Inasikitisha sana: Hivi ni kweli nchi hii tunaweza kukosa ndege au helicopter za ambulance za dharura mpaka tuazime nchi nyingine?

Nilijikuta nikiwaza na kuwazua kwa jinsi Serikali inavyojitapa kuwa nchi hii tuna pesa nyingi na tunaweza kufanya lolote ila tumekosa kitu muhimu kiasi hiki kwa ajili ya wananchi katika hali za dharura mahospitalini.

Jana Rais alisikika alipomtembelea hospitali Askofu Mkuu wa Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu;"Niliongea na Askofu Msaidizi wakati huo wameelezwa na KCMC kwamba ni lazima Askofu Ruwa'ichi apelekwe Muhimbili.

palikuwa hakuna usafiri wa kumleta lazima wachukue ndege ya ambulance ya kumleta na ndege lazima ukodi Afrika Kusini au Kenya, basi wakati wanahangaika nikasema Madaktari wajiandae natuma ndege, ndipo nikatuma ndege harakaharaka ikaenda ikamchukua" - Rais Magufuli.Inahuzunisha.
Tunataka Kujua Source ya Ugonjwa wa Baba Askofu
 
Kwani Tundu Lisu ni mbunge wa kwanza kupata matatizo akiwa bungeni?!

Ubinadamu pia una taratibu zake!

Ililetwa ndege apelekwe Muhimbili kwa mujibu wa utaratibu wa bunge lakini Mbowe akatumia ubinadamu wake kukodi ndege kwenda Nairobi, sioni tatizo hapo!

..Ni mbunge wa kwanza kushambuliwa kwa risasi ktk eneo lenye ulinzi wa serikali 24/7.

..ilipoamuliwa atapelekwa Nairobi kwanini Jiwe au Ndugai hawakumsaidia?

..mbona Madaktari walikuwa na ubinadamu wa kumsindikiza mpaka Nairobi?

..viongozi wakiwa na roho ngumu na ya ukatili wanaambukiza na walio chini yao. Na hili limejidhihirisha ktk suala la TL.
 
Iliamliwa na nani apelekwe Nairobi?!

Aliamua kwa kufuata utaratibu gani?

Tusisahau kuwa Lisu ni mbunge tu kama ilivyokuwa kwa Nassari......! Ingekuwa madaktari wetu wamekiri kushindwa kumhudumia hapo ungekuwa na hoja ya msingi!
 
..aliyeamua ni Katibu Mkuu wa wizara ya afya.

..lakini hili ni suala la UBINADAMU zaidi.

..katika hali aliyokuwa nayo TL na kuzingatia upekee wa shambulizi lile, kweli inaswihi Jiwe na Ndugai kuchukua misimamo waliyochukua masaa machache baada ya tukio?

..najiuliza kama TL angekufa, Jiwe na Ndugai wangepita mbele ya jeneza lake wakisema nini ktk mioyo na nafsi zao?
 
Aliyekuwa katibu mkuu wizara ya Afya ambaye ni mtaalamu wa dawa ya usingizi aliamua Lisu apelekwe Nairobi?!!... Kwa capacity ipi ya kitaaluma au kiutawala?!!

Hii siamini kabisa....... Ni Mbowe aliyeshinikiza tuwe wakweli tu!
 
jambo la kushangaz sanaa mkuu,mount kilimanjaro unaingiza mapato mengi sana kwa mwaka,ila cha kushangaza wagen wanopata emergenc juu mliman huko,wanaitisha helikopta ya kuresque kutoka Nairobi,yaan unashanga Kinapa ipo pale kwa kazi gani?
 
Aliyekuwa katibu mkuu wizara ya Afya ambaye ni mtaalamu wa dawa ya usingizi aliamua Lisu apelekwe Nairobi?!!... Kwa capacity ipi ya kitaaluma au kiutawala?!!

Hii siamini kabisa....... Ni Mbowe aliyeshinikiza tuwe wakweli tu!

..kuna mahojiana TL alifanya akiwa Nairobi.

..ktk mahojiano hayo "alitegua" kitendawili cha nani alimaliza mabishano ya mgonjwa apelekwe Muhimbili au Nairobi.

..hivi unafikiri Madaktari wa serikali wangesafiri na TL kwenda Nairobi bila ruhusa na baraka za Katibu Mkuu wa wizara?

