Inakuwaje pamoja na mbwembwe zote kila mpinzani anayetoka kuhojiwa polisi anaufyata?

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,367
Wadau, amani iwe kwenu.

Kumekuwepo na matamshi ya hawa ndugu zetu wa upinzani kuwa wanaonewa na kwamba polisi inatumika kukandamiza upinzani. Wamekuwa wakisema kwa mbwembwe zote kwamba hawapo tayari kuona jeshi la polisi likitumika kuwakandamiza na kwamba wapo tayari kupambana nao na wengine wamefikia hatua ya kusema wapo tayari kushtakiwa, kufungwa na hata kufa kwa lengo la kutetea demokrasia.

Ila cha kushangaza, hakika yametokea mabadiliko makubwa sana ya kauli za wapinzani. Alianza Lowasa kuwa hatambui matokeo ya Urais mpaka anaingia kaburini. Huyu hajahojiwa lakini ishara zote zinaonesha kuwa amemkubali Rais na sasa ameufyata.

Akaja Zitto Kabwe na madai kuwa Rais ni dikteta na alienda Rwanda kujifunza jinsi ya kukandamiza wapinzani. Baada ya kuhojiwa na polisi, huyu naye ameufyata na sasa amebaki kutweet tu kwenye twitter.

Tundu Lissu aliongea kwa mbwembwe pale Kisutu na madai yake ya Rais Uchwara. Naye licha ya kuahidi kuwa ataendelea kupaza sauti, ni zaidi ya wiki sasa hajaonekana kwenye media.

Freeman Mbowe pia alitokwa mapovu kule kanda ya Ziwa ambako walilenga kufanya fujo. Baada ya kuhojiwa na polisi, hakika amekuwa wa baridi kama maji mtungini.

Kuna Mmasai mmoja anaitwa Ole Sosopi. Huyu ndiye aliyewaamrisha BAVICHA kupambana na Polisi mitaani. Alipokamatwa na kuhojiwa, eti leo hii amekuwa rafiki wa polisi na anasema atashirikiana nao kukwamisha mkutano wa CCM. Leo pia anahojiwa na nina hakika kuwa baada ya hapo atapotea kabisa kwenye majukwaa.

Nilipongeze jeshi la polisi kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha na weledi mkubwa. Hawa wapinzani wanajua kuwa wanatenda kosa ila wanatafuta tu kick ya kujulikana mitaani. Nimpongeze pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa kuliagiza jeshi la polisi kushughulika na wale tu vinara wa uchochezi na si wafuasi wao. Njia hii inaonekana kufanya kazi kwani tayari wameshaufyata.
 
Kwanini watu tumekuwa wazushi hivi? Hizi habari zinazoenea kwenye mtandao wa whatsapp juu ya ajali ya msata lengo lake ni nini?
 
Hakika Mkuu. Ndio maana wakitoka kuhojiwa polisi wanakuwa wabaridiiiii
Uzi wako hauna mashiko kwasababu jeshi la policcm like kwa maslahi ya magamba aka chama mfu,chama cha majipu, chama cha mafisadi , chama cha malori....policcm ni vibaraka wa magamba wanatumwa kulinda magamba
 
Kweli kabisa Mkuu. Yaani siwapendi wapinzani ila inafika wakati huruma ya kibinadamu inanijia.
Mkuu usidanganye, hakuna huruma inayoweza kukujia kwa mtu usiyempenda. Kumbuka kutompenda mtu kuna kitu unakuwa umejenga ndani ya moyo wako ambacho ni 'chuki'. Ukishakuwa na chuki ndani ya moyo wako unakosa huruma, upendo na amani. Kama huwapendi wapinzani maana yake ni hiyo...huna huruma huna upendo na huna amani nao.
 
Usifanye mchezo na polisi .
Majambazi na wahalifu sugu tu huwa wanakubali makosa baada ya mateso makali itakuwa hao wanasiasa.
Huwa wanabinya makende ndio maana wakitoka polisi wanaufyata.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kumekuwepo na matamshi ya hawa ndugu zetu wa upinzani kuwa wanaonewa na kwamba polisi inatumika kukandamiza upinzani. Wamekuwa wakisema kwa mbwembwe zote kwamba hawapo tayari kuona jeshi la polisi likitumika kuwakandamiza na kwamba wapo tayari kupambana nao na wengine wamefikia hatua ya kusema wapo tayari kushtakiwa, kufungwa na hata kufa kwa lengo la kutetea demokrasia.

Ila cha kushangaza, hakika yametokea mabadiliko makubwa sana ya kauli za wapinzani. Alianza Lowasa kuwa hatambui matokeo ya Urais mpaka anaingia kaburini. Huyu hajahojiwa lakini ishara zote zinaonesha kuwa amemkubali Rais na sasa ameufyata.

Akaja Zitto Kabwe na madai kuwa Rais ni dikteta na alienda Rwanda kujifunza jinsi ya kukandamiza wapinzani. Baada ya kuhojiwa na polisi, huyu naye ameufyata na sasa amebaki kutweet tu kwenye twitter.

Tundu Lissu aliongea kwa mbwembwe pale Kisutu na madai yake ya Rais Uchwara. Naye licha ya kuahidi kuwa ataendelea kupaza sauti, ni zaidi ya wiki sasa hajaonekana kwenye media.

Freeman Mbowe pia alitokwa mapovu kule kanda ya Ziwa ambako walilenga kufanya fujo. Baada ya kuhojiwa na polisi, hakika amekuwa wa baridi kama maji mtungini.

Kuna Mmasai mmoja anaitwa Ole Sosopi. Huyu ndiye aliyewaamrisha BAVICHA kupambana na Polisi mitaani. Alipokamatwa na kuhojiwa, eti leo hii amekuwa rafiki wa polisi na anasema atashirikiana nao kukwamisha mkutano wa CCM. Leo pia anahojiwa na nina hakika kuwa baada ya hapo atapotea kabisa kwenye majukwaa.

Nilipongeze jeshi la polisi kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha na weledi mkubwa. Hawa wapinzani wanajua kuwa wanatenda kosa ila wanatafuta tu kick ya kujulikana mitaani. Nimpongeze pia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa kuliagiza jeshi la polisi kushughulika na wale tu vinara wa uchochezi na si wafuasi wao. Njia hii inaonekana kufanya kazi kwani tayari wameshaufyata.
Hata hilo nalo hulijui. Kwa sababu ni wapenda amani na wanafuata sheria bila shuruti. Kubambakiziwa kesi hakuna mtu anaweza kuepuka lakini ukishaeleweshwa hili halitakiwi ndio unarudi kwaenye mstari
 
Mi nadhani wangemhoji manager wa maigizo ndugu fisadi papa lowassa
Nadhani wanasubiri aendelee kujichanganya. Ila jamaa machale yanamcheza. Akiona jinsi vijana wake wanavyoshughulikiwa hakika analazimika kujificha
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom