Mkakati ambao umepangwa hadi hivi sasa na wale mnaoamka nyumbani mtauona kwenye maandishi madogo madogo chini ya vichwa vikubwa vya habari ni ule wa kudai kuwa hawakupewa nafasi ya kujitetea au kusikilizwa.
Mkakati huu utatumiwa na Lowassa (ambaye inadaiwa anajiandaa kujibu mapigo - he won't go down without a fight) na pia ni mkakati ambao Karamagi na Msabaha nao wanataka kuutumia. Kimsingi wanadai wanatuhumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa wakati Karamagi anadai ripoti hiyo ni ya "kisiasa".
Hata hivyo tatizo la mkakati huu ni kushindwa kuelewa Kamati licha ya kuwa na nguvu za kimahakama siyo mahakama. Hivyo badala ya kuleta mashahidi wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi (kama ilivyo mahakamani)ni Kamati inaamua nani aitwe na nani asiitwe na kwanini.
Mojawapo ya tetesi ambazo zinasikika sana ni kuwa RA aliitwa na akakataa. Sijui hilo lina ukweli kiasi gani. Hata hivyo kama Lowassa, Msabaha, Karamagi na waliotajwa wengine hawakupewa nafasi ya kusikilizwa au kuitwa kutoa maelezo kunaweza kusababisha hisia hiyo ya "uonevu" kwani its against the natural justice.
Hii natural justice (haki ya asili) inaonekana katika maandiko yote ya Kikristu na Kiislamu ambapo licha ya Mungu kujua Adam amekosea lakini bado alimpa nafasi ya kujieleza. Hivyo, kati ya dondoo ambazo zitakuwa muhimu sana kujulikana ni kujua nani aliitwa na nani hakuitwa na kwanini. Kuna kipengele kimoja mwanzoni mwa ripoti kinachoashiria (angalau kwa upande wangu) kuwa wote walioitwa kwa summons (subpoena kwa wenzetu US)walienda.
Lakini hapa kuna mtego ambao Mkakati wa kina Lowassa utakwama. Kama mnakumbuka Mwakyembe alitoa wito kwa "mtu yeyote" mwenye maelezo kuhusu Richmond ajitokeze na kuonana na Kamati. Kwenye ripoti hiyo anasema hakuna mtu aliyejitokeza kwa hiari yake (hapa anawabana kina Karamagi, et al).
HIvyo wakija na "hatukupewa nafasi ya kusikilizwa" Mwakyemba atawaambia.. "tarehe... nilizungumza na vyombo vya habari na kutoa wito kwa "mtu yeyote"... hapo ndipo watakapojua kuwa mtego umetegwa aidha watautegua, ama watanaswa!
Usikose kusikiliza maoni yangu kwenye KLH News kuhusu suala hili.
I'm out.. enough excitement for the day!