Inatosha: ‘Academy’ zinatumia Kiingereza kutuzuga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inatosha: ‘Academy’ zinatumia Kiingereza kutuzuga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 16, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Inatosha: ‘Academy’ zinatumia Kiingereza kutuzuga

  Daily News; Tuesday,September 16, 2008 @15:55

  Wakati akiwa Babati mkoani Manyara siku chache zilizopita, Rais Jakaya Kikwete aliwabeza wanafunzi wa shule moja inayofundisha kwa Kiingereza ambao walimwimbia nyimbo za kwaya kwa Kiingereza na Kifaransa na alipowauliza kwa nini hawakuimba kwa Kiswahili wakamjibu kwa kimombo kuwa “We do not know Swahili,” wakimaanisha kwamba hawafahamu lugha hii ya taifa.

  Kwa kumnukuu Rais Kikwete, ingawa Kiingereza ndiyo lugha muhimu duniani Kiswahili kina nafasi ya pekee nchini kwani ndiyo lugha ya taifa na hakipaswi kudharauliwa.

  Alichokisema Rais Kikwete Babati kinaibua upya mjadala wa umuhimu wa lugha hizi mbili – Kiingereza na Kiswahili – katika kufundishia masomo ya shule za msingi na sekondari nchini, hasa katika zile zinazofahamika kama ‘Academy.’
  Kwa jinsi hali ilivyo sifa moja kubwa ya ‘Academy’ hizo ni umahiri wao wa kuwawezesha wanafunzi wake kuwa na uwezo wa kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha tangu madarasa ya chini.
  Sisi hatupingi wazo la kutoa uzito wa pekee katika matumizi ya Kiingereza kwenye shule hizo kwani ndiyo lugha inayohitajika baadaye katika kujifunza taaluma nyingine kama udaktari au uhandisi.
  Kinachotupa tashwishwi ni namna Kiingereza kinavyopewa kipaumbele katika ‘Academy’ kana kwamba ndilo somo pekee linaloweza kumfanya mwanafunzi awe mwanataaluma bora. Kiswahili na masomo mengine yanapewa uzito mdogo au yanawekwa kando.
  Hata hivyo, ukweli ni kwamba dunia tuliyoko sasa ni ya sayansi na teknolojia na kwa sababu hiyo tulitarajia kwamba ‘Academy’ zingekuwa za mfano katika kutoa kipaumbele kwa masomo kama Hisabati na Sayansi badala ya Kiingereza pekee.
  Tunadhani wakati umefika sasa kwa ‘Academy’ na shule nyingine pia kuwa chemichem ya wanasayansi wetu wajao kwa kuwaandaa kwa umahiri kama zilizofanikiwa katika lugha ya Kiingereza. Zikichelea kubadilika zitatuandalia taifa la kesho ambalo linaweza kuwa na mamilioni ya wazungumza kimombo lakini wasio na weledi katika taaluma nyingine yoyote.
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mwandishi, hebu focus kwenye Kiswahili na Kiingereza. Hilo la Hisabati na Sayansi hulijui maana hujalielezea. Watoto kusema hawajui Kiswahili ni kithibitisho kwamba wanawekea Kiingereza kipaumbele kuliko Kiswahili, lakini hilo halisemi lolote kuhusu Hisabati na Sayansi.

  Halafu, hiki kihabari kwenye tovuti ya DailyNews wamekiweka kama "Habari za Kitaifa" wakati hiki ni kimakala uchwara cha mwandishi tu.

  Crummy press!
   
 3. Tonga

  Tonga Senior Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ninakuunga mkono katika hili, pamoja na sifa na matumizi makubwa ya lugha ya kiingereza duniani bado haitupi haki ya kukidharau kiswahili. Kuwa na lugha ambayo unaiita lugha ya taifa ni sifa ambayo sio nchi nyingi zinazo duniani,na zaidi ya hiyo pia tusisahau umuhimu wa lugha zetu za kwanza lugha za makabila(mother tongue) na hizo zinatuongezea umaarufu wa kujivunia kuwa wewe ni mzungumzaji wa lugha zaidi ya moja! Ni watu wengi sana wanatuadmire waafrika kwavile tuna lugha zaidi ya moja, na hilo sio jambo la kuacha lipotee katika vizazi vijavyo kwa ajili ya kasumba ya kingereza, tufundishe watoto wetu kimombo at the same time tuwafundishe kiswahili na lugha zetu za asili.
  Hili linakwenda sambamba na wazazi wanaozalia watoto wao nje ya nchi, huwa najisikia vibaya pale mzazi anapokiri with confidence "Mimi mtoto wangu hajui kiswahili" hili sio jambo la kujivunia bali ni AIBU, kwanini mtoto hajui kiswahili ilhali wazazi wake wote ni waswahili? wewe kama mzazi unazungumza lugha 2 au 3 kwanini unamnyima mtoto wako nafasi ya pekee yakuwa bilingual or multilingual? kama usipompa hii nafasi basi uwe tayari kumlipia akiwa college asome kiswahili as a second/foreign language wakati kwa hakika ni lugha yake ya nyumbani, hatuoni aibu kwa hili? waangalie wanigeria hata wazaliwe wapi wanazungumza lugha yao ya kwanza fluently, tusiache mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu yatupite huku tukikumbatia kasumba ambazo zimeshapitwa na wakati, mtoto anaweza kujifunza lugha zaidi ya moja kwa wakati mmoja na hiyo haimpunguzii umahiri wa lugha mojawapo.
  Let's play our part effectively as parents or guardians and raise our children on the 21 era, and make sure we don't minimize their chances to shine.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  While it is undisputable - at least to sane minds- that Swahili occupies a central position in the fabric of our nation, and rightly deserves not only the right attention but also respect as a formidable and organic language regardless of the historical element, it is equally undisputable that the world economy has no place for a non-world language speaker.

  My fear is, in embracing English medium schools -half baked unregulated ones halfheartedly at that - we are posited in a lose-lose position. The pupils who take pride in their almost nonexistent, "overcontemporarized Spaghetti-Western" English find themselves in a predicament whichby on the one hand they cannot dream of ejaculating some world class Dickensian punditry like yours truly, on the other hand they don't even know who is Amiri Akida Andanenga "Sauti ya Kiza" and Agoro Anduru, let alone Shaaban Robert and "Adili na Nduguze" and I am not even talking about "Mabepari wa Venisi".

  To quote their playbook, they don't got no game, not even a Playstation!

  Time to wake up and instill some discipline, cultivate readership -in both Swahili and English- and cut back on that Multichoice torrent on the idiot box.
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kimsingi nakubali kuwa sayansi ni muhimu ifundishwe vizuri, lakini sijaona ushahihdi kuwa sayansi inafundishwa vibaya kwenye shule za "Academy" at least compared na shule za serikali ambazo zengine hawana practical kabisa.

  Pia hizi ni shule ni private so wazazi wenyewe wanaweza kufanya maamuzi kama itamfaa mtoto wao au la, sioni umuhimu wa serikali kuziingilia sana hizi shule, zaidi ya kuhakikisha some basic standards.
   
Loading...