Mara ya mwisho kwa PRC kupigana vita ilikuwa mwaka 1979, na ulikuwa ni mgogoro mdogo sana kule Vietnam. China imekuwa ikijificha nyuma ya kivuli cha soft power na propaganda, lakini inapokuja kwenye operesheni za kisasa za kijeshi, kwa bahati mbaya ni "Paper Tiger" (mbwa asiye na meno). Licha ya kujimwambafai na gwaride za kijeshi, vitisho kutoka Beijing, na maonesho ya silaha na ndege za kivita, lakini hawa Wachina hatujawaona kwenye operesheni yoyote ya maana ya kivita kwa miaka ya hivi karibuni.
China haina uzoefu wa mapambano ya kisasa kama mataifa mengine kama vile Marekani, NATO (Ulaya), Iran, Israel, na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati.
Hata baadhi ya nchi za Afrika kama vile DRC, Rwanda, Misri, Afrika Kusini, Nigeria, na Ethiopia kwa miaka ya hivi karibuni zina uzoefu mkubwa wa mapambano (military combat experience) kuliko China.
Licha ya kujisifia kuwa na mfumo Bora na tata a wa ulinzi wa anga (Air defense system), China alishindwa kumlinda hata Mkuu wa Nchi wa Venezuela alipotoweka. Wachina wameshindwa kabisa na hawana uwezo kurudisha kisiwa chao (Taiwan) ambacho kipo umbali wa kuogelea tu kutoka nchi kavu yao.
Ukweli ni kwamba Hawa wachina Uwezo wao wa kijeshi umejengwa juu ya propaganda, vitisho na maneno matupu ya vyombo vya habari lakini hawana uzoefu(experience) halisi kwenye mapambano ya kisasa ya kijeshi.