Quinine Mwitu
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 5,530
- 6,119
Kuna dogo mmoja namfaham brother yake ni rafiki yangu sana,kuna kipindi huyu rafiki yangu akiwa porini kufanyakaz kama hotelia huyu dogo nilibaki nae ghetto,dogo alikua anasoma kwa shida sana,ila dogo alikuwa anajitahid sana kimasomo,alikuwa anasema kua IPO siku maisha yake yatabadilika kupitia elimu,alisoma shule moja Arusha inaitwa kimandolu,Mungu Alimsaidia O level alifaulu vizur akaenda karatu boys,mwaka huu kapata division 1 na kupata chuo UDSM kitivo cha elimu,dogo Jana kanipigia,amekata tamaa sana ni baada ya kugundua kuwa hatapata mkopo baada ya serikal kusema kuwa kama ulisoma private school hutapata mkopo ,ameongea kwa uchungu sana,akasema bro serikali hii naona imenipotezea ramani kabisa kimaisha....daa we acha tu bro! Mbona kila kitu nimefanya poa? Mbaya zaid anadai hakuna protocol yoyote inayozingatiwa bado kuna upendeleo maana kama kigezo ni kuwapa waliosoma shule za kata mbona kuna rafiki yake A level na O level kasoma shule za private na kapiga 100%,Serikali iwe makini katika kulitekeleza suala hili hawa madogo wanapoteza tumaini lao hivhivi,