Inawezekanaje mwekezaji azuie maji ya mto kisha awauzie wazawa?

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
WAZIRI wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, amelaumiwa na uongozi wa KanisaKatoliki Jimbo la Iringa kwa kushindwa kuingilia kati mgogoro wa maji uliopokati ya mwekezaji wa mashamba ya mpunga Mbarali na Shule ya Sekondari ya Kilimoya Montfort ambayo inauziwa maji ili kuweza kulima.

Kuibuliwa kwa tuhuma hizo zilizoelekezwa moja kwa moja kwa Waziri Maghembekunafuatia barua kadhaa zilizoandikwa kwenda wizarani na uongozi wa kanisa hilona ule wa shule hiyo pasipo kujibiwa na serikali licha ya uwekezaji wa kanisaulilenga zaidi kuwaendeleza vijana.

"Bado tunaumizwa sana na suala la maji, tumeipigia sana magoti serikali iliitusaidie tupate maji ya kutosha. Shule yetu ni ya mchepuo wa kilimo,ilisajiliwa tukijua kuwa tutalima kwa vitendo baada ya kujiridhisha kuwa majiyapo, tangu apewe mwekezaji ameamua kutuuzia maji," alilalamika Mkuu wa Shulehiyo, Ansgar Kigane.

Kigane alisema kuwa tangu shule hiyo ilipoanzishwa miaka 25 sasa imefanyavizuri sana kwenye masomo ya kilimo kutokana na upatikanaji wa maji uliokuwa ukitolewana Shirika la Kilimo na Chakula (NAFCO) kabla ya kubinafsishwa.

"Kwa kuwa shule yetu ni ya kilimo hasa mpunga na kwa kuwa wanafunzi waliwezakulima na kupata mavuno ya kutosha ilikuwa rahisi kwao kupata chakula bureshuleni, sasa hali imekuwa ngumu, mwaka huu imebidi tununue maji kutoka kwamwekezaji kwa masharti magumu," alisema.

Alibainisha kuwa licha ya jitihada kubwa za kuiomba Wizara ya Maji iingiliekati ili kuona uwezekano wa shule hiyo kupata maji kwa kupitia mfereji mdogoulioruhusiwa wakati wa NAFCO, lakini wamekosa majibu sahihi.

Ofisa Maji Mkuu wa Bonde la Rufiji ambao ndio wenye mamlaka ya kusimamiamaji katika Bonde la Usangu, Idrissa Msuya alisema kwa mujibu wa sheria yamaji, mwekezaji aliyepewa kibali cha kuyatumia haruhusiwi kuyauza na kwambamakubaliano yaliyofikiwa ni uamuzi wa pande mbili ambazo haziihusu mamlakahiyo.

Msuya alisema kuwa mvutano huo wa maji umefumuka baada ya serikalikubinafsisha mashamba ya NAFCO kwani huko nyuma hali haikuwa hivyo na kwambamamlaka hiyo imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuleta suluhu ila anashangaa kwaninihawakubaliani.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa, katika baruazake amekuwa akifanya jitihada kubwa za kuipigia magoti serikali ili iwezekuiruhusu shule hiyo ipewe kibali cha kutumia maji kutoka kwenye mfereji waumma uliojengwa na serikali.
 
:A S 39:Wazir mwenyewe ni Pro Magembe kati ya Mawaziri Watalii kwenye baraza la JK ni huyu bwana kila wizara hafiti ameshazunguka kila Wizara lakini kote hamna nafuu,kote ni taabu tupu,hawezi kuwasaidia hata iweje
 
Hakuna kitu kinachiudhi kama wazawa kunyanyaswa na wawekezaji kwa namna yoyote ile! Eti tunauziwa maji na mwekezaji! Aaah! Bas itu!! Ngoja ninyamaze kwani kutukana sio hulka yangu!
 
KIla mtu na lwake tusipotia maji nywele wawekezaji watatufanya chochote watakacho Kwa ruhusa ya serikali ya CCM
 
Back
Top Bottom