INASIKITISH SANA! (kayumba vs st.Naniu)

INASIKITISH SANA! (kayumba vs st.Naniu)

Joined
May 14, 2016
Posts
54
Reaction score
19
●Kondakta kumsimamisha mwanafunzi kutoka kwenye siti ili aketi mtu mzima ni heshima.
●Je, maskini kusimamishwa aketi tajiri tutaitaje??

■Ngoja niwape mkasa wa hivi karibuni jinsi maskini anavyo dharaulika.

Hivi karibuni chuo kikuu UDSM kiliandaa mashindano kupitia D-lab. Mashindano hayo yalikua ya Tehama kwa watoto wakike yaliitwa "SMART GIRL" na yalihusisha baadhi ya shule za sekondari wilaya ya kinondoni (5) Kawe ukwamani, feza girls, salma kikwete, Alfa na Mikocheni.
Katika mashindano hayo wanafunzi hao wakike kutoka shule hizo walikusanyikia katika college ya ICT pale kijitonyama kwaajili ya kutumia computer labs kufanyia projects zao. Wanafunzi hao walikua wakichukuliwa na daladala zilizokodiwa na D-lab kutoka mashuleni kwao hadi kijitonyama.

MKASA:
wanafunzi wa shule ya serikali ya "kawe ukwamani" na wanafunzi wa shule ya binafsi "feza girls" ambazo zipo jirani walikuwa wakipanda gari kwa mjumuiko. Lakini cha kushangaza na cha kutia aibu na fedheha, dereva aliwaamuru wanafunzi wa shule ya ukwamani wawe wanasimama na kuwapisha wale wa feza wakae kwenye siti. Jambo hili liliwakera sana wanafunzi hao wa ukwamani na kuwafanya wajiskie vibaya nakujiona hawana thamani. Pamoja na kwamba magari hayo ni ya kukodi na yalikodiwa na d-lab na sio feza, lakini wanafunzi wa ukwamani waliamuriwa kusimama. Wakati wa kurudi wanafunzi wa ukwamani walitangulia kupanda na walikalia siti. Dereva aliwaamuru wote washuke ili wanafunzi wa feza wapande kwanza na kukaa kisha wao wataingia kusimama. Baadhi ya wanafunzi walijawa na jazba na walikua wakiulizana wenyewe kwa wenyewe "kwanini hivi? Kwani sisi sio watu? Kwani hili gari ni kwaajili ya akina nani?" Na maswali mengine waliokosa majibu yake. Lakini walipojaribu kumuuliza dereva aliwajibu kwa kejeli na kuwaambia anafuata maelekezo huku akikazia "halafu mnakera nyinyi? Kwanini hamfuati maelekezo?"

Ndugu wadau, hii imekaa vipi? Nimeandika haya kwa hisia kali sana 😤. Nikijaribu kuvaa viatu vya hawa wanafunzi havinitoshi! Nimejiskia vibaya sana. Ni jamii gani tunaitengeneza kwa kuwajengea watoto misingi ya madaraja ya kibaguzi namna hii?
Nawasilisha kwenu kupata mawazo yenu. Ahsanteni.
 
Serikali Iboreshe shule zake... Hizi feza na the likes hakuna kitu zinafanya zaidi ya kudidimiza hata kile kidogo tungeweza kusalvage kwa maslahi ya taifa na utamaduni wetu..

Piga marufuku mamitaala ya kingereza.. turudie kiswahili. Na Kiingereza kifundishwe tu kama lugha. Hata hivyo waliosoma chini ya utaratibu huu ndio wanaoongea na kuandika kiingereza na kiswahili sanifu.. hawa wa kisasa utopolo mtupu.

Na pia tuwaseme wanaouza heshima kama hao waliotoa maelekezo kwa dereva katika bandiko. Wazazi wengi tumeingia kwenye mtego wa mabeberu.
Tunajinyima kufika hatua ya kukufuru ili tu watoto waende kwenye shule zitakazo wafanya waheshimiwe...

Na sio waende kuelimika ili waheshimiwe kwa.mchango na maarifa waliyoyapata. Poleni kwa kusema mbali kabisa na bandiko..nimewiwa kusema hili kwa maana hata katika kazi kuna hii stigma.. haupimwi kwa uwezo ila kwa ufahari wa taasisi.

Ni aibu.. systematically tumeelimishwa vyetu ni vya hovyo.. na sasa tumehitimu maana tunafadhili muendelezo wa kudidimiza vya kwetu.. kwa fedha zetu wenyewe za ngama... 🙁

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Acha tu mkuu
 
Back
Top Bottom