"Indian school" ni shule ya wahindi?

Mpindo

Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
62
Reaction score
55
Wakuu, maneno mawili ya kingereza hayo kwa tafasili isiyo rasimi ni "SHULE YA KIHINDI". Je! Katika zama hizi bado kuna shule za namna hiyo ambazo ni dhahiri zina viashilio vya ukabila?

Shule hii ambayo ina jina lenye kueleza namna moja tu kwamba kama wewe si mhindi hupaswi kusoma hapo, hata magari yao asubuhi yakibeba wanafunzi ni wahindi tupu wamebebwá na magari yao ya njano, ilipataje usajili hapa Tanzania nchi isiyo na shida na ukabila? Najiuliza, je! Naweza kuanzisha shule nikaiita "HEHE SCHOOL" au "CHAGA SCHOOL" Zama hizi na bado ikapata usajili kwa kusomesha WAHEHE TU au WACHAGA tu?

Ilipate kubaki salama shule hii kipindi chote cha Nyerere hadi sasa kipindi cha Magufuli?
 
Wahindi wanatumia mitaala ya kwao huko walikotoka na walimu wanatumia wa kwao, mitaala yetu ni tofauti na ya kwao, possibly hata quality ya elimu yetu ni questionable labda ndo maana wanaona ni vyema wakawa na shule yao
 
Acha ujinga dogo.... CCM yajenga nchi...
 
Acha ujinga jombaa kitu kidogo kama hiki unashindwa kujiongeza?!

Indian school ni sawa tu na kusema Tanganyika school

India ni Taifa kama ilivyo Tanganyika yetu.

Nimekushangaa sana ulivyoweka mfanano wa taifa la watu na wahehe!
Au unafikiri india kuna kabila moja tu!!?

Ndiyo nyie mdhaniao kila mzungu ni padri au anajua kingereza.
 
Uhindi sio ukabila acha bange
 
Wahindi wanatumia mitaala ya kwao huko walikotoka na walimu wanatumia wa kwao, mitaala yetu ni tofauti na ya kwao, possibly hata quality ya elimu yetu ni questionable labda ndo maana wanaona ni vyema wakawa na shule yao
Ooh!
Kumbe inaweza pia kuruhusiwa mtu akawa na usajili wa shule kwa ajili ya WAHEHE ambapo pamoja na masomo ya kawaida pia katika mitaala yake akafundisha utamaduni wa kihehe, heshima, mila zao na ujasiri wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…