Inasikitisha Suleimani Kova kutojitambua hata kidogo

Inasikitisha Suleimani Kova kutojitambua hata kidogo

Seif al Islam

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
2,156
Reaction score
640
Akihojiwa juzi kuhusu uwezekano wa viongozi wakuu wa chadema hususani mbowe na slaa kuitwa na kuhiojiwa na polisi kuhusu sakata la Lwakatare, kamanda Kova alinukuliwa akisema, "timu ile ya watu 12 iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa sakata la mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda, ndiyo inahusika katika matukio yote ya ugaidi, ikiwemo kutekwa kwa watu mbalimbali na kutishiwa waandishi wa habari, hivyo watakuja na majibu yao kuhusiana na kile watakachobaini," alisema kamanda Kova.

Hapa Kova anajaribu kwa kujua au kutokujua kuwadanganya Watanzania kuwa matukio ya kukamatwa na kuteswa waandishi na watu wengine kama Dr Ulimboka ni ya kigaidi na kusahau kuwa yule Mkenya wake aliyemkamatwa kwa msaada wa kanisa(japo lilikanusha baadae) ameshtakiwa kwa kosa jingine la kuteka, na kutesa na sio kosa la kigaidi kama anavyokaribu kuueleza umma.kova amka.

Tuna kumbukumbu kubwa na hatusahau kama wewe. Ukitaka kudanganya unapaswa kuwa na kumbukumbu kubwa kuliko yule unayemdanganya.
 
Kova ana LLB?sidhani vyeo kama hivyo vinatakiwa mtu awe na upeo wa sheria
 
..director wa hii filamu anamuangalia tu kwa mbaaaliii
 
Kova hana lolote ila kapewa cheo kwa ajili ya uzoefu.
 
KOVA is a big joke!

Mnamkumbuka Kamanda Gewe?That was really a policeman!
 
Yanakuwa kama haya??
avatar16662_64.gif

Kova akiwa anadanganya utajua tu.
Macho yake huwa yananyooka vizuri tu....yale makengeza yanaisha kabisa.
 
imani ni nzuri sana pale unapoangukia imani ya ukweli lakini inageuka sumu pale inapokuwa ya kupotosha.
hawa na wenzao wengi wanaamini kuwa hapo walipo ndio maisha yenyewe ilmradi wana vijirasilimali na wataendelea kuvilinda kwa nguvu yao na hata wakiondoka basi ccm itaendelea kuwepo na kuendelea kuteua watu watakaowapa 'ulinzi'.
Ni hiyo hiyo imani inayowasahaulisha kusema hata yale wanayotakiwa kuyasema kwa kuyaona hayana umuhimu!
 
wanatujua sisi ni wadanganyika tu..lakini ikoa siku tutakuwa makamanda wa kutokudanganyika.inabidi tuwaombee sana hawa viongozi wetu kwa Mungu ili wajirudi
 
imani ni nzuri sana pale unapoangukia imani ya ukweli lakini inageuka sumu pale inapokuwa ya kupotosha.
Hawa na wenzao wengi wanaamini kuwa hapo walipo ndio maisha yenyewe ilmradi wana vijirasilimali na wataendelea kuvilinda kwa nguvu yao na hata wakiondoka basi ccm itaendelea kuwepo na kuendelea kuteua watu watakaowapa 'ulinzi'.
Ni hiyo hiyo imani inayowasahaulisha kusema hata yale wanayotakiwa kuyasema kwa kuyaona hayana umuhimu!
true!!!
 
Back
Top Bottom