Mbochong'a
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 759
- 1,293
Habari wakuu.
Moja kwa moja kwenye mada. Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imekuwa mwiba mchungu kwa chama cha demokrasia na maendeleo kwa kufanyiwa visa tofauti tofauti nadhani wote tunavifahamu. Sio siri chama kikuu cha upinzani kinapitia wakati mgumu sana imefikia hatua wananchi wameshakata tamaa na kusema wabunge wa chadema hawatarudi tena bungeni.
Lakini kwa upande wangu mimi naona hata wana CCM wenye chama chao wanapata maumivu pia. Kwa sababu ya mambo mbalimbali wanayoyapitia sanasana kwenye angle ya uteuzi. Rais amekuwa mwepesi sana kuwateuwa wapinzani waliohamia CCM kuliko wabunge wa CCM kwenye nafasi za unaibu waziri.
Walioteuliwa unaibu mpaka sasa ni Mwita na Mollel.. Hii inatengeneza maumivu makali sana kwa wabunge wa CCM ambao wapo wengi sana na wenye vigezo. Japo hawataonesha waziwazi wanavyoumia but kisaikolojia hawatakuwa vizuri.
Wengine ambao wanaumizwa na teuzi ni UVCCM na baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya wilaya na mkoa. Hawa ni kama wamesuswa hivi kwenye teuzi za ukuu wa wilaya, mkoa, ukatibu mkuu, u-RAS n.k. Watu kama Mosses Machali, Julius Mtatiro, Katambi, Kafulila, Mghirwa, Pro. Kitila Mkumbo na wengine wameteuliwa wakitokea upinzani. Hii inapelekea baadhi ya wanachama wa CCM kuumia japo hawataonesha lakini lazima ari ya kufanya kazi ipungue kwa namna moja au nyingine.
Kwa hiyo nichukuwe fursa hii kuwapa pole sana CHADEMA na baadhi ya wana CCM kwa magumu mnayoyapitia katika awamu hii ya tano. Vumilieni tu, kwenye maisha lazima kuwe na mapito ya ugumu na changamoto za hapa na pale. Komaeni bila kuchoka wakati wenu wa kufurahi utafika tu. Kwa maana kila lenye mwanzo halikosi mwisho.