INDIA: Kijana mmoja auawa kwa kumiliki farasi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Kijana mmoja mkulima kutoka watu wa tabaka la chini India - la jamii ya Dalit - amepigwa hadi kufa kwasababu anamiliki na kumuendesha farasi

Police katika jimbo la Gujara wanasema kuwa wanaume watatu kutoka tabaka la juu wametiwa nguvuni ili wahojiwe kuhusiana na kisa hicho.

Baba yake marehemu anasema kijana wake huyo alikuwa ameonywa asimuendeshe farasi huyo kwasababu watu matajiri wa tabaka la juu nchio wanaopaswa kuendesha farasi.

Umiliki wa farasi unaangaliwa kama ishara ya mamlaka na utajiri katika baadhi ya maeneo ya India.

Afisa wa ngazi ya juu wa polisi amesema hakuna sababu nyingine ya kuuawa kwa mtu huyo iliyobainika.

Kijana huyo Pradeep Rathod, mwenye umri wa miaka 21, alipatikana akiwa na majeraha makubwapamoja na damu karibu na kijiji cha Timbi katika jimbo la Gujarat Alhamisi usiku .

Farasi wake alipatikana kando yake akiwa ameuawa pia, alisema baba yake marehemu.

Katika malalamiko yaliyowasilishwa kwa polsi, baba yake marehemu alisema mwanae alipenda sana farasi na alikuwa amemnunulia mmmoja.

"Mapenzi ya mwanangu ya farasi yamemsababishia kifo chake," alisema baba yake kulingana na taarifa ya shirika la habari la AFP, ambalo lilishuhudia taarifa hiyo.

'' karibu wiki moja iliyopita, nilipokuwa ninaendesha farasi pamoja na kijana wangu, mmoja wa watu kutoka jamii ya tabaka la juu la Kshatriya alituonya tusiendeshe tena farasi kijijini.

"Alisema kwamba watu wa jamii ya Dalit hawawezi kuendesha farasi , ni watu wa jamii ya Kshatriyas wanaoweza kuendesha farasi.

Pia alitishia kutuua ikiwa hatutamuuza farasi ," ilieleza taarifa ya mashtaka ya baba yake marehemu''.

India ina historia ya mashambulio na ubaguzi dhidi ya watu wa jamii ya Dalit, ambao zamani waliitwa "wasio guswa", ameeleza mhariri wa BBC wa masuala ya Asia Kusini Anbarasan Ethirajan.

Mwezi Oktoba mwaka jana Jayesh Solank kutoka jamii ya Dalit aliuawa alipokuwa amehudhuria densi ya kitamaduni ya jamii ya Hindu katika jimbo hilo la Gujarat.

Ubaguzi wenye misingi ya tabaka ni kinyume cha sheria nchini India lakini bado umeshamiri kote nchini humo.
 
Kazi ya ubaguzi huwa ni endelevu, haina mwisho iko kama ibada. Kujiona wewe ni bora kuliko mwingine ni upumbavu usiotibika, hapa ndipo ubinafsi na choyo unapolelewa, unakuzwa na kuzaa chuki baadae mauwaji. Bahati mbaya tabia hizi za kishetani huwa hazifi haraka ndani ya jamii husika na zina ambukiza kama kisonono, si mnawakumbuka wale weusi wenzetu wa SA baada ya kubaguliwa na wazungu na kuuwawa kwa miaka mingi sasa na wao wameanza kubagua na kuwa weusi wenzao hasa wageni.

Jilindeni na ubinafsi na choyo hizi ni dhambi zinazoleta mauti na utengano kwenye jamii. Mwone mwenzako kuwa bora na mwenye heshima/mkuu kuliko wewe, mpende adui yako na juu ya yote uwe na hofu ya Mungu, hapa ndipo ilipo dawa ya ubaguzi.
 
India ina maendeleo sana ila ina mambo ya kipuuzi na kipumbavu!
kama mtu anaweza kununua farasi kwa nn asimiliki? wangeoanga bei ya farasi ili iwe ngum kwa maskini kununua
 
Kazi ya ubaguzi huwa ni endelevu, haina mwisho iko kama ibada. Kujiona wewe ni bora kuliko mwingine ni upumbavu usiotibika, hapa ndipo ubinafsi na choyo unapolelewa, unakuzwa na kuzaa chuki baadae mauwaji. Bahati mbaya tabia hizi za kishetani huwa hazifi haraka ndani ya jamii husika na zina ambukiza kama kisonono, si mnawakumbuka wale weusi wenzetu wa SA baada ya kubaguliwa na wazungu na kuuwawa kwa miaka mingi sasa na wao wameanza kubagua na kuwa weusi wenzao hasa wageni.

Jilindeni na ubinafsi na choyo hizi ni dhambi zinazoleta mauti na utengano kwenye jamii. Mwone mwenzako kuwa bora na mwenye heshima/mkuu kuliko wewe, mpende adui yako na juu ya yote uwe na hofu ya Mungu, hapa ndipo ilipo dawa ya ubaguzi.
Ahsante kwa tafakuli nzuri. Ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu ukianza.....
 
India Ni full vituko yan mpaka wao kwa wao wanabaguana yan full ubaguz WA Hali ya juu
 
Ubaguzi wa India wa caste system ni mbaya sana. mbaya zaidi wengi wa hao dalit ni wale weusiweusi.
 
Yaani mi ningekuwa ndo miongoni mwa hao wadalit hao wanyanyasaji ningedeal nao perpendicularly hata kwa kuamsha hamasa kwa vijana wenzangu. Unyanyasaji wa kipumbavu sana huu
 
Back
Top Bottom