India: Wengine 'waliomvua nguo' Mtanzania mbaroni

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Washukiwa zaidi wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini India kuhusiana na kisa ambapo mwanafunzi Mtanzania alipigwa na kuvuliwa nguo mjini Bangalore.

Washukiwa wengine wanne wamekamatwa na kufikisha tisa, jumla ya washukiwa wanaozuiliwa na polisi.
Maafisa watatu wa polisi pia wamesimamishwa kazi, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Watatu hao wanatuhumiwa kukataa kupokea malalamiko kuhusu kushambuliwa kwa mwanafunzi huyo wa kike wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake wa tatu.

Balozi wa Tanzania nchini India John WH Kijazi anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya ndani ya jimbo la Karnataka.

Baadaye, atakutana na wanafunzi waliodhalilishwa karibu na chuo chao.
Maafisa wawili kutoka afisi ya wizara ya mambo ya nje ya India wataandamana na balozi huyo.
Kisa cha kushambuliwa kwa wanafunzi hao kimeshutumiwa vikali na serikali ya Tanzania ambayo imeitaka India kuhakikisha usalama wa wanafunzi wanaoishi na kusomea humo.

Watanzania mtandaoni pia wamekuwa wakishutumu kisa hicho na kuitaka serikali kuchukua hatua.
Tangu kutokea kwa kisa hicho, wanafunzi wengi kutoka Tanzania wamekuwa wakihofia usalama wao.

CHANZO: BBC
 
Visa na mikasa kwa wanafunzi wa Tanzania Nchini India havianja juzi wala jana vipo siku nyingi sana isipokuwa hiki kimeshika wengi kutokana na kuripotiwa na vyombo vya habari, wakati Waziri Membe akitawala wizara hiyo alitumia visa hivyo kama dili la kujipatia pesa kwa kuunda tume kisha kuvuna posho hakuwahi kukemea kwa nguvu ndiyo maana vimeendelea hadi sasa, ni wakati Serikali imfikuze balozi wa India na kumrejesha balozi wa Tanzania aliyepo India angalau itawaamsha wazinduke na kuilipa fidia familia ya huyo Kijana huku ikiwa ni fundisho kwa Nchi zingine zenye Tabia mbovu kwa wageni hususani Watanzania.
 
Back
Top Bottom