Inakuwaje hatuwezi hata kutengeneza charger ya simu?

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
17,079
Reaction score
12,313
Nimezunguka madukani kuna kila aina ya charger, za simu, za sola, za taa, sasa! Inakuwaje hatuwezi hata kutengeneza charger za simu? Ni elimu gani wahandisi wa udsm sua dit ambazo wanahitaji kuweza hii kazi ndogo? Au hadi wapate teuzi za jpm ndo waweze?
 
Hebu tu changiane mawazo hapa kati ya zipi yaeza kuwa ndo point ya swali le2

low wages

Poor science and technology

Poor transport and communication

Corruption
Poor garvament polcy

Ccm tangu 1961

Poor power supply (tanesco)

low lever of education(waliofika chuo ni elimu ya kukariri madesa)

MANA HIZI POINT NILI2MIA SANA SEKONDAR
 
Nimezunguka madukani kuna kila aina ya charger, za simu, za sola, za taa, sasa! Inakuwaje hatuwezi hata kutengeneza charger za simu? Ni elimu gani wahandisi wa udsm sua dit ambazo wanahitaji kuweza hii kazi ndogo? Au hadi wapate teuzi za jpm ndo waweze?

shida inakuja kwamba , atatengeneza ila bei itakua kubwa, mchina anauza 2000, wewe utataka uuze 3000 maana bila ivyo hupati faida, maana vifaa vyote(materials) umenunua uko uko china

ni sawa na utengeneze gari, utanunua vyuma say kutoka china, utatengeneza chassis, aya utanunua

utanunua ready-made engine, kutoka china, unakuta materials nyingi unaagizia unafanya assembly mwisho wa siku product bei iko juu

wakati mchina anauza chaja ya mpaka buku, wewe umetumia buku 3 kununua items na kutengeneza chaja ile ile!
 
Ukiangalia kwa undani hili ni tatizo la Waafrika wote kusini ya sahara, tumebweteka mno ,utashangaa kijana akitengeneza kiredio tu Tv zote zitaonesha na watu na degree zao wanatoa macho kama hawaamini vile.Sijui katuroga nani
 
Elimu zetu zimejikita kwenye makaratasi tu si kwenye vitendo, hata wale wenye uwezo wa kudhubutu kufanya jambo la maana hukumbana na vikwazo vigumu pia na ukosefu wa mitaji. Aidha hata tafiti zinazofanywa zimo vitabuni tu wala si vinginevyo. Mfn shughuli km ujenzi, na ufundi wa vitu kama magari, rangi hufanywa vizuri sana kwa uimara zaidi na vijana walioko mtaani na hata hawajaenda shule kabisa kuliko mainjinia walioenda vyuoni na wenye digrii (NB. SI LAZIMA IWE HIVYO JAPO HUO NDIO UKWELI NA UHALISIA )
 
Unashangaa hilo? Achana na wahandisi tu wa mavyuoni kuna wanaume taa (bulb au tubelight) ikiungua anaita fundi kuja kuweka nyingine.

Au kitasa kimeharibika anaita fundi. Ajabu kweli.
 
Nimezunguka madukani kuna kila aina ya charger, za simu, za sola, za taa, sasa! Inakuwaje hatuwezi hata kutengeneza charger za simu? Ni elimu gani wahandisi wa udsm sua dit ambazo wanahitaji kuweza hii kazi ndogo? Au hadi wapate teuzi za jpm ndo waweze?
Waliopata hizo teuzi wamefanya nini zaidi ya kuzitupa taaluma zao na kujikita kwenye siasa.
Tubadili mfumo wa elimu zetu hasa za ufundi, badala ya kukariri maandishi, vyuo vyetu ndio viwe chanzo cha kutengeneza vitu kama hivyo katika elimu ya vitendo
Serikali itenge hela za kutosha, na mashirika binafsi yajitolee kuwezesha ukuaji wa ubunifu.
 
shida inakuja kwamba , atatengeneza ila bei itakua kubwa, mchina anauza 2000, wewe utataka uuze 3000 maana bila ivyo hupati faida, maana vifaa vyote(materials) umenunua uko uko china

ni sawa na utengeneze gari, utanunua vyuma say kutoka china, utatengeneza chassis, aya utanunua

utanunua ready-made engine, kutoka china, unakuta materials nyingi unaagizia unafanya assembly mwisho wa siku product bei iko juu

wakati mchina anauza chaja ya mpaka buku, wewe umetumia buku 3 kununua items na kutengeneza chaja ile ile!
Mbona tumepandisha kodi ya mafuta ya kula ili alizeti ya shelui na mawese yanunulike! Tukimudu situtapiga marufuku charger za china kama tulivyofanya kwa sukari ya zanziber? Na charger zetu zitanunulika
 
Waliopata hizo teuzi wamefanya nini zaidi ya kuzitupa taaluma zao na kujikita kwenye siasa.
Tubadili mfumo wa elimu zetu hasa za ufundi, badala ya kukariri maandishi, vyuo vyetu ndio viwe chanzo cha kutengeneza vitu kama hivyo katika elimu ya vitendo
Serikali itenge hela za kutosha, na mashirika binafsi yajitolee kuwezesha ukuaji wa ubunifu.
Mkurugenzi wa costech na VC wa DIT si ni wateule wa rais wameshindwa nini kuwapeleka wahadhiri wao china kufanya tafiti kuona charger inatengenezwaje? Je hatuwezi kuwatumia TISS kufanya ujasusi wa technology hii ndogo?
 
Mbona tunazalisha mita za luku, hatushindwi charger
Tbs na tra hebu watuambie nchi inatumia shs ngapi za kigeni kuagiza hutu tujitu? Mfano 85% ya powerbank rechargable betry ni lithium ambayo hapa nchini ipo kila mahali wala sio ya kuchimba ni kuzoa tu sasa tunashindwa nini kutengeneza betri ya simu na powerbank?
 
Back
Top Bottom