PreGE2025 INEC: Ambao hawana changamoto na Kadi zao za 2015 na 2020 wasiende kwenye vituo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
d1c697995f45550a7d7482f2ad0f87cb.jpeg

1742476675607.png
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewakumbusha wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 na 2020 na kadi zao za mpiga kura hazijapotea, hazijaharibika au hawajahama maeneo yao walikojiandikisha awali wasiende kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Aidha Tume imewataka wananchi wa Dar es Salaam wenye sifa za kujiandikisha kuwa wapiga kura, wajitokeze kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura vilivyoko katika maeneo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Tume leo tarehe 19 Machi, 2025 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg Kailima, R. K, uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unahusisha kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania waliotimiza umria wa miaka 18 na zaidi na hawakuwahi kuandikishwa hapo awali.

Tangazo hilo limetaja mambo mengine yanayohusika kwenye uboreshaji wa Daftari kuwa ni kuandikisha wapiga kura ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 siku ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mambo mengine ni kuboresha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine la kiuchaguzi, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura ambao kadi zao zimepotea au kuharibika na kuboresha au kurekebisha taarifa za wapiga kura.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, mpiga kura anaweza pia kuwasiliana na Maafisa wa Tume waliopo katika Kituo cha Huduma kwa Mpiga Kura kwa kupiga simu bure kwenda namba 0800112100.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Mkoa wa Dar es Salaam umeanza siku ya Jumatatu ya tarehe 17 Machi, 2025 na utakumalizika tarehe 23 Machi, 2025.
Tangazo.jpg

Pia soma

~
INEC: Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi au ambaye atafikisha umri huo siku ya uchaguzi ndiye anatakiwa kujiandikisha

~ Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yawataka wananchi wa Dar es Salaam waliojiandikisha kwenye Daftari mwaka 2015 na 2020, kadi zao hazijapotea, hazijaharibika au hawajahama wasiende kwenye vituo
 
Attachments

  • 1742476675607.png
    1742476675607.png
    202.4 KB · Views: 25

Pia soma ~ INEC: Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi au ambaye atafikisha umri huo siku ya uchaguzi ndiye anatakiwa kujiandikisha
no reform no election
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewakumbusha wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 na 2020 na kadi zao za mpiga kura hazijapotea, hazijaharibika au hawajahama maeneo yao walikojiandikisha awali wasiende kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Aidha Tume imewataka wananchi wa Dar es Salaam wenye sifa za kujiandikisha kuwa wapiga kura, wajitokeze kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura vilivyoko katika maeneo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Tume leo tarehe 19 Machi, 2025 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg Kailima, R. K, uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unahusisha kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania waliotimiza umria wa miaka 18 na zaidi na hawakuwahi kuandikishwa hapo awali.

Tangazo hilo limetaja mambo mengine yanayohusika kwenye uboreshaji wa Daftari kuwa ni kuandikisha wapiga kura ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 siku ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mambo mengine ni kuboresha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine la kiuchaguzi, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura ambao kadi zao zimepotea au kuharibika na kuboresha au kurekebisha taarifa za wapiga kura.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, mpiga kura anaweza pia kuwasiliana na Maafisa wa Tume waliopo katika Kituo cha Huduma kwa Mpiga Kura kwa kupiga simu bure kwenda namba 0800112100.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Mkoa wa Dar es Salaam umeanza siku ya Jumatatu ya tarehe 17 Machi, 2025 na utakumalizika tarehe 23 Machi, 2025.

Pia soma

~
INEC: Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi au ambaye atafikisha umri huo siku ya uchaguzi ndiye anatakiwa kujiandikisha

~ Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yawataka wananchi wa Dar es Salaam waliojiandikisha kwenye Daftari mwaka 2015 na 2020, kadi zao hazijapotea, hazijaharibika au hawajahama wasiende kwenye vituo
Wananchi hawafatilii hizi habari, wao wanakuja na kadi zao ilihali hazina shida,
Kujisumbua tu
 
Wanapiga posho tu hakuna la maana, zoezi la kufanya wiki moja nchi nzima linafanywa mwaka mzima, matapeli tupu.
 
Watu wanataka hivyo vikadi tu sio kwa ajili ya kupiga kura
 
Back
Top Bottom