Inatia Hasira! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inatia Hasira!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mcfm40, Jun 25, 2012.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,142
  Likes Received: 1,780
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wanaJF,
  Nipo hapo Afrika kusini kwa muda sasa. Huwa najiuliza maswali mengi bila kupata majibu ninapokuwa nakatiza mitaa hasa ya Capetown. Miundo mbinu yao hasa barabara flyovers utashangaa.

  Najua makaburu wamefanya kazi kubwa hapa lakini najaribu kulinganisha na kujifargua kwa makufuli na km 11,000 za barabara. Kusema ukweli tanzania hatuna barabara, ni mzaha mtupu!! yaani miaka hamsini ya uhuru rumeshindwa kuweka hata kaflyover kamoja hapo ubungo? miaka hamsini..! Kaflyover Kamoja tu! imekuwa ni siasa tuuu...!

  Fikiria labda kila baada ya miaka kumi tungekuwa tunajenga kaflyover kamoja kwenye makutano ya barabara zetu, tungekuwa mbali sana? Inatia hasira na ni aibu kujisifia bila kufanya ulinganisho hata wa mbali tu na wenzetu! Hata Ethiopia wanatushinda? Kwanza kusema awamu ya nne wamejenga km11,000 kulinganisha na awamu nyingine, ina maana hizo awamu nyingine waliokuwepo madarakani ni CUF au CHADEMA? Si ni nyie nyie CCM? Au mnakubali sera zenu za huko nyuma hazikuwa na mashiko?

  Tunapoitazama CCM tunaitazama kwa ujumla wake tangu uhuru sio katika vipindivipindi. Tunaangalia continuity ya sera na mipango ya CCM katika kutufikisha hapa tulipo! We cannot compartmentalize development!

  Mawaziri wa Kikwete wanajua udhaifu wake ndio maana kila wanapozungumza wanasisitiza yale yaliyoyofanywa na serikali ya awamu ya nne kwa kumtaja Kikwete, bila kuzungumzia yana connection gani na yaliyofanywa na awamu nyingine! Kwa sababu wanajua mengi yaliyoahidiwa hayakutelezwa.

  Kwa hiyo ni muda muafaka sasa CCM na serikali yake iache kujilinganisha na awamu zilizotangulia (thye are the same people) bali wajilinganishe na majirani zetu na nchi nyingine tulizopata uhuru pamoja. Kwamba wao wako wapi na sisi tupo wapi! Hapo ndipo wanaweza kujifaragua kwamba tunaongoza kwa miundo ya barabara. Sio kumlinganisha Kiwete na Mkapa au mwinyi huo ni upuuzi na udhaifu!
   
 2. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Mkuu mie nilitokwa na Chozi.
  Sikuamini Macho yangu OR Tambo Int. Airport na Namna mahoteli yalivyo karibu na Airport.
  Check reli ya Juu kwa juu, Flyovers mkuu hawa CCM ni Washenzxasfdsgh
  Staki kusema Mengi ila Nina Hasira na CCM.

  Nina picha lakini zinakataa kupest.
  SHAME ON YOU -CCM.
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  silly sessions ..silly government...silly party..!
   
 4. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tukubali kupigwa hadi kufa, kupigwa mabomu risasi kama tunataka kuikomboa nchi
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Nchi inahitaji wachapazi na wazawa.
  Nawahakikishia Watanzania kuwa tuna Rasilimali zaidi ya SOOUTHAFRICA ila viongozi wa CCM ni WALAFI zaidi ya SouthAfrica.
  Yamekaa tu bungeni kulala lala utadhani yanaumwa Sleep Apnea
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  I always say,wakati mwingine inaniuma kuzaliwa tanzania,nchi yenye mali asili nyingi kuliko,halafu maendeleo 0!!!nchi hii hii kunawatu hawajui shule ya msingi inafananaje.yaani hawa nyinyiemu,watalipa haya maumivu ya watanzani.naamini ipo siku.
   
 7. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tunafanya feasibility study na kigoma itakuwa kama dubai ndogo.
   
 8. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mapinduzi ya kiffikra yanahitajika kwa watz, kisha nyinyiem iwekwe pembeni 2015. huenda kukawa na mabadiliko. mafisadi wanakera sana tu...........
   
 9. D

  Davie Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  N2 sisi akilizetu zipo mfukoni N2.JPG
   
 10. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135

  UCHUMI WA AFRIKA KUSINI NI ZAIDI YA BILIONI 400 $, na WA KWETU LABDA BILLIONI 50 $! Sasa cha kukushangaza ni nini?

  Unawezaje kulinganisha AK na TZ? kwa kiwango chochote kile?
  Zaidi ya asilimia 90 ya watu wa cape town wana vhoo vya maji (flashed toilets), AK wana makampuni zaidi ya 10 yanayopata zaidi ya Dollar Billioni moja KAMA FAIDA (nikiimanisha baada ya kulipa kodi), Soko la Hisa la AF ni TOP TEN Duniani, SAB Miller ni kampuni kubwa ya ya pili Duniani kwa kuzalisha bia, fedha ya AK rand iko ni moja kati ya currency kubwa duniani, orodaha inaendelea na kuendelea...

  AF wameanza kuexport Almasi dhahabu na madini mengineyo kwa takribani miaka mia sasa (fikiria hapo...), De Beers imezaliwa AF inashikilia 3/4 ya soko la Almasi Duniani....

  Baada ya hayo yote nafikiri unalinganisha vitu visivyolingana. Mimi sio mpenzi wa ccm lkn unaposema tujenge flyovers Dar, napata shida kuelewa kipi ni muhimu, Je ni flyover ya ubungo, au Br ya Iringa -Dodoma? Je ni flyover buguruni au kuunganisha Tabora na mikoa kama Mbeya, mpaka Kigoma na Dar? Naomba unijibu hayo maswali, kumbuka uchumi wetu ni chini ya 50 Bill $!!!!
   
