Inasikitisha sana: Hivi ni kweli nchi hii tunaweza kukosa ndege au helicopter za ambulance za dharura mpaka tuazime nchi nyingine?

Umeeleza vizuri madaktari ndio hupendekeza mgonjwa apelekwe hospitali gani kama ilivyokuwa kwa Lisu na Askofu.

Safari ya Nairobi ilikuwa ni mipango binafsi ya Chadema na siyo ushauri wa madaktari!

..Ilikuwa ni mapendekezo na maombi ya familia kuwa TL apelekwe Nairobi kwa matibabu zaidi.

..Na Madaktari, wakiongozwa na PS wa wizara ya afya, waliridhia mapendekezo / maombi hayo. Ndiyo maana walikubali kumsindikiza mgonjwa.

..Swali ni kwanini serikali ilikosa huruma ya kumpatia usafiri mgonjwa, kiongozi wa bunge, ambaye alikuwa mahututi ktk hatari ya kukata roho?
 
Naamini kabla ya Disemba, 2019 tutanunua tatu. Yaani hela zinazookolewa kwenye dhahabu/ madini na nyara nyingine za serikali zikipigwa mnada kwa miezi hii 3 October had Disemba, 2019 tunanunua! Juzi nimesoma gazeti Tarime tu pale 2bn zimekusanywa kwa Wachina. Mhe. Rais, Dreamliner zinakuja zije sambamba moja ya aina hii! Rais alishasema toa maoni yako , yeye atafanyia kazi. Tanzania oyeeeee!
 
Mabilioni yaliyotumika kujengea uwanja wa Ndege wa Chato ambao hauna umuhimu wowote kwa sasa yangetumika kununua hata helicopter tatu kwa ajili ya kutumika kama air ambulance. Unaweza kupata helicopter nzuri kuanzia $500,000.
 
Nilijikuta nikiwaza na kuwazua kwa jinsi Serikali inavyojitapa kuwa nchi hii tuna pesa nyingi na tunaweza kufanya lolote ila tumekosa kitu muhimu kiasi hiki kwa ajili ya wananchi katika hali za dharura mahospitalini.

Jana Rais alisikika alipomtembelea hospitali Askofu Mkuu wa Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu;"Niliongea na Askofu Msaidizi wakati huo wameelezwa na KCMC kwamba ni lazima Askofu Ruwa'ichi apelekwe Muhimbili.

palikuwa hakuna usafiri wa kumleta lazima wachukue ndege ya ambulance ya kumleta na ndege lazima ukodi Afrika Kusini au Kenya, basi wakati wanahangaika nikasema Madaktari wajiandae natuma ndege, ndipo nikatuma ndege harakaharaka ikaenda ikamchukua" - Rais Magufuli.Inahuzunisha.
Mmmm watanzania...acha kila mtu mjuaji.
Hiyo helicopter ya ambulance Serikali inunue ya nini? Mashirika ya bima yatafanya KAZI gani?
 
Mabilioni yaliyotumika kujengea uwanja wa Ndege wa Chato ambao hauna umuhimu wowote kwa sasa yangetumika kununua hata helicopter tatu kwa ajili ya kutumika kama air ambulance. Unaweza kupata helicopter nzuri kuanzia $500,000.
Naomba tutajie aina ya hiyo Helicopter ya $500,000.
 
..Ilikuwa ni mapendekezo na maombi ya familia kuwa TL apelekwe Nairobi kwa matibabu zaidi.

..Na Madaktari, wakiongozwa na PS wa wizara ya afya, waliridhia mapendekezo / maombi hayo. Ndiyo maana walikubali kumsindikiza mgonjwa.

..Swali ni kwanini serikali ilikosa huruma ya kumpatia usafiri mgonjwa, kiongozi wa bunge, ambaye alikuwa mahututi ktk hatari ya kukata roho?
Familia ya Lisu inapsjua Nairobi hadi walazimishe mgonjwa apelekwe huko?!!...ile ilikuwa ni mipango ya Chadema!
 
Kwa kifupi tu ni kwamba, kama baba Askofu angekua ni Mtanzania wa kawaida tuu wa kutoka Nalinjinji, au Kantalamba, au Kamsamba, hadi sasa hivi uwezekano kwamba angekua amefariki ni 90%. Hivyo ndivyo ambavyo Watanzania wengi wa kawaida wanafariki kwa kukosa proper medical attention wanapohitaji.
na angekua mtanzania wa kawaida wa kutoka mchambawima possibility ya kufa ingeongezeka na kufikia 99.9%. double standards at its f**ng best.
 
Una hoja nzito.kanisa la Efatha kwa Mwingira wana Hadi ndege ya kanisa.Katoliki sijui kwa Nini hawana.lawama zingine kwa serikali Kama za mleta mada hazina msingi.Wao Kama kanisa lenye mahospitali walitakiwa wawe nazo hizo ndege za ambulance

Na Wananchi wenye Hali duni , wao wajifie tu si ndivyo
Mkuu !?
 
Ni kweli inafikirisha.

Ila hata kama una familia na mmezoea kula maharage, utashangaa siku ukinunua kitoweo cha nyama, ama utakuta visu ni butu au havipo kabisa. Unaweza mtupia lawama mwanafamilia fulani kwa kuwa na kisu butu au kukosa kisu kabisa lakini ukasahau kwamba umepiga hatua ya kununua nyama. Tusisahau kwamba uwepo wa Neurosurgeons hapo MOI ambao wamemfanyia operation Mhe. Askofu, ndio umetufanya tuone kwanini hatuna air ambulance.

