Sasa hivi wakati ccm bado wako madarakani sahau. Kama unabisha, jaribu kumpa paka kipande cha nyama, halafu akianza kula msogelee ukitaka kukichukua kipande kile ili umgawie paka mwingine ambaye ndio kwanza katokea kutoka porini, utasikia music. Hata mbwa wana hulka hiyo. Music utakaousikia ndio sawasawa na ule ccm watakaoutoa kwako kama unataka kurudisha mali za wananchi kwa wananchi ambao kusema kweli ndio walioikabidhi ccm wakati wa chama kimoja. Ili kukipata kipande hicho bila bughudha, mwondoe paka huyo kwa style yoyote halafu kichukue kipande na kukifanya utakavyo.
Damu iliyokuwa inaimbiwa kumwagika wakati wa kampeni, nyingi ilimwagwa na mashabiki wa ccm, lakini kwa kuwa wapinzani hawana visemeo vya uhakika kujitetea wakageuziwa kibao na wao sasa wakaonekana wanamwaga damu. CCM atakapokuwa KANU au ZANU ndipo wataweza kuelewa unachosema. Hata ukiwapeleka mahakamani kwa sasa watatetewa tu. Humsikii Chenge anamponda SITTA kwa sababu ati aliachia mafisadi waanikwe hadharani na sasa anadhani yeye atamudu kudhibiti Bunge lisiongelee mambo hayo akiwa speaker? Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.