Inawezekana kweli?

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96
Kwa jinsi CDM JF wing na waungaji mkono wao walivyo na matusi na dharau kwa wenzao kwa kujiona kuwa wao wamesoma zaidi, je hili linawezekana?

DIWANI pekee wa kuchaguliwa katika Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Frank Nyalusi amepingwa mahakamani kuendelea kushikilia wadhifa huo katika kata anayoiwakilisha kwa madai kwamba hajui kusoma na kuandika.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Nyalusi alichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Mivinjeni baada ya kumshinda Raymond Tolage wa CCM aliyekuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka mitano iliyopita.

Katika uchaguzi huo, watu 1,500 kati ya 3,575 katika kata hiyo walipiga kura, huku kura 796 zikienda kwa Nyalusi, kura 680 zikienda kwa Tolage na 23 zikiharibika.

Wakati Nyalusi anawakilishwa katika kesi hiyo na wakili Basil Mkwata, mlalamikaji Tolage anawakilishwa na wakili Alfred Kingwe.

Kesi hiyo iliyokuwa itajwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Iringa mapema wiki iliyopita, itatajwa Aprili 15, mwaka huu baada ya shauri hilo kuahirishwa.

Akizungumza sababu za kuifungua kesi hiyo, Tolage alisema endapo atashinda itawezesha mchakato wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kuvitazama kwa umakini mkubwa vipengele vya sheria za uchaguzi.

“Taarifa nilizonazo zinaonesha kwamba diwani Nyalusi hajui kusoma na kuandika wakati sheria inataka ili uwe diwani ni lazima ujue kusoma na kuandika Kiswahili au Kingereza au lugha zote mbili,” alisema nje ya mahakama hiyo wakati kesi hiyo ikipangiwa tarehe nyingine.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii kama kweli hajui kusoma na kuandika, diwani huyo alisema ukweli juu ya suala hilo utajulikana mahakamani.

“Yeye si kafungua kesi akisema mimi sijui kusoma na kuandika, ukweli huo ataujua mahakamani,” alisema Nyalusi.

Wakati diwani huyo akifikishwa mahakamani, CCM imemshushia tuhuma kwamba anazuia wananchi kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Isakalilo inayojengwa kwa ushirikiano wa kata mbili za Mivinjeni na Isakalilo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Mary Tesha amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo kwa kutumia kamati yake ya nidhamu kumchukulia hatua diwani huyo.

Tesha alisema, hata kama diwani huyo anawakilisha wananchi
 
Back
Top Bottom