Inakuwaje Syria, Somali, Iraq, Congo zinatuzidi kwa Furaha

mpiga domo

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
852
1,505
Habari Wakuu,

Leo kwenye gazeti la New York Times nimeona tumeshika tatu mkia kati ya nchi ambazo wananchi wake hawana furaha. Syria pia yupo juu yetu. Inakuwaje wakuu hadi North Korea wananchi wake wana furaha kuliko siye. Hadi Somali ambapo watu wanajitoa mhanga kila siku.

Unaweza kuhisi sababu ni nini, ama tufanye nin.
 
Mzee wetu Nyerere alituambia, kadri wanavyotuona tuna msimamo, wataanza kutuzomea .....huyooo huyooo, wamechanyikiwa, wapigeni mawe, huyoo huyooo.....!!!!. Usiyashangae magazeti kama hayo, wana ajenda zao za chini chini.
 
Nimeiona hiyo habari Yahoo news.
Ni utafiti unaofanyika dunia nzima kila baada ya miaka fulani.
Imeshirikisha nchi 155.
Norway ndio ya kwanza ikifuatiwa na Nordic countries nyingine,U.S imedrop from 13 to 14 na Central African Republic ndio ya mwisho,huku Tanzania,Syria,Rwanda,Burundi zikiwa mkiani kabisa.
Wametumia vigezo mbalimbali kama uwezo wa kiuchumi wa mtu mmoja mmoja,uhuru wa kujiamulia mambo,uwezekano wa kupata msaada mtu anapopata shida,
 
Huwezi kuwa na nchi yenye furaha kama wananchi wake wambea wambea, wanafiki, wasengenyaji. Ugomvi wa gwajima na bashite Upo tena na upande umechagua. Uglmvi wa kiba na mondi una team. Mange na serikali Upo una team. Arsernal ikifungwa unajaza mitusi kwenye post ya arsener Wenger. Mkikosa miss Tanzania kutwaaa mitusi kwenye page ya watu. Ugomvi wa davido na mond Upo na team. Korea kaskazini kurusha makombora wewe mshipa unakusimama. Trump kashinda marekani wewe unazila na kusononeka ata kula huli. Madaktari wamepewa shavu kwenda kufanya kazi Kenya umenuna. Hiyo furaha inatoka wapi...?

Hatuwezi kuwa na furaha kama wambea na washakunaku. Hao somalia umeskia lini wanatukana kwenye page za watu. Umewahi skia mange msomali...?

Umbea umbea na unafiki watanzania ndo mana ata tunakufa mapema. Mda wote una stress kichwani sijui lissu atasema nini Leo. Sijui mange atakiwasha wapi Leo yarabb. Sijui north Korea ataipiga lini south Korea nishuhudie vita ya 3 ya dunia.

Tuache umbea tutaishi Kwa furaha.
 
kupigana vita ni moja ya njia za kuondoa dukuduku moyoni,kama unaonewa na huwezi kupigana matokeo yake ndo haya
We MsomaliA Nenda kwenu .Kwanini usiwe wazi tu Kipimo majungu .Watanzania Popote hatupendani .tembea u one. Wivu sana. Unaona kabisa Wenzetu Wanapeana sna kampan sisi. Majungu sana. Kila dhambi sasa twatend ila ukiona hujakamatwa unamnyoshea kidole aliyeshikwa., rudi kwenu hujajua vita au unataka kutuletea majanga
 
Izo ni mbwembwe za watu weupe wakishaona kiongozi fulan Wa afrika anafanya kazi basi wanaanza kumshambulia indirectly.... Toka lini Syria..somalia watuzidi furaha?¿???? Wamagaribi washenzi tuuu ....hata gadafi naye kabla hawajamtungua walianza kusema ivo taratibu wakawa wanapandikiza mbegu yachuki kwa kundi dogo lilokua likimpinga mwisho wakalisaidia I'lo kundi na wakamuua gadafi ..
 
Habari Wakuu,

Leo kwenye gazeti la New York Times nimeona tumeshika tatu mkia kati ya nchi ambazo wananchi wake hawana furaha. Syria pia yupo juu yetu. Inakuwaje wakuu hadi North Korea wananchi wake wana furaha kuliko siye. Hadi Somali ambapo watu wanajitoa mhanga kila siku.

Unaweza kuhisi sababu ni nini, ama tufanye nin.
Kuna msemo unasema chizi kapewa lungu ndiyo sababu chizi akipewa lungu atajifuraisha mwenyewe
 
Sasa ww unavamiwa na mkuu wa mkoa.. Furaha hiyo utapata wap??
Acha ujinga, hii si ajenda. Kuna matukio makubwa zaidi ya hili hiko mnakosema kuna furaha, lakini hayatiliwi maanani. Wale polisi wanaowaua waafrika kule USA utasema kuna furaha? Tz tuna tabia ya kukuza jambo tu. Hadi inakera. Halafu tun apeleka yetu kwao wakat yao yaliyo makubwa zaidi wanapotezea. Huu ni uzezeta. Snowdern kaifanyia nn Marekani. Lakini umesikia wanapiga kelele? Nini kilitokea ktk uchaguzi wa marekani. Ungekuwa kwetu eti wamechakachua. Sisi ni wapumbavu, wambea, wanafiki na tunafikiri kwa kucha.
 
Habari Wakuu,

Leo kwenye gazeti la New York Times nimeona tumeshika tatu mkia kati ya nchi ambazo wananchi wake hawana furaha. Syria pia yupo juu yetu. Inakuwaje wakuu hadi North Korea wananchi wake wana furaha kuliko siye. Hadi Somali ambapo watu wanajitoa mhanga kila siku.

Unaweza kuhisi sababu ni nini, ama tufanye nin.
Labda Tanzania Kaskazini ndoo hawana furaha lakini sisi maeneo mengine ya Tz ni furaha kwa kwenda mbele.
 
Huwezi kuwa na nchi yenye furaha kama wananchi wake wambea wambea, wanafiki, wasengenyaji. Ugomvi wa gwajima na bashite Upo tena na upande umechagua. Uglmvi wa kiba na mondi una team. Mange na serikali Upo una team. Arsernal ikifungwa unajaza mitusi kwenye post ya arsener Wenger. Mkikosa miss Tanzania kutwaaa mitusi kwenye page ya watu. Ugomvi wa davido na mond Upo na team. Korea kaskazini kurusha makombora wewe mshipa unakusimama. Trump kashinda marekani wewe unazila na kusononeka ata kula huli. Madaktari wamepewa shavu kwenda kufanya kazi Kenya umenuna. Hiyo furaha inatoka wapi...?

Hatuwezi kuwa na furaha kama wambea na washakunaku. Hao somalia umeskia lini wanatukana kwenye page za watu. Umewahi skia mange msomali...?

Umbea umbea na unafiki watanzania ndo mana ata tunakufa mapema. Mda wote una stress kichwani sijui lissu atasema nini Leo. Sijui mange atakiwasha wapi Leo yarabb. Sijui north Korea ataipiga lini south Korea nishuhudie vita ya 3 ya dunia.

Tuache umbea tutaishi Kwa furaha.
Mkuu umefanya utafiti wako na wewe kugundua kwamba umbeya ndo umetufanya tushike mkia au pia na wewe unaleta mambo ya ubuyu kwenye utafiti?
 
Back
Top Bottom