Inasikitisha Suleimani Kova kutojitambua hata kidogo

Inasikitisha Suleimani Kova kutojitambua hata kidogo

Mkuu umenikumbusha mbali sana,hivi huyu kamanda (mstaafu) Alfred Gewe yuko wapi?
Mkuu BHULULU
Kamanda Gewe yuko kijijini kwake Babati vijijini na familia yake.Aligombea ubunge 2010 kupitia CCM(sijui aliingia CCM lini) lakini akapigwa mwereka na mhindi(uchaguzi wa ndani).
 
Waliishaambiwa ukitaka kudanganya usimuhusishe Kova, hajui uongo analazimishwa na CCM

Kanuni kuu ya uongo ni hii...."Ukiwa muongo usiwe mwepesi kusahau"..... tatizo la waongo wengi ndani ya CCM na POPLICCM ni usahaulifu!!
 
Yanakuwa kama haya??
avatar16662_64.gif
umechoka kusmile ukiwa na meno 32 wewe???
 
Hakuna marefu yasiyo na ncha ipo siku wataumbuka na upotoshaji wao kutaka tuamini kuwa cheusi ni cheupe(giningi)
 
Kova anajicho kama la kobla nakumbuka wale wapiga nondo wa mbeya alikuwa anawaona hata kwa kutumia chogo
 
Kova akiwa anadanganya utajua tu.Macho yake huwa yananyooka vizuri tu....yale makengeza yanaisha kabisa.
duh! Kova badili style ya macho wabongo tushakujulia,nimejikuta nacheka,kweli umemuumbua kova.
 
Mkuu BHULULU
Kamanda Gewe yuko kijijini kwake Babati vijijini na familia yake.Aligombea ubunge 2010 kupitia CCM(sijui aliingia CCM lini) lakini akapigwa mwereka na mhindi(uchaguzi wa ndani).

Mkuu nashukuru sana kwa taarifa,huyu jamaa ni kati ya ma-RPC waliokuwa wanajua kazi yao.
 
Akihojiwa juzi kuhusu uwezekano wa viongozi wakuu wa chadema hususani mbowe na slaa kuitwa na kuhiojiwa na polisi kuhusu sakata la Lwakatare, kamanda Kova alinukuliwa akisema, "timu ile ya watu 12 iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa sakata la mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda, ndiyo inahusika katika matukio yote ya ugaidi, ikiwemo kutekwa kwa watu mbalimbali na kutishiwa waandishi wa habari, hivyo watakuja na majibu yao kuhusiana na kile watakachobaini,” alisema kamanda Kova.

Hapa Kova anajaribu kwa kujua au kutokujua kuwadanganya Watanzania kuwa matukio ya kukamatwa na kuteswa waandishi na watu wengine kama Dr Ulimboka ni ya kigaidi na kusahau kuwa yule Mkenya wake aliyemkamatwa kwa msaada wa kanisa(japo lilikanusha baadae) ameshtakiwa kwa kosa jingine la kuteka, na kutesa na sio kosa la kigaidi kama anavyokaribu kuueleza umma.kova amka.

Tuna kumbukumbu kubwa na hatusahau kama wewe. Ukitaka kudanganya unapaswa kuwa na kumbukumbu kubwa kuliko yule unayemdanganya.
na mtahaha sana. huo ni wanzo tu.
 
Kanuni kuu ya uongo ni hii...."Ukiwa muongo usiwe mwepesi kusahau"..... tatizo la waongo wengi ndani ya CCM na POPLICCM ni usahaulifu!!
Mkuu: wasipokuwa wasahaulifu watadanya bila kugundulika....
 
Waliishaambiwa ukitaka kudanganya usimuhusishe Kova, hajui uongo analazimishwa na CCM
Kova akitaka kudanganya nafsi yake inamsaliti maana muonekano wake unaonesha kabisa wakati gani anaongea uongo na wakati gani anaongea ukweli...
 
Mtu muongo lazima awe na kumbukumbu kubwa vinginevyo utakuwa kama Kova.
 
Katika nchi yetu uzalendo ulishazikwa siku nyingi. Siku hizi lugha ni "mimi" na "familia yangu" na taifa baadaye au hamna! Hayo anayosema Kamanda Kova hata kama hayaamini atayasema na kurudirudia. Kwa sababu hata akisema uwongo mchana kweupe, maadamu analinda maslahi ya wachache na wenye dola na pesa hamna athari kwake( no consequence). Sana sana anapongezwa tu. Sasa katika hali kama hiyo yeye atafanya nini? Akiwa upande wa haki, haraka sana anapachikwa jina kuwa si mwenzetu na kibarua chake kinakuwa hatarini. Tatizo ni mfumo uliomweka pale,haujampa nafasi ya kutenda haki maana nyuma anahisi kuna jamaa wanamsubiri atoe hiyo haki halafu yeye agongwe kichwani na kitu chenye ncha kali. Mfumo ndio tatizo,swali ni je ni namna gani tunabadilisha mfumo ili mtu kama Kova au IGP awe huru kutoa maamuzi? Mfano haupo marekani wa uropa,upo hapa karibu baada ya kuvuka mpaka wa Namanga. Kenya!
 
Back
Top Bottom