Inakuwaje bongo fleva inapigwa Kanisani na nyimbo za dini zinapigwa kwenye kumbi za starehe

Kiokotee

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
1,675
2,194
Hili nimelishuhudia mwenyewe kwa masikio yangu mawili;

1. Nyimbo za Anasa kupigwa kanisani yaani kama Bongo fleva.

2. Nyimbo za Ibada kama kwaya kupigwa kwenye Kumbi za Starehe.

Tunafahamu huko kote ndipo walipo waumini lakini mazingira kama ya kumbi za starehe unapiga ile Nyimbo ya "Hakuna Mungu kama wewe" kumbuka Ndani ya hizo kumbi kuna Anasa na Uchafu wa kila aina.

Kama nitapewa majibu kwa kutumia maandiko nitashukuru sana!

( Tumsifu kristo)
 
1.Nyimbo za Anasa kupigwa kanisani yaani kama Bongo fleva.
2.Nyimbo za Ibada kama kwaya kupigwa kwenye Kumbi za Starehe.
Tunafahamu huko kote ndipo walipo waumini lakini mazingira kama ya kumbi za starehe unapiga ile Nyimbo ya "Hakuna Mungu kama wewe" kumbuka Ndani ya hizo kumbi kuna Anasa na Uchafu wa kila aina...Kama nitapewa majibu kwa kutumia maandiko nitashukuru sana!!
( Tumsifu kristo)
Umeeleza kwamba huko kwenye kumbi ndipo kuna madhambi?Basi,hizo nyimbo ndiyo sahihi ili nyoyo zao ziwe laini.
 
Hili nimelishuhudia mwenyewe kwa masikio yangu mawili;
1.Nyimbo za Anasa kupigwa kanisani yaani kama Bongo fleva.
2.Nyimbo za Ibada kama kwaya kupigwa kwenye Kumbi za Starehe.
Tunafahamu huko kote ndipo walipo waumini lakini mazingira kama ya kumbi za starehe unapiga ile Nyimbo ya "Hakuna Mungu kama wewe" kumbuka Ndani ya hizo kumbi kuna Anasa na Uchafu wa kila aina...Kama nitapewa majibu kwa kutumia maandiko nitashukuru sana!!
( Tumsifu kristo)
Yesu alikula pamoja na walevi na makahaba..kumaanisha kwamba wagonjwa ndio wanahitaji daktari..hata shetani haangaiki na waovu anahangaika na walio lipokea neno ili awaangushe.

Injili inawafaa zaidi ambao bado hawajampokea kristo kuliko ambao tayari wamempokea.

Acha zipigwe huko ili neno liwafikie waziache njia zao mbaya wamrudie Mungu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ajabu ni kuwa huwezi kukuta qaswida bar
 
Hivi hizo kaswida huwa zinauzika kweli? Mimi napenda watu woote tuache miziki ya kidunia tushindane kidini coz sisi wakristo nyimbo zetu za din mpaka marekani unazipata
Uislamu hauna nyimbo hao wanoimba izo qaswida ni matamanio yao tu lkn si mafundisho ya Uislamu
Uislamu umeruhusu mashairi bila ya ala za muziki
hlf kitu kingine ulivosema mpk marekani sisi Waislamu imani yetu imejengeka na mapenzi ya Akhera zaidi kuliko dunia mna duniani tunapita tuu kma walivopita wengine
 
Hili nimelishuhudia mwenyewe kwa masikio yangu mawili;

1. Nyimbo za Anasa kupigwa kanisani yaani kama Bongo fleva.

2. Nyimbo za Ibada kama kwaya kupigwa kwenye Kumbi za Starehe.

Tunafahamu huko kote ndipo walipo waumini lakini mazingira kama ya kumbi za starehe unapiga ile Nyimbo ya "Hakuna Mungu kama wewe" kumbuka Ndani ya hizo kumbi kuna Anasa na Uchafu wa kila aina.

Kama nitapewa majibu kwa kutumia maandiko nitashukuru sana!

( Tumsifu kristo)
Luka 5:27-32
27 Baada ya hayo, Yesu akatoka nje, akamwona mtoza ushuru mmoja aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesu akamwambia, “Nifuate!”

28 Lawi akaacha yote, akamfuata.

29 Kisha Lawi akamwandalia Yesu karamu kubwa nyumbani mwake; na kundi kubwa la watoza ushuru na watu wengine walikuwa wameketi pamoja nao.

30 Mafarisayo na walimu wa Sheria wakawanung'unikia wafuasi wake wakisema: “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”

31 Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari, lakini wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa.

32 Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, ili wapate kutubu.”
 
Yesu alikula pamoja na walevi na makahaba..kumaanisha kwamba wagonjwa ndio wanahitaji daktari..hata shetani haangaiki na waovu anahangaika na walio lipokea neno ili awaangushe.

Injili inawafaa zaidi ambao bado hawajampokea kristo kuliko ambao tayari wamempokea.

Acha zipigwe huko ili neno liwafikie waziache njia zao mbaya wamrudie Mungu.

#MaendeleoHayanaChama
Na bongofleva kupigwa kanisani nako hii imekaaje mana inaniumiza mno
 
Hivi hizo kaswida huwa zinauzika kweli? Mimi napenda watu woote tuache miziki ya kidunia tushindane kidini coz sisi wakristo nyimbo zetu za din mpaka marekani unazipata
Waislam tukiwa katika Swala hatuimbi Qasda na wala hazipigwi Msikitini.
Wala usijisumbue maana kuna Baazi ya Mghuramaa wazipinga .
Ndio maana hazina nguvu saana
 
Hivi hizo kaswida huwa zinauzika kweli? Mimi napenda watu woote tuache miziki ya kidunia tushindane kidini coz sisi wakristo nyimbo zetu za din mpaka marekani unazipata 😂😂😂
Ndio mkuu, kuna kipindi nilikuwa na studio mtaa wa mashehe, nilikuwa napiga pesa nzuri sana.
 
Muziki Ni haramu
ZABURI 150:1-6

1 Msifuni Bwana.

Msifuni Mungu katika patakatifu pake,

msifuni katika mbingu zake kuu.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu,

msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,

msifuni kwa kinubi na zeze,

4 msifuni kwa matari na kucheza,

msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

5 msifuni kwa matoazi yaliayo,

msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.

Msifuni Bwana!
 
Muziki zawadi ambayo Mungu ameupa moyo
Huo ni mstari wa biblia lakini sijui ni kitabu gani nadhani Zaburi au mithali

Back
Top Bottom