Inawezekanaje mtu kusema ameolewa bila kufunga ndoa na mwanaume?

Mi naona huo ni upuuzi tu, na wala siwezi kujisema hata siku moja. Yaan siwezi kujipa promo la kipuuzi kwanza huko ni kujizibia ridhiki tu.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya ndoa 1971 kuna kitu kinaitwa dhaanio la ndoa (presumption of marriage) hii hutokea wapenzi wanapoishi chini ya paa moja kwa zaidi ya miaka miwili na kupelekea jamii kuwachukulia kama mume na mke.

NB. Dhaanio hili huweza kupingwa.
 
Labda kwa wanavyotafsiri wao maana ya ndoa ni tendo na si kuvaa shela wala suti
 
Hakuna ndoa hapo BT, bali mrembo anaogopa upweke
na anafurahia gegedo hivyo ni lazima ajisemeshe yumo ndani ya ndoa kumbe ni kimada tu!

Habari zenu,

Hivi mtu anaposema ameolewa lakini hajafunga ndoa ana maana gani?

Hii ni ndoa ya namna gani?

Naomba mnieleweshe maana naona uzee huu unanifanya nisielewe mengi ya mjini, halafu muhusika alivyovurugwa nikimuhoji sana anashusha kichambo na povu tu.
 
Mwanamke ukiishi na mwanaume miezi sita mnakuwa mke na mme hata kama hamjafunga ndoa ....
Hii tabia yakiswahili sana miezi sita nalipia chumba ili nisiwe nakupeleka hoteli i dont mean nataka mke njoo tu hamia si utapika na k utanipa nnavotaka let me take advantage skuowi hata malaika washuke ....tena kwenu wanaridhia kabisa wanajua uko kwa bwanako this bulshit inawashushia tu hadhi .........
 
Habari zenu,

Hivi mtu anaposema ameolewa lakini hajafunga ndoa ana maana gani?

Hii ni ndoa ya namna gani?

Naomba mnieleweshe maana naona uzee huu unanifanya nisielewe mengi ya mjini, halafu muhusika alivyovurugwa nikimuhoji sana anashusha kichambo na povu tu.
tatizo wabongo mmekalilishwa vyeti kwa kila kitu, kwani mababu zako waliishije, afu enzi hizi hakuna upendo mtu anafunga ndoa akili yote kwenye miradhi
 
Halafu ukitaka kumuoa anadai ameshaolewa kweli kuna watu wanaakili za ajabu
 
Kuna ndoa za aina tatu ninazozijua
1. ya kimila. Hii ni makubaliano yako na mwanaume yenye Baraka za wazazi na jamii nyingine inayokuzunguka.
Mume akishamaliza kutoa mahari anakabidhiwa mke.
Hizi ndio nyingi zaidi kwa Maisha tuliyonayo

2. Ya kiserikali.
Mnaenda bomani mnaunganishwa kwa viapo vyenu.
3. Ya kidini.
Muunganiko unaanzia nyumbani mpaka kanisani au msikitini.
Huwa inahyshisha pia Vyeti Vya kiserikali.

Ninachoshangaa ni watu kujifanya hawajui ndoa za kimila wakati Ndio watu wengi kwenye jamii zetu wanaziishi na kudumu.
Hizi zingine watu huwa wanafuata Vyeti tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wengi wamezaliwa kwenye ndoa hizo.wazazi waliona kwa ndoa za kimila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom