Inakuwaje Wizara nyeti bajeti yake inafyekwa?

Haya maelezo ya kupunguza bajeti ya afya kwa 20% ni ya kipuuzi kabisa. Pesa ya kununua ndege ipo, pesa ya kutoa rushwa kwa Wabunge wa CCM ipo, pesa ya kujenga Airport uchwara Chato ipo, pesa ya kununua wachumia tumbo akina tumbili na wenzake ipo na wakati huo huo wanafyeka kwa 20% bajeti ya afya!!!!

Sababu ya serikali kupunguza bajeti ya Wizara ya Afya Hizi Hapa

xUMMYBEAUTY.jpg.pagespeed.ic.SGnchAdG3a.jpg

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema kuwa, kupungua kwa asilimia 19.6 bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19 ikilinganishwa na mwana 2017/18 kunatokana na dhamira ya serikali kutekeleza bajeti hiyo kwa kutumia fedha za ndani ya nchi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuka ameeleza kuwa, wabunge walishauri serikali ipunguze utegemezi kutoka kwa wafadhili katika kutekeleza bajeti ya afya.

Katika mwaka wa fedha 2017/18, bajeti ya wizara hiyo ilikuwa TZS 1.07 trilioni lakini kwa mwaka 2018/19 imepungua na kufikia TZS 898.3 bilioni.

“Kilichotokea, bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka huu fedha za ndani zimeongezeka kutoka TZS 628 bilioni hadi kufikia TZS 681 bilioni,lakini fedha kutoka kwa wafadhili zimepungua,” alisema Waziri.

Waziri Ummy alisema kuwa, dhamira hiyo inaonsha nia ya Rais Dkt Magufuli kupunguza utegemezi wa wadau wa maendeleo katika kupunguza changamoto za Watanzania.

Alisema kuwa, lengo ni kuona kwa namna gani serikali kwa kujitegemea yenyewe inaweza kutekeleza bajeti yake.

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilieleza kuwa, kupungua huko kwa bajeti ya Wizara ya Afya kwa asilimia 19.6 kunaweza kuathiri utaoji huduma za afya.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba alisema katika mwaka wa fedha 2017/18, fungu la fedha za maendeleo, wizara ya afya ilitengewa TZS 785 bilioni, lakini hadi kufikia Februari TZS 385.77 bilioni sawa na 49% kilipokelewa na kutekeleza miradi.

Alibainisha kuwa, katika fedha hizo za maendeleo, TZS 336.3 bilioni ni kutoka vyanzo vya ndani na 449.5 ni kutoka vyanzo vya nje.

“Kamati imebaini fedha zilizopokewa kutoka vyanzo vya ndani ni TZS 64.7 bilioni sawa na 19% ya fedha zilizoainishwa. Pia, fedha za nje zilizopokewa ni TZS 321 bilioni sawa na asilimia 71,” alisema Serukamba.
Duh! Eeee bhana eeeee !!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukikutana na watu kama Polepole hapo utawasikia: "Hiyo sio kwamba imefyekwa; acheni upotoshaji! Hiyo inaitwa pre-expenditure accrual by health cash ambayo; kutokana na mfumo mpya, inakuwa credited kwenye Hati Fungani!" PUMBAAAVU!!

Unakusanya mapato pungufu lakini ili uonekane unakusanya nyingi; unahesabia hata ambazo hazipaswi kuwa kwenye mahesabu yako!

Na zile zilizopatikana badala ya kuzipeleka kwenye huduma za msingi; unaenda kuzipeleka kwenye white elephant projects huku zingine zikikosa maelezo ya kuridhisha kuhusu allocation zake!

Matokeo yake ndo haya! Huduma za msingi zinapigwa panga!!

Wakati CAG Report ikionesha ongezeko kubwa la gharama matibabu ya nje ya nchi; Bajeti ya Wizara ya Afya inapigwa punguzo kubwa namna hiyo ili bila shaka gharama ya matibabu nje nchi izidi kupaa! Sina shaka kwenye hizi ongezeko la hizi gharama ndiko wanakopatia fursa ya kuiba fedha za Watanzania!!
wanajificha kwenye hati fungani, (receivables), na hela ya Zanzibar,

kama hizo hela hazijatumika basi hiyo naksi ya trial 1.5 ni mapato hewa ya TRA waliyokuwa wanatangaza kwa mbwembwe, na huenda ni zaidi ya trial.1.5.
tukubaliane kuwa mapato ya mwezi ya TRA yalishuka mpaka mil 800-900 kwa mwezi. kwa figure hizi hesabu za mwaka 2016/2017 zitabalance
 
Haya maelezo ya kupunguza bajeti ya afya kwa 20% ni ya kipuuzi kabisa. Pesa ya kununua ndege ipo, pesa ya kutoa rushwa kwa Wabunge wa CCM ipo, pesa ya kujenga Airport uchwara Chato ipo, pesa ya kununua wachumia tumbo akina tumbili na wenzake ipo na wakati huo huo wanafyeka kwa 20% bajeti ya afya!!!!

Sababu ya serikali kupunguza bajeti ya Wizara ya Afya Hizi Hapa

xUMMYBEAUTY.jpg.pagespeed.ic.SGnchAdG3a.jpg

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema kuwa, kupungua kwa asilimia 19.6 bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19 ikilinganishwa na mwana 2017/18 kunatokana na dhamira ya serikali kutekeleza bajeti hiyo kwa kutumia fedha za ndani ya nchi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuka ameeleza kuwa, wabunge walishauri serikali ipunguze utegemezi kutoka kwa wafadhili katika kutekeleza bajeti ya afya.

Katika mwaka wa fedha 2017/18, bajeti ya wizara hiyo ilikuwa TZS 1.07 trilioni lakini kwa mwaka 2018/19 imepungua na kufikia TZS 898.3 bilioni.

“Kilichotokea, bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka huu fedha za ndani zimeongezeka kutoka TZS 628 bilioni hadi kufikia TZS 681 bilioni,lakini fedha kutoka kwa wafadhili zimepungua,” alisema Waziri.

Waziri Ummy alisema kuwa, dhamira hiyo inaonsha nia ya Rais Dkt Magufuli kupunguza utegemezi wa wadau wa maendeleo katika kupunguza changamoto za Watanzania.

Alisema kuwa, lengo ni kuona kwa namna gani serikali kwa kujitegemea yenyewe inaweza kutekeleza bajeti yake.

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilieleza kuwa, kupungua huko kwa bajeti ya Wizara ya Afya kwa asilimia 19.6 kunaweza kuathiri utaoji huduma za afya.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba alisema katika mwaka wa fedha 2017/18, fungu la fedha za maendeleo, wizara ya afya ilitengewa TZS 785 bilioni, lakini hadi kufikia Februari TZS 385.77 bilioni sawa na 49% kilipokelewa na kutekeleza miradi.

Alibainisha kuwa, katika fedha hizo za maendeleo, TZS 336.3 bilioni ni kutoka vyanzo vya ndani na 449.5 ni kutoka vyanzo vya nje.

“Kamati imebaini fedha zilizopokewa kutoka vyanzo vya ndani ni TZS 64.7 bilioni sawa na 19% ya fedha zilizoainishwa. Pia, fedha za nje zilizopokewa ni TZS 321 bilioni sawa na asilimia 71,” alisema Serukamba.
Sasa za fedha za ndani ni sh 64.7b na nje ni zaidi ya 300b utasemaje pesa za ndani zimeongezeka?
 
Tuliambiwa kwamba Serikali ina pesa nyingi sana, sasa kama hilo ni ukweli iweje bajeti ya afya ifyekwe? Bunge liliidhinisha bilioni 2 kwa ajili ya Chato Airport lakini zilizotumika ni zaidi ya bilioni 300. Iweje bajeti ya Chato iongezwe bila idhini ya Bunge na wakati huo huo ile ya afya wakipewa 53%?

Kuna tatizo tena ni tatizo kubwa sana la mambo kufanyika holela holela tu huku maamuzi ya Bunge yakiwa hayaheshimiwi hata chembe.
Waache wapuuzwe, kwa nini?...
  • Kama wanaikumbatia serikali na kuweka mahaba ya chama na wananchi wanufaika nao iweje wasionekane .....?
  • Kama wanachaguliwa viongozi na chama/serikali na wanabariki, iweje wasichezeshwe sindimba?
  • Kama wengi wao wanaendesha bunge kimipasho, kwa nini serikali isiwakolezee biti za taarabu?
  • Kama wao wanapitisha maamuzi ya kigezo cha kupata ubunge ni elimu ya darasa la saba, iweje asikimbizwe na PhD? Atashindana naye kwa uwezo upi wa kujenga hoja hata kama ni uongo? Haana uwezo wa kujua hili baya kwake yote kheri... kisa anakalia kiti kizuri, nyumba nzuri, gari zuri, uheshimiwa, wacha walio wachagua wavute vumbi wakipata hata mkia watashuru na kukweza.... Kipofu haoni mbalamwezi.
  • Kama pongezi ni kwa kila kitu bila kuangalia jambo kwa ukweli wake, utaachaje kuburuzwa?
  • Elimu darasa la saba eti ndiye mtunga sheria tena kwa kimombo.... hapo kama siyo mazingaombwe ni nini?
  • Kama unatoa pongezi, unaomba msaada kisha unaunga mkono hoja, iweje
  • Kama wanaambiwa mapato yaliyokusanywa ila matumizi hayaeleweki na hawahoji bali kupongeza, unategemea nini kwa mgema akisifiwa?
  • Bado tupo tupo sana hadi ngozi zitakapo badirika....
Barikiwa sana!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom