inawezekana kubadili operating system ya simu????

djesco

Senior Member
Jun 26, 2013
166
52
wakuu kila siku huwa najiuliza hili swali hivi inawezekana kweli ukabadili operating system ya simu yaani mfano simu yangu inatumia windows kama operating je naweza kubadili na kuweka android!?
karibuni
 
Mkuu ninachojua mimi ili uweze kubadili OS moja ya simu kwenda OS nyingine kwenye simu huwa inategemea sana aina ya kernel, loader na memory architecture ya hizo OS, mfano haiwezekani ukabadili simu ya windows phones OS kwenda Android OS kwa sababu zina kernel na loader tofauti, windows phones OS inatumia windows NT kernel wakati Android OS inatumia linux kernel , lakini kuna OS zinazoweza kuingiliana mfano, simu za Android zinauwezo wa kuingiza Ubuntu mobile OS kwa sababu zote zinatumia kernel ya linux zote, pia kuna fununu kuwa simu ya Nokia N9 ambayo inatumia Meego OS na kernel ya linux iliweza kupokea Android OS. Haya ni mawazo yangu tu, huenda mtu mwingine ana mawazo tofauti na haya na nikawa nipo wrong, wadau watanisahihisha ama kuongeza vitu vingine nilivyosahau
 
Haupo wrong mkuu, hiyo kitu ni kwel, kernel zina matter
 
kaka kuna simu za nokia tatu na ya htc moja hizi zinakua zipo wazi kuingia os yeyote na ikitokea madeveloper wakaport basi zinaingia.

1. nokia n9
2. nokia 950
3. nokia n900
4. htc hd7

kama hii n900 wameshaport kernel ya ios bado kutengeneza gui tu ili hii simu irun ios.

simu hizi zinarun android ukitaka pia.

htc hd7 ndio simu ya windows kama simu yako sio hii itakua ngumu
 
Back
Top Bottom