Inawezekana maumivu wanayopata CHADEMA awamu hii yakawa sawa na wanayopata wana CCM vindakindaki!

Mbochong'a

JF-Expert Member
May 2, 2011
759
1,293
Habari wakuu.

Moja kwa moja kwenye mada. Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imekuwa mwiba mchungu kwa chama cha demokrasia na maendeleo kwa kufanyiwa visa tofauti tofauti nadhani wote tunavifahamu. Sio siri chama kikuu cha upinzani kinapitia wakati mgumu sana imefikia hatua wananchi wameshakata tamaa na kusema wabunge wa chadema hawatarudi tena bungeni.

Lakini kwa upande wangu mimi naona hata wana CCM wenye chama chao wanapata maumivu pia. Kwa sababu ya mambo mbalimbali wanayoyapitia sanasana kwenye angle ya uteuzi. Rais amekuwa mwepesi sana kuwateuwa wapinzani waliohamia CCM kuliko wabunge wa CCM kwenye nafasi za unaibu waziri.

Walioteuliwa unaibu mpaka sasa ni Mwita na Mollel.. Hii inatengeneza maumivu makali sana kwa wabunge wa CCM ambao wapo wengi sana na wenye vigezo. Japo hawataonesha waziwazi wanavyoumia but kisaikolojia hawatakuwa vizuri.

Wengine ambao wanaumizwa na teuzi ni UVCCM na baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya wilaya na mkoa. Hawa ni kama wamesuswa hivi kwenye teuzi za ukuu wa wilaya, mkoa, ukatibu mkuu, u-RAS n.k. Watu kama Mosses Machali, Julius Mtatiro, Katambi, Kafulila, Mghirwa, Pro. Kitila Mkumbo na wengine wameteuliwa wakitokea upinzani. Hii inapelekea baadhi ya wanachama wa CCM kuumia japo hawataonesha lakini lazima ari ya kufanya kazi ipungue kwa namna moja au nyingine.

Kwa hiyo nichukuwe fursa hii kuwapa pole sana CHADEMA na baadhi ya wana CCM kwa magumu mnayoyapitia katika awamu hii ya tano. Vumilieni tu, kwenye maisha lazima kuwe na mapito ya ugumu na changamoto za hapa na pale. Komaeni bila kuchoka wakati wenu wa kufurahi utafika tu. Kwa maana kila lenye mwanzo halikosi mwisho.
 
Maendeleo hayana chama

Mimi nafurahi Rais Magufuli haangalii chama ila anaangalia utendaji wa mtu

Hata USA hawaangalii mambo ya vyama kwenye uteuzi
 
Chadema haiwezi kusikia maumivu kwenye uteuzi maana haiwahusu.

Maumivu yao yako kwenye kubambikwa makesi, kuteswa, kupigwa risasi, kuondolewa kwenye nafasi walizo chaguliwa na wananchi kwa mbinu chafu na kuzuiwa kufanya kazi zao za siasa kwa mujibu was katiba.

Uchaguzi 2020 inahitajika Tumehuru ya uchaguzi ili hata kama CCM inashinda ishinde kwa haki.

Kama njama za uchaguzi zitafanikiwa na upinzani utamalizwa kwa kupangwa mamluki basi jambo moja kubwa sana litatokea nchi hii, nalo ni VIKUNDI VYA UGAIDI NA UASI kuanza kutumika.

Leo tunacheka na kudharau lakini matendo kama ya Boko haram na Alshabab yanavyo athiri huko waliko wananchi wanafahamu.

Magaidi kutega Bomu Kariakoo ili kuikomesha serikali bila kujali maisha ya watu sio ajabu.

Wala kuchapwa risasi mwanasiasa hadharani tena mchana (mfano Makonda kwa Dar) sio matukio mageni hata kidogo.

Sasa wanaccm furahini tuu demokrasia kupotezwa na kujiona nyie miamba, cha moto mnakitafuta.
 