..Unafahamu kuwa kiutaratibu Katibu Mkuu wizara ya afya ndiye anayepokea maombi ya wagonjwa kutibiwa nje, na ndiyo mtendaji mwenye jukumu la kuyakubali au kuyakataa?
 
Kumbe swala la kumpeleka Tundu Lisu Nairobi ilikuwa ni uamuzi wa serikali siyo familia ya Tundu Lisu?
 
Sio kila kitu lazima afanye Magufuli ooops rais. Wizara ya Afya wanafanya nini? Hili ni katika majukumu yake, Air Ambulance nk. Amkeni Watanzania tujenge nchi yetu.
 
Mwanzo nilidhan Mimi ndo huwa sina akili.. Kumbe tuko wengi... Maada imekuja bila siasa ndani yake but comment zina Pande mbili tayar..
 
Kumbe swala la kumpeleka Tundu Lisu Nairobi ilikuwa ni uamuzi wa serikali siyo familia ya Tundu Lisu?

..according to TL kulikuwa na mabishano ya Muhimbili vs Nairobi.

..sasa anadai aliambiwa Dr.Mpoki alitoa kauli, " ...I am a medical doctor, he goes to Nairobi..."

..na mimi naamini maelezo hayo ni ya kweli kwasababu ya uwepo wa Madaktari wa serikali ktk msafara wa kumpeleka TL Nairobi.

..sasa katika mazingira hayo, najiuliza kwanini Jiwe na Ndugai walisusia? Kwanini hawakutoa ndege ya serikali imuwahishe mgonjwa Nairobi?

..Jiwe na Ndugai wangeonyesha utu na upendo kwa TL wananchi wa kawaida kama wewe msingelazimika kutetea na kuhalalisha ukatili aliotendewa TL.
 
Siyo kweli... hizo ndege za wagonjwa hata hapa zipo, kwenye baadhi ya hospital za private...

Sijui kwa nini hawapendi kuzitumia...

Cc: mahondaw
 
Naomba tutajie aina ya hiyo Helicopter ya $500,000.
Zipo nyingi used kwa bei hiyo, cheki links zifuatazo tena hizi ni chache sana, ila kuanzia $500,000 na kuendelea unapata.
 
..according to TL kulikuwa na mabishano ya Muhimbili vs Nairobi.

..sasa anadai aliambiwa Dr.Mpoki alitoa kauli, " ...I am a medical doctor, he goes to Nairobi..."

..na mimi naamini maelezo hayo ni ya kweli kwasababu ya uwepo wa Madaktari wa serikali ktk msafara wa kumpeleka TL Nairobi.

..sasa katika mazingira hayo, najiuliza kwanini Jiwe na Ndugai walisusia? Kwanini hawakutoa ndege ya serikali imuwahishe mgonjwa Nairobi?

..Jiwe na Ndugai wangeonyesha utu na upendo kwa TL wananchi wa kawaida kama wewe msingelazimika kutetea na kuhalalisha ukatili aliotendewa TL.
Mabishano yalikuwa kati ya Dr Mpoki na nani?!
 
Sio helicopter za ambulance tu, hata helicopter za zimamoto hatuna. Kuna kipindi moto uliwaka pale mpakani na Rwanda kwa upande wa Tz. Ilibidi wanyarwanda ndio watume helicopter ya zimamoto.
 
Nilijikuta nikiwaza na kuwazua kwa jinsi Serikali inavyojitapa kuwa nchi hii tuna pesa nyingi na tunaweza kufanya lolote ila tumekosa kitu muhimu kiasi hiki kwa ajili ya wananchi katika hali za dharura mahospitalini.

Jana Rais alisikika alipomtembelea hospitali Askofu Mkuu wa Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu;"Niliongea na Askofu Msaidizi wakati huo wameelezwa na KCMC kwamba ni lazima Askofu Ruwa'ichi apelekwe Muhimbili.

palikuwa hakuna usafiri wa kumleta lazima wachukue ndege ya ambulance ya kumleta na ndege lazima ukodi Afrika Kusini au Kenya, basi wakati wanahangaika nikasema Madaktari wajiandae natuma ndege, ndipo nikatuma ndege harakaharaka ikaenda ikamchukua" - Rais Magufuli.Inahuzunisha.
Hela zipo, sema priority!
 
Back
Top Bottom