ...............dah hii nayo kali kuliko
 
hivi kitaalam inawezekana kupima vinasaba kabla mtoto hajazaliwa?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom