Indonesia: Taifa hatari duniani kusafirisha madawa ya kulevya

Indonesia: Taifa hatari duniani kusafirisha madawa ya kulevya

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,550
Ni taifa lenye idadi ya watu mil 252.8 lina ukubwa wa sq km 1,919,440 na lina idadi ya visiwa 17,508 ndo taifa lenye waislamu wengi kuliko lolote duniani likiwa na idadi ya 86% waislamu na wakristo 8.7%.

Leo hii katika taifa hilo wananyongwa raia 9 kutoka Brazil, Ghana, Nigeria, France na Australia. Wanauawa leo katika jela iliyopo katika kisiwa cha Nusambakapang kwa kupigwa risasi moyoni au kichwani, kosa lao ni kupatikana na madawa ya kulevya aina ya heroin na bangi.

Tayari majeneza yao yameshaandaliwa na ndugu zao wamepewa ruhusa ya kuwatembelea kabla hawajachinjwa kwa risasi, ndugu zao watakuwa nje ya gereza wakisubiri maiti zao baada ya kuwa wameuawa, katika mauaji hayo yupo mwanamke Veloso raia wa Philipines atakayeuawa pamoja na wenzake, mwanamke huyu alibebeshwa heroin bila kujua na ma drug dealers, wanae kila siku wanalia kumuona mama yao, kumuua mtu ambaye hajaua ni ukatili wa ajabu sana, wito umetolewa duniani kuitaka serikali ya Indonesia isitishe mauaji hayo lakini imegoma kabisa.

Huo ni unyama wa hali ya juu kabisa.
 
Ni taifa lenye idadi ya watu mil 252.8 lina ukubwa wa sq km 1,919,440 na lina idadi ya visiwa 17,508 ndo taifa lenye waislamu wengi kuliko lolote duniani likiwa na idadi ya 86% waislamu na wakristo 8.7%.Leo hii ktk taifa hilo wananyongwa raia 9 kutoka Brazil,Ghana,Nigeria,France,na Australia,wanauawa leo ktk jela iliyopo ktk kisiwa cha Nusambakapang kwa kupigwa risasi moyoni au kichwani,kosa lao ni kupatikana na madawa ya kulevya aina ya heroin na bangi,tayari majeneza yao yameshaandaliwa na ndugu zao wamepewa ruhusa ya kuwatembelea kabla hawajachinjwa kwa risasi,ndugu zao watakuwa nje ya gereza wakisubiri maiti zao baada ya kuwa wameuawa,ktk mauaji hayo yupo mwanamke Veloso raia wa Philipines atakayeuawa pamoja na wenzake,mwanamke huyu alibebeshwa heroin bila kujua na ma drug dealers,wanae kila siku wanalia kumuona mama yao,kumuua mtu ambaye hajaua ni ukatili wa ajabu sana,wito umetolewa duniani kuitaka serikali ya Indonesia isitishe mauaji hayo lakini imegoma kabisa,huo ni unyama wa hali ya juu kabisa.

..........walipaswa wapeleke hayo madawa ya kulevya kule kwenye Wakiristo wengi ! Kwani hawajui Waislaam hawaruhusiwi kilevi chochote !? Allah's Glories.JPG

Drug Dealer Pistol.jpg

Bastola ya Dhahabu ya Drug Dealer, ina picha ya Bikira Maria !
 
Duh Indonesia ni balaa.
Mkuu , hapana Indo ' siyo balaa... bali MADAWA YA KULEVYA NDIO MASAYIBU NA BALAA !! maana drugs huangamiza jamii na vizazi vifuatavo, Yaani hata kutibu muathirika mmoja wa madawa haya ina gharimu taifa sii chini ya USD 16,000 ~ 20,000 !! ( yaani kumrudisha muathirka katk hali ya kawaida ) !! kwa lugha ingine fedha hizo zinaweza kutibu wagonjwa wakawaida kati ya 50 hadi 70 na wajawazito 40 na kuwapa matunzo yenye mafao zaidi.......

WARNING:- DRUGS KILL !! wiseboy. Hilo nifundisho kwa wale wenye nia ya kupoteza umma na malengo ya kujitajirisha binafsi!!
 
Last edited by a moderator:
Ila mi naona dunia nzima ingeanzisha kuwapiga risasi tu. Haya madawa yanaharibu sana watu, vijana wengi hupotea na kuharibika. Nchi kama Indonesia ndio zatakiwa, lazima tiwe na msimamo ili dunia ibaki sehemu nzuri. Tukiendekeza haki za binadamu dunia itapotea
 
mwanamke huyu alibebeshwa heroin bila kujua na ma drug dealers, wanae kila siku wanalia kumuona mama yao, kumuua mtu ambaye hajaua ni ukatili wa ajabu sana, wito umetolewa duniani kuitaka serikali ya Indonesia isitishe mauaji hayo lakini imegoma kabisa.

Huo ni unyama wa hali ya juu kabisa.

