Fascinating
Member
- May 14, 2025
- 93
- 224
Kuna mfululizo wa dokumentari nilikuwa naufuatilia unaoonyesha safari ya timu ya Recharging Hope. Hawa ni vijana wabunifu, wanaosafiri kwa pikipiki zinazotumia umeme wa jua (Solar-powered electric motorcycles) kutoka Nairobi kuelekea Cape Town. Lengo lao ni kuonyesha kuwa teknolojia za kijani (Green Tech) zinawezekana Afrika kwa kutimiza azma ya kuendesha pikipiki kwa zaidi ya kilomita 6,000 kupitia nchi sita-Kenya, Tanzania, Malawi, Zambia, Botswana, na Afrika Kusini.
Lakini kama kawaida yetu hapa nyumbani, huwa hatukosagi namna ya kujichafua. Yaani tumejishikiria, wamepita kote huko salama, lakini kimbembe kimeenda kuwakuta mwishoni kabisa mwa ardhi yetu. Hali hii inatia kichefuchefu na inacha maswali mazito juu ya uelekeo wetu kama taifa linalojinasibu kutaka maendeleo:
Urasimu wa Kipumbavu kupata huduma za Mipakani
Katika Episode ya 3, timu ya Recharging Hope imeweka wazi madhila yaliyowakuta mpaka wa Tanzania na Malawi. Wanasema walisota kwa zaidi ya saa nne kutokana na urasimu usio na kichwa wala miguu. Kibaya zaidi, wanakiri kuwa kuna watu walijaribu kuwatapeli (scam) mchana kweupe, jambo lililozua malumbano makali. Hii ni aibu ya kitaifa jamani! Badala ya kuwapokea kwa stara watu wanaotengeneza makala kwa tabasamu na kuwapa kila msaada ili kuitangaza nchi kwenye hizo Makala zao, sisi tunawatazama kama "fursa" ya kupooza njaa zetu na tamaa za muda mfupi.
Tunafukuza "Startups" na Kujichimbia Kaburi la Uwekezaji
Dunia haitusubiri. Startups na makampuni ya teknolojia yanatafuta mazingira ambako akili na muda wao vinaheshimiwa. Ikiwa watu wanapata "stress" ya kijinga na kukumbana na ukasuku wa kishamba wa maafisa wetu, nani mwingine atathubutu kuja akiiona hii Makala? Kwa tabia hizi, tusishangae kuona wawekezaji wakikimbilia nchi jirani ambako mifumo yao imetulia na haina "njaa" ya namna hii.
Tunaharibu Taswira ya Nchi Kimataifa (Reputational Damage)
Video hii inatazamwa na dunia nzima. Jamaa wameipa Title ya "Stopped by ICE in Tanzania???" ni pigo kwa utalii na diplomasia yetu. Inatengeneza taswira ya nchi "iliyooza" (rotted) kuanzia kwenye mifumo ya utoaji huduma. Hata kama tuna mibuyu mizuri na ukarimu wa watu wa vijijini kama jamaa alivyosema, uchafu huu wa maafisa wetu wa mipakani wanafuta mema yote yaliyotangazwa kupitia kwenye hiyo "Royal Tour".
Jamani tuache ushabiki usio na tija. Nchi yetu inahitaji mabadiliko ya kifikra kuanzia ngazi za chini hadi juu. Vinginevyo, tutabaki tunapiga makofi kwa mafanikio ya wenzetu huku sisi tukiishia kuwakamua na kuwakatisha tamaa wageni wachache wanaokuja na mwanga wa matumaini.
Tazama aibu hii hapa:
Stopped by ICE in Tanzania???
Wakuu, nawasilisha kwa uchungu mno!