India Yaokoa Maisha ya Watanzania

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11

3916734.jpg

Mojawapo ya majengo ya Hospitali ya MuhimbiliTuesday, January 12, 2010 11:21 PM
WATAALAMU watano wa figo waliopelekwa nchini India kusoma wanatarajia kuwasili nchini mwishoni mwa mwezi huu tayari kutoa matibabu kwa wagonjwa mapema mwezi Februari mwaka huu.Mkuu wa kitengo cha figo cha Hosptali ya Muhimbili Dk. Linda Ezekiel ameiambia Nifahamishe.com kuwa kurudi kwa wataalamu hao kutapunguza msongamano wa wagonjwa pamoja na kuondoa gharama za matibabu ya kwenda nje ya nchi.

Alisema shughuli zitakazofanywa na wataalamu hao ni pamoja na kuanza kutoa huduma ya matibabu ya kubadilisha figo na damu.

Pamoja na huduma hizo pia kutakuwa na upasuaji wa kutoa jiwe katika figo, kusafisha maji ambayo yatakuwa yakitumika kuwawekea wagonjwa wa figo ili kutoa sumu mwilini.

Dk. Linda alifafanua kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho hapa nchini kunalifanya taifa kupiga hatua kwa kupata wataalamu watakaosaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Dk. Linda aliongeza kuwa, kituo hicho kina mashine nane za kisasa kwa ajili ya kusafisha figo na kwamba kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 42 kwa juma kutokana na zamu tatu za kuwahudumia wagonjwa.

Dk. Ezekiel alizitaja dalili anazopata mgonjwa wa figo kuwa ni kuugua shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari, maumivu makali ya misuli katika pande zote za mwili pamoja na kupata maumivu chini ya fumbatio.

Aidha alieleza kuwa ongezeko la maabara za upimaji katika mikoa imesaidia kutoa huduma kwa wagonjwa wa figo na pia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali mbalimbali.

Hata hivyo alifafanua kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kuokoa maisha ya watu bado kuna wananchi waishio vijijini wanaosisitizwa kufika katika zahanati kwa ajili ya kupima afya zao

Hata hivyo katika hospitali hizo kuna mpango maalumu wa kuelimisha madaktari wasaidizi jinsi ya kutibu magonjwa sugu ili kwenda sambamba na kuyadhibiti magonjwa hayo.
 
Back
Top Bottom