Watu wanakufa sana kwa sababu ya utumiaji wa madawa ya kulevya..!!!
 
Huo ni unyama wa hali ya juu kabisa.

Wewe tuondolee siasa unafahamu madawa ya kulevya yanaua wangapi duniani?toa uchafu wako lazima wauawe nenda kinondoni ndio utajua madawa yana athari gani.
 
Lolowapi nadhani umemuelewa vibaya wiseboy, anamlilia huyo mama aliyebebeshwa bila ridhaa yake huku akiacha watoto wake.
 
Wewe tuondolee siasa unafahamu madawa ya kulevya yanaua wangapi duniani?toa uchafu wako lazima wauawe nenda kinondoni ndio utajua madawa yana athari gani.
Takwimu-Ukipita manyanya pale kwenye kila watu 10 wapitao kati yao ambao ni 4 ni watumiaji wa madawa (mateja)
 
Issue sio kumuonea huruma huyo mama.issue ni yeye kuhusika na kuua watu kwa njia ya madawa

Indonesia omronyesha njia wengine tuige toka kwao baasi
 
Mbona China nao Hivyo Hivyo peleka sembe uwone kitakacho kusibe
 
Duniani Hakuna Haki!Haya Mataifa Yanayojifanya Kutetea Haki Za Kibinadamu Mbona Mwaka 2014.August Waisrael Wamewaua Wapalestina Zaidi Ya 2000 Tena Katika Kambi Za Wakimbizi Za Umoja Wa Mataifa!Nani Alisema?Au Hao Wapalestina Haki Za Binadamu Haziwahusu? Unafiki Mtupu!.
 
Binadamu bdo ni mkaidi, kila siku kila saa kila dakika watu wanafikiria jinsi ya kuingiza unga huko Indonesia,ukiona sehemu ambayo sheria ni kali ujue sembe ina thamani kubwa sana
 
Ni taifa lenye idadi ya watu mil 252.8 lina ukubwa wa sq km 1,919,440 na lina idadi ya visiwa 17,508 ndo taifa lenye waislamu wengi kuliko lolote duniani likiwa na idadi ya 86% waislamu na wakristo 8.7%.

Leo hii katika taifa hilo wananyongwa raia 9 kutoka Brazil, Ghana, Nigeria, France na Australia. Wanauawa leo katika jela iliyopo katika kisiwa cha Nusambakapang kwa kupigwa risasi moyoni au kichwani, kosa lao ni kupatikana na madawa ya kulevya aina ya heroin na bangi.

Tayari majeneza yao yameshaandaliwa na ndugu zao wamepewa ruhusa ya kuwatembelea kabla hawajachinjwa kwa risasi, ndugu zao watakuwa nje ya gereza wakisubiri maiti zao baada ya kuwa wameuawa, katika mauaji hayo yupo mwanamke Veloso raia wa Philipines atakayeuawa pamoja na wenzake, mwanamke huyu alibebeshwa heroin bila kujua na ma drug dealers, wanae kila siku wanalia kumuona mama yao, kumuua mtu ambaye hajaua ni ukatili wa ajabu sana, wito umetolewa duniani kuitaka serikali ya Indonesia isitishe mauaji hayo lakini imegoma kabisa.

Huo ni unyama wa hali ya juu kabisa.

kaka nimeiona hii leo Bali Nine death row duo facing the firing squad TONIGHT | Daily Mail Online

isome na utaiona mkuu, sasa nauliza huko mjengoni wanang'ang'ania kusaini mambo ya uhuru wa habari, sasa je na hili nilisikia bungeni likizungumzwa, je nalo raisi ataweka sahihi yake au wanawabana waandishi wa habari tu, hilo hatasign
 
Binadamu bdo ni mkaidi, kila siku kila saa kila dakika watu wanafikiria jinsi ya kuingiza unga huko Indonesia,ukiona sehemu ambayo sheria ni kali ujue sembe ina thamani kubwa sana
yaaaa the more wanavyoweka sheria kali tje more sembe inakuwa ghali
 
.. akajasembamba kwa tz ni ndoto hata hyo sheria ikianzishwa sana sana watanyongwa wavutaji tu ila wale wauza unga papa watakuwa wanapeta tu.
We jiulize swali moja tu kwanini serikali inashindwa kusafisha eneo la manyanya kinondoni ambapo ndy kuna ngome kubwa ya wauzaji wadogo na watumiaji wengi wa madawa
Miaka na miaka hakuna kinachofanyika zaidi ya police kja na kuwakimbiza na badaye wauzaji na mateja wanarudi hapo.
 
Last edited by a moderator:
yaaaa the more wanavyoweka sheria kali tje more sembe inakuwa ghali

Ndyo kwenye sheria kali sembe iko juu, ndomana unakuta wale mapunda wenyewe wa nakuambia ah acha tuombe Mungu " akida kwa ndy cha moto atakiona
 
Back
Top Bottom