Sent using Jamii Forums mobile app

Upinzani hauwezi kumalizwa Tanzania ila tunataka Wapinzani wanaojielewa, Wapinzani Wazalendo km Nccr mageuzi Sio hawa wahuni wa ufipa

Hatutaki siasa za Upinzani km Chadema wanaowaabudu muzungu

Ndio maana tumesema mwisho wa Chadema ni October na sio mwisho wa upinzani

Na Kwanini Chadema mnapenda sana ugaidi ? Mnadhani mtafanikiwa hata robo? Mliyekuwa mnamtumia kwenye mikakati hiyo Lwakatare mmeshamfukuza mudo wote atamwaga siri za Chadema
 
Mi naona bora hata hawa wapinzani wanaumia lakini wanaongea kutoa madukuduku yao rohoni...

Hawa wa CCM unatumbuliwa afu eti unatakiwa utabasamu machoni wakati moyoni kuna machozi..

Kuwa ndani ya CCM kwa sasa ni kama kuishi gelezani...kumfurahisha mtu mmoja afurahi kila mara ili uwe na uhakika wa kesho yako si kazi ndogo aisee...
 
Kusema hayana chama ni sahihi, lakini kwa kinachofanywa na Rais kuteuwa wapinzani kinapunguza ari na ufanisi wa wanachama wakongwe wa chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema haiwezi kusikia maumivu kwenye uteuzi maana haiwahusu.

Maumivu yao yako kwenye kubambikwa makesi, kuteswa, kupigwa risasi, kuondolewa kwenye nafasi walizo chaguliwa na wananchi kwa mbinu chafu na kuzuiwa kufanya kazi zao za siasa kwa mujibu was katiba.

Uchaguzi 2020 inahitajika Tumehuru ya uchaguzi ili hata kama CCM inashinda ishinde kwa haki.

Kama njama za uchaguzi zitafanikiwa na upinzani utamalizwa kwa kupangwa mamluki basi jambo moja kubwa sana litatokea nchi hii, nalo ni VIKUNDI VYA UGAIDI NA UASI kuanza kutumika.

Leo tunacheka na kudharau lakini matendo kama ya Boko haram na Alshabab yanavyo athiri huko waliko wananchi wanafahamu.

Magaidi kutega Bomu Kariakoo ili kuikomesha serikali bila kujali maisha ya watu sio ajabu.

Wala kuchapwa risasi mwanasiasa hadharani tena mchana (mfano Makonda kwa Dar) sio matukio mageni hata kidogo.

Sasa wanaccm furahini tuu demokrasia kupotezwa na kujiona nyie miamba, cha moto mnakitafuta.
Hivyo vitu ulivyoandika kufanyiwa kwa Chadema vyote nime summarize kwenye first paragraph. Nimemaanisha hata baadhi ya wana CCM nao wanayapata hayo maumivu kwa namna moja au nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani hauwezi kumalizwa Tanzania ila tunataka Wapinzani wanaojielewa, Wapinzani Wazalendo km Nccr mageuzi Sio hawa wahuni wa ufipa

Hatutaki siasa za Upinzani km Chadema wanaowaabudu muzungu

Ndio maana tumesema mwisho wa Chadema ni October na sio mwisho wa upinzani

Na Kwanini Chadema mnapenda sana ugaidi ? Mnadhani mtafanikiwa hata robo? Mliyekuwa mnamtumia kwenye mikakati hiyo Lwakatare mmeshamfukuza mudo wote atamwaga siri za Chadema
Wapinzani wanaojielewa ni wale wanaompongeza na kumsifia Rais sio!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi naona bora hata hawa wapinzani wanaumia lakini wanaongea kutoa madukuduku yao rohoni...

Hawa wa CCM unatumbuliwa afu eti unatakiwa utabasamu machoni wakati moyoni kuna machozi..

Kuwa ndani ya CCM kwa sasa ni kama kuishi gelezani...kumfurahisha mtu mmoja afurahi kila mara ili uwe na uhakika wa kesho yako si kazi ndogo aisee...
Yaani kuwa CCM ukishatumbuliwa ni sawa na kujifunika shuka moja na nyoka. Wanapitia wakati mgumu sana. Wanajuta haki ya Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom