Inaniuma sana, nimeamua nitapike ni kisa cha kweli!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inaniuma sana, nimeamua nitapike ni kisa cha kweli!!!!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by leah freddy, Feb 17, 2012.

 1. l

  leah freddy New Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ilikua ni mwaka 2007 nilijiiingiza kwenye tagged, nilipata marafiki wengi sana, mja wa marafiki hao nilimpa number yangu ya simu, kwa bahati mbaya ple nilipokua nafanya kazi nikaachishwa mawasiliano yakawa hafifu, siku moja nikiwa nimepata kazi sehemu nyingine niliingia kwanye mtandao nikamkuta kwa kweli nilifurahi sana, basi tukaendelea kuwasiliana, siku moja akaomba nikutane nae nikawa nakataa, aliendelea kutaka kuonanna nami siku moja niliamua kukubali, basi nikaenda tuka meet some where, nilifurahi sna nae alifurahi sana, akaniuliza backgroudn yangu nae nami nikamuuliza akanieleza, tukaendelea kuwasiliana, wakati huo tuliheshimiana na hatukuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, akanionyesha nyumbani kwake na mimi nikamuonyesha kwetu, siku zilienda miaka ikayoyoma nikawa na furaha nae akawa na furaha, baada ya kama miaka miwili tukajikuta tumejiingiza kwenye mahusiano tulipedana sana na tukapanga mambo mengi ya kiamaisha.
  Ghafla alibadilika akanichukia pasipo sababu akawa ananijibu vibaya nikimuuliza akawa hana cha kuniambia, ilipita week moja pasipo kuonana, week iliyofuata nikamwambia naenda kwake akanikatalia na kunipa short answers. siku moja nilikajikaza nikaenda kwake kabla sijaingia nikakuta jiko viatu vya mwanamke mlangoni na jiko likiwa limewashwa na kwenye cordo kuna mdada anapika. nikamsalimia nikauliza kama jamaa yupo ndani akaniambia ee kabla sijaomba aniitie akawa ametokea sitin , hakutaka niiingie ndani na mimi nilielewa kila kinachoendelea, nikamwomba tutoke nje mara moja na nilijitahidi nisionyeshe kama kuna kitu nimehisi, tulipofika nikamuuliza huku machozi yananilenga lenga kwanini umeamua kunifanyia hivyo alibadilika rangi na hakuweza kunijibu chochte. Kuna promiss alinipa na akaahidi kunisupport kwa hali na mali nikamuuliza kama alikua yupo tauyari akanijibu ndio,basi nikamwambia alll the best. Jamani nilipofika nyumbani niliumia sana ilinigharimu sana, na chaajabu hakutaka hata kuwasiliana na mimi, na ukweli ni kwamba sikuwahi kugombana nae wala kumkosea chochote. Nimiaka miwili sasa hataki kuona na hata sms yangu lakini UKWELI YULE NDO MWANAUME NILIO MPENDA NA MPAKA SAIVI NAMPENDA HAIJALISHI ALINITEDNA, SIPO HAPPY NA MWANAUME YOYOTE, USHAURI PLZ!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  My dear
  maisha hayapo jinsi unavofikiri.relax jiachie duniani humu wanaume ni wengi tena utapata mzuri kuliko huyo utashangaa.
  Sio kila tunachotaka kinakuwa jinsi tutakavo,ishi kwa mbadala baada ya muda ule mbadala utakuwa ndo sahihi tena zaidi ya ufikiriavo
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  pole kwa kupenda usipopendwa jitahidi kufuta namba zake na mawasiliano ya namna yoyote ile halafu usimfikrie sana ni hayo tu..
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Binti wa kike hii ni mikasa ya maisha songa mbele na utampata mwingine ambaye atakufanya usahau yote haya
  Mkasa kama wako uliwahi kunipata ila mie nilifanya suprise ambayo ilinitokea puani,
  Kwa sasa naishi maisha yangu ya furaha na amani
  Huyo si wako na hakupendi tena zoea hiyo hali na jitahidi kumsahau.
   
 5. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Pole sana dada,waswahili husema mpende akupendae na asiye kupenda achana naye,sasa kwa nini unaumia na mtu asiye kupenda.Muombe Mungu atakupa mchumba bora kwani mchumba mzuri hutoka kwa Bwana.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Jibu hapo ni kuwa shukuru Mwenyezi Mungu kampa ujasiri wa kuishia khali badi kweupe.......................wewe bado kijana using'ang'anie uhusiano na yule ambaye unaona haoni dhiki kukuachia maumivu.......................anza kuwasiliana na wanaumme wengineo.......................siyo lazima iwe kimapenzi lakini kuwa na marafiki wengineo....................baada ya muda si mrefu mungu atakuletea mwanaumme bora zaidi ya huyo...............usikubali kusema ya kuwa ni yeye tu................kweli kupenda ni hisia lakini wako wengi ambao utawapenda zaidi ya yule..................nao watakupenda na kukuheshimu sana...............rejection is tough but it comes for a reason.............................mara nyingi ni kukuandaa kwenye uhusiano mwingine na ambao ni bora..........................ukipitia kwenye tanuru la namna hiyo unakomaa.......................na atakapokuja yule ambaye mungu kakuandikia utamthamini sana kwa sababu machungu ya kuachwa wayajua fika.............................usijiulize kwa nini kaniacha.....................mara nyingi hata yeye hajui...................ni moyo wake tu umekuwa mgumu kwako..........................it is nothing personal.............................move on before it is too late to catch another airbus.......................
   
 7. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kisicho riziki hakiliki, hiyo haikuwa riziki yako sahau na jaribu kwingine.
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  pole sana...hayo ndo matatizo ya cyber- marriage
   
 9. Mpiga Nyoka

  Mpiga Nyoka JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Kaza moyo songa mbele siku hazigandi dada yangu na ukiendelea kumuweka moyoni huyo mwanaume unakosa penzi la mpenzi wako afuatae. Don't dwell in the past.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  [h=2][/h]
  Mkuu wangu Leah Freddy!

  Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

  Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

  Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

  Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari 2008 pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

  Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti.

  Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni $940 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

  JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

  Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

  Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa Januari 9, 2009, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

  Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

  Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

  Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

  Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili zaidi ya 35,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 350,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

  Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

  Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

  Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

  Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka (12months, walau 450 kwa mwezi) inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

  Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

  Benki zetu (hapa naongelea walau NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

  Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

  Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.

  =================================

  Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:

  1. Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

  Paypal users:

  Details will follow

  2. Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo Mubyazi wa Dar es Salaam.

  3. Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

  NBC:

  Acc #: 033201064359
  Jina: Maxence Melo Mubyazi

  CRDB:

  Account Name: Maxence Melo Mubyazi
  Bank: CRDB Pugu Road Branch
  Swift Code: CORUTZTZ
  Acc No: 01J2092391800

  4. Njia ya nne:

  Unaweza kutuma recharge vouchers za tiGO, Zain, VodaCom au Zantel au ZAP (0784526444), M-PESA (0755642929), tiGO PESA, Z-PESA n.k kwenda kwa Maxence - 0713444649 naye atakufahamisha kuwa kazipokea. Namba za ZAP, M-PESA na Z-PESA anaweza kukupa ukiwasiliana naye.

  =================================

  Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

  Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

  Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.

   
 11. Geraldo DaVinci

  Geraldo DaVinci JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 277
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  pole sana he wasnt meant for you you will meet your true love someday
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  SHERIA NA KANUNI ZA JAMII FORUMS

  Tafadhali jiepushe na mambo yafuatayo:

  1. Kumvunjia heshima, kumkejeli, kumtukana, mjumbe yeyote.


  Wadau wengi wamekuwa wakiivunja kanuni hii ambayo tulikubaliana tangu 2006; haturuhusu kwa namna yoyote iwayo kuvunjiana heshima kwa makusudi wala matusi kwa namna yoyote iwayo. Mfano: Kuandika neno fvck kwa nia ya kukwepa censorship ni kutukana kwa kudhamiria kabisa, tumelishtukia hili na mara inapobainika hoja husika huondolewa na mhusika kufahamishwa juu ya kosa lake, anapothibitika kuendelea kukaidi basi hufungiwa kwa muda au kufutiwa uanachama kabisa!
  2. Kuleta katika JAMII FORUMS maelezo yenye maudhui mabaya, au kuweza kuleta maudhi yoyote kwa wajumbe ama kwa wingi wake, ukubwa wake, au mfumo wake.


  Hili nalo pia husababisha hoja za watu kufungwa, kufutwa au mhusika kupewa onyo.

  3. Kuleta makala au kuendeleza mijadala yenye kuleta ugomvi, uchochezi na yenye muelekeo wa kutengenishana badala ya kuungana miongoni mwa wajumbe wa JAMII FORUMS na Watanzania wote kwa ujumla.


  Nadhani maelezo yaliyo juu yanajieleza wazi, natamani wengi wangeelewa maana ya maneno hayo juu! JF si sehemu ya kuanzisha uchochezi aidha wa kidini, kisiasa n.k.

  Endapo itabainika umeanzisha hoja kwa nia ya kuibua uchochezi au ugomvi na mtu basi tunasikitika hoja hiyo itakufa HARAKA SANA.
  4. Kuleta maongezi binafsi baina ya mwanachama na mwanachama (waliojisajili) waliyoongea kwa kuaminiana kutoka katika Private Messages (PM) au barua pepe (Emails) na kuyaanika hadharani kwa nia ya kuchafuana.


  Kuna wadau walikuwa na kawaida ya kuwasiliana na wenzao kwa mapenzi yao wenyewe au hata bila wao kuhitaji, namna pekee ya kuwasilisha PM au email ambayo unaona inaleta tatizo kwako si kuibwaga katika hadhara bali kuituma kwetu na sisi tukaifanyia uchunguzi na kubaini ubovu wa PM wenyewe au Email husika ili mhusika achukuliwe hatua za kinidhamu. Tunalichukulia suala la PM na Emails kuwa private, kulileta hadharani ni kutafuta magomvi na kudhalilishana.

  5. Kusambaza kwa makusudi au kwa uzembe barua zenye virusi vya kompyuta.  Kwa bahati hili halijatokea sana JF, threads ambazo zinakuwa zinaonekana kuwa na links ambazo si salama huwa zinaondolewa haraka, aidha waanzishaji wa hoja husika hufahamishwa lakini wakionekana kukaidi hatuna sababu za kuendelea kuwasiliana nao badala ya kuwafungia kwa muda (kutokana na kukaidi) na kisha kuanza kuwa-monitor kadiri siku zinavyokwenda.
  6. Kutoa maelezo au shutuma dhidi ya mwanachama mwenzako, kiongozi wa au watu wenye hadhi kijamii bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwa lengo la kuchafua rekodi safi ya mhusika kijamii.


  Wahusika mnaovunja sheria hii mnajua athari yake; tunaweza kuwa tunachukizwa na kitu flani kilichofanywa na kiongozi flani ndani ya serikali au kidini, kuanzisha shutma ambazo zinalenga kumchafua mtu bila kuwa na ushahidi ni kutaka kumchafulia jina mhusika. JF si sehemu ya kuchafuliana majina, hatua za kinidhamu huchukuliwa kwa wale wenye nia ya kuitumia JF kwa maslahi yao binafsi.
  7. Ni sharti kwa kila mwanachama kutoa maelezo au mchango wake kwa uwazi na ukweli na kutomuogopa yeyote wala kumpendelea yeyote bali kuweka mbele maslahi ya taifa.


  Tunaheshimu SANA hoja za kila mmoja, kuna wadau walikuwa wanadhani huenda wao si mali kitu hapa JF, tunatambua kuwa Mwenyezi Mungu katujalia karama tofauti, lakini wakati huohuo tunaamini kila mmoja anaweza kubadilika kadiri siku zinavyokwenda. Hakuna mwanachama wetu ambaye tunamwona "mbabe" dhidi ya wenzake, wote ni sawa mbele zetu na tunawapa heshima sawa.
  Hatua za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa dhidi ya yeyote yule atakayeshindwa kuzingatia maelezo hayo hapo juu.  Hii si sheria bali ni angalizo tu.
  ==========================

  Other Rules to be noted:

  1 - Flaming, Bashing, and Trolling:
  Hate posts and personal attacks will not be tolerated on the boards. Treat others on these message boards as you would expect them to treat you. Posting topics specifically designed to provoke a negative response from someone (aka trolling) is also asked to be avoided.
  Nadhani nimeigusia hii hapo juu, lakini ni msisitizo zaidi.

  2 - Profanity:
  Profanity is not tolerated in the board, some words will be censored, also there is to be no name calling, doing so will give you a warning, and then a ban if you continue.
  Maelezo ya hapo juu hasa yenye rangi nyekundu hupelekea posts nyingi kuondoshwa na pengine wahusika KUFUNGIWA kwa muda!

  3 - Spam:
  Purposely spamming a message board with senseless, vacuous, or empty messages to gain a higher post count, or just to annoy others is HIGHLY frowned upon! Commercial spamming and advertising are just as unwelcome unless it is done in the special designed area. Promoting your site is only allowed with permission of the site owners. Bumping old threads is allowed in the request forums, but needless bumps in other forums will be classed as spam.  Niliyoiwekea rangi nyekundu mkuu MS aliianza, mdau mwingine (Shy) naye amekuwa akiweka links kibao kwenye post zake, sharing is caring... Lakini sharing inapofanyika hapa JF ni vema kuweka content husika kisha utoe CREDIT kwa chanzo cha habari, haipendezi kubwaga habari JF bila kuweka chanzo (credit) cha habari. Japo kuna vyombo huchukua habari zetu hapa bila kutu-credit lakini sisi bado tunasisitiza wanachama wetu kuona umuhimu wa kuthamini vyanzo vya habari zetu.
  4 - Email & Private Message Spam:
  If the members are using the private message facility to spam the others with pointless, unsolicited mail they will be banned. If anyone receives one of these messages, please contact an admin immediately.


  Hili tulilisisitiza kuwa endapo litawatokea wanachama basi wawasiliane nasi haraka. Wanaoonekana kutuma malalamiko ni wachache na hatua huchukuliwa.

  5 - Piracy, and Warez:
  We do not mind discussions about piracy or warez, as long as they are just that...discussions. Linking or giving information about any site that distributes illegal software, or warez, seeking help to circumvent any copyright laws, or encouraging software or media piracy grounds for an immediate ban.  Inajieleza

  6 - Impersonating Other Users / Accessing Another User Account:
  You may not impersonate another board member or create an account specifically for the purpose of provoking other users. Also, accessing or using someone else's account or attempting to access another poster's account is strictly prohibited. You will be banned.  Mpaka sasa hatujapokea malalamiko ya kuvunjwa kwa sheria hii lakini ipo

  7 - Off-Topic Posts:
  There is no major punishment for off-topic posters. But lets be honest, it drives us all mad!! If you have something to say but it really has nothing to do with the current thread you are in, please open a new thread for it. Otherwise it will just be deleted and won't solve anything at all.  Wengi wamekuwa wakiivunja hii makusudi kabisa; wanaanzisha salaam ndani ya topic na mods huchukua hatua za kuondoa kila post yenye kuwa nje ya hoja au wanapoona topic imejaa majibizano yasiyo na tija kwa jamii basi topic nzima hufungwa au kuondolewa kabisa. Aidha, kuanzisha mjadala wa kidini sehemu ya siasa wakati kuna jukwaa la dini ni kukosea, mods huhamisha mjadala husika kwenda jukwaa husika wakiwa wameacha redirection na ukibonyeza title ya topic husika utajikuta unaendelea kuisoma katika location mpya.

  Ieleweke kuwa kila post ambayo inaondolewa kwenye public domain ipo; zinabaki kwa ushahidi siku za usoni maana wengine hukana kuwa walifanya makosa wanayoambiwa walifanya; hatufuti MOJA KWA MOJA, zinawekwa sehemu kwa ajili ya reference za makosa ya wanachama wetu.

  8 - Circumventing a Ban:
  If you log onto the forums and receive a message that you have been banned, please submit an unban request and wait for a staff member to get in touch with you. You may NOT re register under a new name if the software lets you. But, if you try to sign up again and we caught you, then it will become a permanent IP Ban. We do NOT send out notices that you have been banned.  Inajieleza wazi tu. "Member flani" kuna kipindi alikosea kulingana na mojawapo ya sheria lakini alipogundua aka-submit unban request nasi tukawasiliana na yule ambaye walikuwa wamekoseana na wakakubaliana kuwa yameisha na akafunguliwa. Tunatambua kuwa wote huwa tunajikuta tumepandwa na jazba na wakati mwingine kutoa kauli ambazo si za kiungwana, uungwana ni vitendo, ukigundua umekosea ukaomba radhi basi utasamehewa!
  9 - Nudity / Porn:
  Please remember that this board is a PUBLIC forum. There are 12 year olds here just as there are 50 year olds. Nudity and porn is prohibited for obvious reasons.  Inajieleza

  10 - Signatures & Avatars:
  We do not have any specific set of rules regarding signatures. However, we do ask you that it will not be offensive to others and the length should be within reason. If you desire to have a custom avatar, it must be 100x100 pixels or less. No adult, drug related or racist content please.  Signatures za watu wengine huwa ndefu SANA, au zina maneno yasiyo na heshima kabisa. Huwa tunaziondoa na kumfahamisha mhusika, akionekana kuwa mbishi basi ananyimwa access ya kuwa na signature. Hii pia hujitokeza kwa avatars.
  11. Do not post any copyrighted material unless the copyright is owned by you, except for brief credited excerpts to illustrate a point;


  Inarejea kulekule, kuwa ni vema unapochukua content kokote haijalishi ni copyrighted au sio copyrighted, basi toa credit ya chanzo cha habari usiibwage as if ni wewe umeandaa hoja husika.
  12. You will not post what is commonly called spam, which includes but is not limited to such things as advertisements, chain letters, pyramid schemes, solicitations, or promoting a particular cause or organization. Exceptions may be granted for worthy (in our sole opinion) causes if you obtain prior permission from us;

  13. We reserve the right to ban any user temporarily or permanently, refuse posting from screen names we find offensive, edit or delete any post, limit postings on any topic, and shut down any topic altogether, for any reason, or no reason, without explanation or warning.

  14. You are solely responsible for the content of your messages. We cannot verify content and thus accept no responsibility for it, nor do we vouch for the accuracy, completeness, or utility, of any message or the qualifications of any user.

  15. Do not post private messages at JamiiForums or elsewhere without the express permission of the sender of the Private Message.

  16. Do not engage in internet stalking. This includes, but is not limited to, following a JamiiForums member from site to site, or from thread to thread within this site; taking posts from JamiiForums in order to attack a poster at another site; and attempting to defame or discredit JamiiForums members on other sites for views they may have expressed at JamiiForums.


  Hizo juu zinajieleza; ingawa nyingine ni kama zinajirudia

  17 - Questionable Content:
  Since we can't have a rule to cover everything, this is the rule to, well, cover everything. These are public boards, so act like you would if you were in a public place. These issues are left to the discretion of the individual moderators, but may include any material that is knowingly false and or defamatory, misleading, inaccurate, abusive, vulgar, hateful, harassing, obscene, profane, sexually oriented, threatening, invasive of a person's privacy, that otherwise violates any law, or that encourages conduct constituting a criminal offense.


  Na hii ndo huwapa mods kazi ngumu, wanajaribu kuzipitia threads kuangalia kama zinastahili kubakia katika public domain au zinavunja yale niliyoonyesha kwa rangi nyekundu hapo juu.... Inakuwa ni mtihani lakini kwa ushirikiano wa members wanaojali basi huzifanyia kazi accordingly.

  IELEWEKE KUWA:

  JF kamwe haitamsimamia au kumpendelea mtu kwa sababu ya DINI yake au ITIKADI YA KISIASA aliyokuwa nayo.

  Tutaendelea kutoa uhuru, hatuwezi kumfungia mtu kwakuwa hupendi anavyopingana na mtizamo wako wa kisiasa au kidini; kama huwezi kujizibizana naye kaa mbali naye.

  Hatutamwonea huruma yeyote anayeonekana kutaka kuvunja sheria kwa kisingizio chochote kile; endapo unaona kuna mtu kaenda kombo na sheria hizi usisite kuwasiliana nasi, unaweza kubonyeza CONTACT US ambayo ipo kwenye 'bar' ya bluu hapo juu au hata kutumia barua pepe kwenda support@jamiiforums.com ili hatua za haraka zichukuliwe.

  Naamini nimeyajibu maswali ya baadhi ya watu. Topic hii haihusiani na siasa wala uchaguzi lakini kuelekea uchaguzi tunajua wengi watakuwa wanavunja sheria makusudi katika jukwaa hili hivyo tukaonelea vema tuweke bayana haya ili maamuzi yanapochukuliwa wajue ni misingi gani imefuatwa.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Pole binti, u r still living in the past

  Tatizo ni lipi sasa hapo au kwakuwa aliku promise kukusaidia hali na mali?
   
 14. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole najua namna unavojisikia,ilishanipata siku moja but amin nakwambia ipo siku utalifurahia tukio hili na kumshukuru mungu kwa kilio cha furaha,

  Nakushauri uruhusu moyo ukubali matokeo japo si rahasi but u have to do it!kubali na kuamini kuwa huyo hakuwa wako na ilikuwa lzm muachane tu hata km isingekuwa wakati huu ili ampishe aliyeumbwa kwa ajili yako achukue nafasi yake siku moja,

  Pia mbele ya safari utaona faida ya kuachwa kwan kuanzia hapo utaijua thamani ya mapnz kwa utakayempata kwan utakua unaujua uchungu wake,

  Mwombe mungu akupe ujasiri na kusahau kwa kujichanganya na watu,ji keep busy,usiruhusu mawazo yake au ya tukio kukutawala,amini wapo wanaojua kupenda zaidi yake,na wa kwako yuko njian na ipo siku mtakutana na yote yatakuwa historia and u will be happy again and forever!!!
   
 15. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  PakaJimmy
  majibu yako na hii poster hayaendani kabisa yaani. . Ye anaongelea hisia zake kwa mpenziwe ..
  We unaongelea michango ya JF ... duhh
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  I think he was the rong mana to you that's why God show you early before get marrage so ilopo mshukuru Mungu kwa kila jambo
   
 17. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu, sio kweli.........watu wanakutana na wanapendana popote, na wanaachana au kuumizana!
  Haijalishi wamekutana wapi.
   
 18. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni post yake ya kwanza.........kama ada, PJ kampa sharia na taratibu za JF.
   
 19. juma sal

  juma sal Senior Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  oyo achana nae .......si hakupendi jamani....ww kwani unaweza kukumkubali yeyote yule kwa sababu tu yeye anakupenda?
   
 20. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nawe wakati umejiunga thread yako ya kwanza kuirusha hewani huyu jimmy paka akakupa hii kitu au kabla ya kujiunga unasoma masharti na kanuni zote za JF,?
   
Loading...