Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,920
Kwanza fahamu kuwa kama hujaona jambo au tukio fulani haimaanishi kuwa haliwezi kuwepo au kutokea
Maisa yana safari ndefu sana
Wakati mwingine ni fupi pia
Inategemea tu ni kwa kipimo kipi unayapimia hayo maisha
Kuna watu wamewahi kuishi maisha "mazuri" sana na baadae maisha "yakaharibika" na wakajiaminisha kuwa hayawezi kurudia tena
Wengine walikuwa na maisha "magumu" sana na wamekuja "kufanikiwa" na wanajiaminisha hawawezi kurudi tena chini
Kuna wengine wamewahi kupitia halizote kwavipindi zaidi ya kimoja na hawaamini katika chochote yaani kurudi au kubaki walipo
Hayo yote ni maisha na hizo ni fikra tu na zitabaki kuwa hivyo na mtu kufikiri chohcote hakukifanyi anachofukiria kuwa kweli,yanayotokea ndio yanayoweza kuangaliwa zaidi kwa uthibitisho
Kwenye mapenzi au mahusiano nako ni hivyo hivyo
Kuna waliotendwa na kujiaminisha kuwa hawawezi tena kupendwa au kupata wenza waaminifu na wamefikia hatua na kudhani kuwa fikra zao ndio hali halisi na wameamua kuzifanya kuwa ndio maisha yao
Watu hawa wamejikuta wakiishi maisha ya ajabu sana,wanaweza kupata mwaminifu lakini kwakuwa wameshajiaminisha kuwa hakuna mwaminifu hata huyu nae watamuona vile vile tu
Watu hawa wanaishi kwenye dunia ya kufikirika,yaani haipo
Nasema haipo kwasababu dunia tunayoishi haijawahi kuwa na watu wa aina moja wenye mtazamo mmoja tu,haijawahi na haitakuja kutokea kwasababu maisha yatakwama tu
Hakuna maisha ya mtazamo mmoja kwani hayo hayatakuwa maisha,maisha ili yaende ni lazima kuwe na challenge za kimawazo
Hakuna mahali ambapo watu walikosa changamoto na wakaendelea,hata sisi binadamu changamoto za kutaka kuwasiliana,kusafiri,kujitibu n.k ndizo zimefanya leo tupo hapa tulipo,kutaka maisha ya aina moja ni kujikinza kuliko pitiliza
Huna haja ya kushindana na hali halisi bali wewe jitahidi kwa uwezo wako kuishi maisha ya furaha kadri uwezavyo kwani ukiamua kuwa na kisirani kwasababu umetendwa haubadilishi ukweli
Ukiamua kuishi kwa kuwachukia watu wa jinsia tofauti na yako eti kwasababu mmoja wao amekutenda haubadilishi ukweli kuwa wapo wema na wataendelea kuwepo tu
Wabaya wapo ili ubora wa wema uonekane
Hebu amka sasa!

Last edited by a moderator: