Inasikitisha sana: Hivi ni kweli nchi hii tunaweza kukosa ndege au helicopter za ambulance za dharura mpaka tuazime nchi nyingine?

Nilijikuta nikiwaza na kuwazua kwa jinsi Serikali inavyojitapa kuwa nchi hii tuna pesa nyingi na tunaweza kufanya lolote ila tumekosa kitu muhimu kiasi hiki kwa ajili ya wananchi katika hali za dharura mahospitalini.

Jana Rais alisikika alipomtembelea hospitali Askofu Mkuu wa Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu;"Niliongea na Askofu Msaidizi wakati huo wameelezwa na KCMC kwamba ni lazima Askofu Ruwa'ichi apelekwe Muhimbili.

palikuwa hakuna usafiri wa kumleta lazima wachukue ndege ya ambulance ya kumleta na ndege lazima ukodi Afrika Kusini au Kenya, basi wakati wanahangaika nikasema Madaktari wajiandae natuma ndege, ndipo nikatuma ndege harakaharaka ikaenda ikamchukua" - Rais Magufuli.Inahuzunisha.
Nani alaumiwe?
 
Kwani huko Afrika ya Kusini na Kenya ni serikali ndiyo zina ndege za kukodisha? No, ni makampuni ya watu binafsi. Tuko bado mno kwenye mtazamo wa kuitegemea serikali.

Hawapo tena watu aina ya Ndesamburo wenye mtaji na uthubutu wa kufanya biashara ya kukodisha ndege? Tumezidi mno kujikita kwenye vibiashara koko vya baa na mabasi!

Serikali si baba wala mama. Kazi yake ni kuweka mazingira wezeshi tu.
 
Mr PhD siasa iko wapi hapo?!!!
Suala la JPM kua na huruma linaingilia wapi hapo......wakati yeye ndo kashikilia hazina yote na Atm ya BOT anaamua lolote hata bila kufuata protocol ....... . ...nyie ndo mnasifia upumbavu ananunua ndege kwa hela ya umma ile ile nakuacha kununua dawa ma hospitalini watu wanakufa kwa magonjwa ya kawaida.....
 
Utabeba watu wangapi kati ya watu 50m?
Jibu ni kujenga na kuboresha hospitali za wilaya kwa speed ya radio.
 
Una uhakika kwamba zikinunuliwa hutasema kwamba wagonjwa wangapi wanapanda ndege bora zinunuliwe ambulance za magari?
Hilo litakuwa swala lingine mkuu. Ikiwepo moja tutashangilia na kudai ya pili, hii ndio nature ya sisi binadamu.
 
Watanzania vigeu geu at work

Zikinunuliwa mtahoji tutakula helicopters
 
Nilijikuta nikiwaza na kuwazua kwa jinsi Serikali inavyojitapa kuwa nchi hii tuna pesa nyingi na tunaweza kufanya lolote ila tumekosa kitu muhimu kiasi hiki kwa ajili ya wananchi katika hali za dharura mahospitalini.

Jana Rais alisikika alipomtembelea hospitali Askofu Mkuu wa Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu;"Niliongea na Askofu Msaidizi wakati huo wameelezwa na KCMC kwamba ni lazima Askofu Ruwa'ichi apelekwe Muhimbili.

palikuwa hakuna usafiri wa kumleta lazima wachukue ndege ya ambulance ya kumleta na ndege lazima ukodi Afrika Kusini au Kenya, basi wakati wanahangaika nikasema Madaktari wajiandae natuma ndege, ndipo nikatuma ndege harakaharaka ikaenda ikamchukua" - Rais Magufuli.Inahuzunisha.

Ungeanza kwa kupongeza. Negativity is very unhealthy my dear professor majungu. Vituo vya afya na zahanati zote na Hospital za Wilaya huzioni unakimbilia Helikopters. Watapanda wangapi kati ya 55 Millionen Leuten.
 
Utabeba watu wangapi kati ya watu 50m?
Jibu ni kujenga na kuboresha hospitali za wilaya kwa speed ya radio.
Kwani watu 50m wanaugua kwa mkupuo mkuu?.....ni aibu aibu nchi kama Tz kukosa ambulance ya ndege wakati tunaweza kutaifisha dhabu za watu zaidi ya 300kg....
 
Na vikinunuliwa ndio wakwanza kuropoka hovyo Ndege za nini hakuna maji
Upuuzi mtupu
Huwezi kamilisha kila jambo never
 
Tunaposimama na kutamba kuwa tumenunua Bombardier 3, Airbus 2 na Dreamliner 2 tena cash huku nchi haina Air ambulance sio tatu, hata moja hakuna.
Maana hospital kuu zote Muhimbili, Bugando na KCMC kulipaswa kuwa na vyombo hivyo hata kwa kuanzia ni aibu na nchi ya Wagagagigikoko wasio jua vipaumbele
 
Hii nchi asilimia 80 tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu
Washauri wa mzee baba wachukue hili Kama changamoto kwamba for now inabidi tuboreshe huduma za afya especially emergency cases ( ingawa najua wanasiasa wanajua sema tu ndo hivyo Tena😪)
 
Suala la JPM kua na huruma linaingilia wapi hapo......wakati yeye ndo kashikilia hazina yote na Atm ya BOT anaamua lolote hata bila kufuata protocol ....... . ...nyie ndo mnasifia upumbavu ananunua ndege kwa hela ya umma ile ile nakuacha kununua dawa ma hospitalini watu wanakufa kwa magonjwa ya kawaida.....
Unateseka sana!
 
Kwani huko Afrika ya Kusini na Kenya ni serikali ndiyo zina ndege za kukodisha? No, ni makampuni ya watu binafsi. Tuko bado mno kwenye mtazamo wa kuitegemea serikali.

Hawapo tena watu aina ya Ndesamburo wenye mtaji na uthubutu wa kufanya biashara ya kukodisha ndege? Tumezidi mno kujikita kwenye vibiashara koko vya baa na mabasi!

Serikali si baba wala mama. Kazi yake ni kuweka mazingira wezeshi tu.
Watakao kuelewa si wengi hapa. Mtu amezaliwa na amekua kila siku anaona Ambulances zinazomilikiwa na hospitali ya Mwananyamala, hivyo anakariri maisha kila kitu government.
 
Ndege ilitumwa ya kumpeleka Muhimbili!

..waliokuwa wakimhudumia Askofu walitaka apelekwe Muhimbili, na serikali ikatoa ndege.

..familia ya TL walitaka TL apelekwe Nairobi, hawakuwa na fedha za kumsafirisha, na mgonjwa alikuwa ktk hatari kubwa ya kupoteza maisha. kwanini serikali haikumfikiria na kutoa ndege haraka asafirishwe?
 
Umeeleza vizuri madaktari ndio hupendekeza mgonjwa apelekwe hospitali gani kama ilivyokuwa kwa Lisu na Askofu.

Safari ya Nairobi ilikuwa ni mipango binafsi ya Chadema na siyo ushauri wa madaktari!
 
Back
Top Bottom