 11. B

  Bob G JF Bronze Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  huku ccm Tunajenga matumbo yetu na zikizidi hela tuna tumia 4 totoz, tena barabara hizo bei yake ni nafuu kuliko za chini, tabu hatuna Mipango si siasa 2 na porojo za majitaka na masifa hewa
   
 12. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Kijakazi,
  CCM siyo watu wa kuunga mkono hata kidogo.
  With time tunaweza kuwa South Africa lakini si Tabia hii tunayoiendekeza.
  Nasema haya kwa sababu mimi nimeenda nara kadhaa afrika kusini, Ni sehemu chache zina Mataa zaidi ya hapo kuna FLYOVERS lakini pia Barabara zote zilizo na hadhi ya kuaitwa N kwa maana ya National Road ni bora sana na hazina manundu kama ya hii ya juzi juzi Kilwa road.
  hata hicho kidogo tunachopata tunapeleka wapi??
   
 13. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  I am speechless
   
 14. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Kama umenisoma vizuri mimi siungi mkono CCM au chama chochote kile kwa sasa kwa maana mpaka sasa bado sijashawishiwa na chama chochote kile lkni hiyo ni mada nyingine!

  Nakubaliana na wewe kabisa kwamba hicho kidogo tunapeleka wapi hapo ndio pa kuanzia ninachopinga mimi ni pale mtu anapotaka kulinganisha AK na TZ kwa ngazi yoyote ile haiwezekani, HATULINGANI!!! na pia sio fair kwa maana mnalinganisha visivyolingana na NA HUO NDIO UKWELI! kuendelea kupingana nao ni kujidanganya na kujiumiza bure kama mtoa hoja alivyodai, lkni ukilielewa hilo basi utaishi vizuri na labda ningeshauri jaribu kubadilisha unapoweza hata kama ukiweza kujitolea kumfundisha mtoto wa shule ya kata hisabati akafaulu huo pia ni mchango na watakaofwata wengine wataendeleza badala ya kuwaza maflovers ya AK!
   
 15. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Haimaanishi hujasema. Kuna kitu huwezi hata kuandika kwa jinsi ulivyokerwa.
  Watu aina hiyo mko wengi na tunaheshimu uwepo wenu ingawa CCM wanajua Ukimya means unawakubali.
  Si unajua kundi wanaloliongoza...
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Haaa, unasema hakuna fly over hata moja? Kwani ile ya manzese hujaiona? Usitushushe hivyo bwana. By the way, wewe tatizo lako ni fly over tu? Wanafunzi kukaa chini hilo hujaona tatizo? Na why fly over? Tunahitaji barabara zaidi maeneo ya vijijini ambako ndiko vinakotoka vyakula, sasa wewe unaiangalia Dar es salaam tu na kusahau kwamba kuna majiji mengine kama Mwanza na kuna maeneo ya vijijini ambako hakupitiki kabisa wakati wa kifuku na hivyo tunahitaji kujenga huko pia? Maybe fly over iwe ni last option, tufikirie juu ya kutumia trein, na pia tufocus zaidi katika kujenga barabara vijijini.
   
 17. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Nimekupata.
  Hatujafikia huko lakini ni nani anayejipanga kuelekea huko?????
  Zaidi kujijengea miji iliyojaa slums.
  Mimi binafsi natambua gharama ya Flyovers na kwa Dar Es Salaam kwa barabara zetu hakuna eneo la kuweka hizo barabara.
  Niliwahi kushauri kuwa kwa nini mabonde kama ya Mto msimbazi yasitumike kuweka barabara upande huu nji hata nane na upande mwingine vilevile badala kujenga fly overs. tuna maeneo bado tunaweza kuyatumia ispokuwa ujima wa viongozi na vision zao mbovu ndo maana wanafikia hapo walipofika.
  South Mwanangu tunahitaji kujifunga mkanda ktk viwanda na Rasilimali.
  Nimetembelea N4,N12,N14 nk ni barabara nzuri ajabu.

  Hebu tuwaangalie hata wakenya Thinka Super High way mbona wameweza.
  Nani aliyetuloga kuwa barabara ni lazima iwe Morogoro Roag.
  Kwa nini usipasue nyingiine mbali na makazi na ukaweka barabara nzuri na watu wataifuata tena watajenga kwa mpango.
  Tuvumilie hadi lini muda unakwenda na watu wamezibuka kuhusu ujenzi????
  CCM hakika wanatuzamisha
   
 18. h

  hans79 JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Wewe acha tu leo nilikuwa nasikiliza bunge eti wanashangilia waziri mkuu kuwaambia posho za madiwani, yaani upuuzi mtupu ni kheri lisingelikuwepo sababu wakubwa wazima wanashangili ujinga.Pana wengi wanamsifu magufuli eti mchapakazi,aibu tupu jiji la dar linanunuka uchafu usiombe mvua inyeshe utakutana na mamvi yametapaka kwenye baadhi ya mitaa.Hivi vichocho vya barabara giza tupu,harafu waziri anajisifu kujenga vichochoro yaani aibu tupu.
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Mkuu mambo yameanza kigoma...Wameweka taa za barabarani zinawashwa pale anapokuja baba Riz tu otherwise zipo tu kama minazi ya kilwa!!....
   
 20. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,094
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  niliwahi kuleta hoja humu jf kurudi tuwe chini ya waingeleza, watu wakabisha sana...oneni majuu tena sio ulaya, kwa majirani zetu tu.
   
Loading...