Hizi ndege au helikopta ambazo ni ambulance huwa zinamilikiwa na makampuni binafsi katika hizo nchi walikosema zipo. Mara zote hukodishwa au hutoa huduma kwa wanachama wa makampuni ya Bima za Afya fulani. Lakini pia wengine ukiacha bima za afya huwa wana emergency medical evacuation insurance, ambayo huitumia hasa anaposafiri kwenda sehemu fulani kusikokuwa na matibabu bora ili akipata shida aweze hamishiwa maeneo yenye huduma bora.

Hii biashara ya kusafirisha wagonjwa kwa ndege inahitaji mitaji mikubwa. Na hata mtu akiamua ku invest huko basi lazima awe na uhakika wa kupata faida. Sasa unaweza jiuliza ni nani anaweza wekeza eneo hilo, na atapata return gani? Hata hayo makampuni ya Afrika Kusini yakija TZ yatapata wateja? Je, mashirika ya Bima za Afya nayo yako tayari kuingia gharama za evacuations?

Je, serikali ianze kuwekeza kununua ndege za kusafirisha wagonjwa badala ya kujenga vituo vya afya, hospitali na kupeleka watumishi pamoja na vitendea kazi? Kuna matukio mangapi ya wagonjwa miongoni mwa watanzania wanaokaribia milioni 60 wanaohitaji hizo evacuations yanayoifanya serikali kama serikali ifikirie kununua ndege au helikopta za evacuations?

Nadhani ni muda muafaka kwa watu binafsi kuanza kuwekeza katika air evacuations (ambazo zimeshaanza kufanywa na makampuni kadhaa) na pia sasa makampuni ya Bima za Afya yafikirie kuwa na vitita vya evacuations kwa wagonjwa wote (na sio kwa baadhi ya wagonjwa kama BOT na NMB). Ila pia hima watanzania wote tujiunge na mifuko ya Bima ya Afya ili kupunguza gharama za matibabu.
 
Familia ya Lisu inapsjua Nairobi hadi walazimishe mgonjwa apelekwe huko?!!...ile ilikuwa ni mipango ya Chadema!

..hata kama ilikuwa ni mipango ya cdm bado inashangaza kuwa ndani ya serikali hakuna aliyeingiwa simanzi au kuona umuhimu wa kusaidiana nao kwa kuwapatia usafiri wa kumuwahisha TL Nairobi.

..angekufa ungekuta Jiwe na Ndugai wanatoa kauli nzuri-nzuri za kumpamba na kujionyesha kuwa alikuwa mpendwa wao. Lakini they were not ready to do what was in their power to save his life.

..unajua viongozi wasipothaminiana, au wakichukiana, siyo rahisi wananchi wa kawaida wakapendana na kuwa na mshikamano.
 
Kwani Nairobi kuna nini cha ajabu ambacho Muhimbili hakuna?

Mbona walishindwa kumhudumia mgonjwa hadi mwisho na wakalazimika kumpeleka Ubelgiji?
 
Kwani Nairobi kuna nini cha ajabu ambacho Muhimbili hakuna?

Mbona walishindwa kumhudumia mgonjwa hadi mwisho na wakalazimika kumpeleka Ubelgiji?
😁😁😁😁 Lisu alitoroka hospitali Nairobi akiwa na madrip akakimbilia ubelgiji kama Kuna matibabu mazuri kilimkimbiza Nini? Mleta mada leta jibu
 
Kwani Nairobi kuna nini cha ajabu ambacho Muhimbili hakuna?

Mbona walishindwa kumhudumia mgonjwa hadi mwisho na wakalazimika kumpeleka Ubelgiji?

..hii siyo hoja ya Nairobi vs Muhimbili.

..hoja yangu ni UBINADAMU na UTU ambao nadhani ulikosekana kwa watendaji wa Bunge na serikali ktk kumsaidia TL.

..Jiwe, Ndugai, na Mbowe, walitakiwa washikamane, wawe kitu kimoja, siku ile Sept 7 ktk kuokoa maisha ya kiongozi mwenzao.

..UPENDO na UMOJA wetu umekwenda wapi?
 
Mtanza

Mtanzania ambae bado anawaamini ccm akapimwe akili
Tupo na kwa taarifa yako..

P
 
..hii siyo hoja ya Nairobi vs Muhimbili.

..hoja yangu ni UBINADAMU na UTU ambao nadhani ulikosekana kwa watendaji wa Bunge na serikali ktk kumsaidia TL.

..Jiwe, Ndugai, na Mbowe, walitakiwa washikamane, wawe kitu kimoja, siku ile Sept 7 ktk kuokoa maisha ya kiongozi mwenzao.

..UPENDO na UMOJA wetu umekwenda wapi?
Kwani Tundu Lisu ni mbunge wa kwanza kupata matatizo akiwa bungeni?!

Ubinadamu pia una taratibu zake!

Ililetwa ndege apelekwe Muhimbili kwa mujibu wa utaratibu wa bunge lakini Mbowe akatumia ubinadamu wake kukodi ndege kwenda Nairobi, sioni tatizo hapo!
 
Back
Top Bottom