thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Nani alaumiwe?Nilijikuta nikiwaza na kuwazua kwa jinsi Serikali inavyojitapa kuwa nchi hii tuna pesa nyingi na tunaweza kufanya lolote ila tumekosa kitu muhimu kiasi hiki kwa ajili ya wananchi katika hali za dharura mahospitalini.
Jana Rais alisikika alipomtembelea hospitali Askofu Mkuu wa Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu;"Niliongea na Askofu Msaidizi wakati huo wameelezwa na KCMC kwamba ni lazima Askofu Ruwa'ichi apelekwe Muhimbili.
palikuwa hakuna usafiri wa kumleta lazima wachukue ndege ya ambulance ya kumleta na ndege lazima ukodi Afrika Kusini au Kenya, basi wakati wanahangaika nikasema Madaktari wajiandae natuma ndege, ndipo nikatuma ndege harakaharaka ikaenda ikamchukua" - Rais Magufuli.Inahuzunisha.