Inawezekana akampa mwanamke mimba?

Angry Bird

JF-Expert Member
May 3, 2016
514
500
Madoctor, wataalamu na wote mlio na uelewe wa ugonjwa huu naombeni mnipe majibu. Google imeniacha na maswali.

Huyu bwana ameugua kisukari kwa muda mrefu sana, figo zishafail anafanyiwa dialysis mara mbili kwa wiki. Inawezekana akampa mimba mke wake?
 
MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,650
2,000
Madoctor, wataalamu na wote mlio na uelewe wa ugonjwa huu naombeni mnipe majibu. Google imeniacha na maswali.

Huyu bwana ameugua kisukari kwa muda mrefu sana, figo zishafail anafanyiwa dialysis mara mbili kwa wiki. Inawezekana akampa mimba mke wake?
Nguvu za kiume anazo? Anaweza kufanya mapenzi kikamilifu?? Kama majibu ni NDIO, basi anaweza kutia mimba!!
 
Njunwa Wamavoko

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
5,611
2,000
Madoctor, wataalamu na wote mlio na uelewe wa ugonjwa huu naombeni mnipe majibu. Google imeniacha na maswali.

Huyu bwana ameugua kisukari kwa muda mrefu sana, figo zishafail anafanyiwa dialysis mara mbili kwa wiki. Inawezekana akampa mimba mke wake?
Kusafishwa figo haina maana kwamba hauna uwezo wa kutwisha mimba.
Naweza kukwambia tu kwa kifupi Figo haina msaada wowote kwa mfumo wa uzazi.
Ila wagonjwa wengi wanaofanyiwa dialysis wanakua ni wagonjwa kweli kweli na mpaka ufanyiwe dialysis maana yake wewe ni CKD stage 5(stage ya mwisho) na ile Sumu ya Ammonia ambayo utolewa na figo inavyopanda kichwani sidhani kama mtu atakua na mawazo au hata hamu ya kufanya hilo swala.

Upande mwingine wa Sarafu.
Mtu mwenye Kisukari ukiona figo ime fail impression yangu ya kwanza ni kwamba hakuwa ana control sukari vizuri ndo maana amepata Moja ya complication ya kisukari. i.e Diabetic Nephropathy

Kwa hiyo kama ana complication kama hii anaweza kuwa na Complication ya kushindwa kusimamisha Erectyle disfunction ambayo wazee wengine uamua kutumia Viagra bila kushauriwa na daktari na uishia kufia kwenye Vinena.

Hivo hatuwezi jua kama anaweza kusimamisha au lah
akutane na mwezi wake kwenye zile siku za neema na kama hana complication nyingine ya Kisukari ya Ejaculation basi atampa mimba bila shika.

Natambua kukaa na ugonjwa wa kisukari kwa mda mrefu hata kama una control sukari baadhi ya complications zitakuja ila baada ya miaka mingi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom