Inakuaje unachunguza simu ya mumeo?

Inakuaje unachunguza simu ya mumeo?

Utajua ujui

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
268
Reaction score
899
Za asubuhi.

Inakuaje mwanamke unakuwa busy kupekua simu ya mumeo na kuanza kusoma message kuanzia jamiiforum ,fb hadi normal text.

Wakuu niko na mwanamke ninayeishi naye sijamuoa Ila treatment anazonifanyia ninaweza nikafanya awe singo mama.

Nimemkataza kutoshika simu yangu lakini aelewi zaidi ya kugombana kila siku.

Ananuna muda wote.

Hamuwezi mkakaa mkafurahi kama wanavyofanya wanafamilia wengine.

Ana Gubu.
 
Mkuu mimi mke wangu alichukuaga simu yangu usiku me nimelewa nimezima kumbe anaijua pin akatoa lock akaanza kuchukua marina ya kike anawapigia usiku sana na kuwatumia meseji me asubuhi napewa malalamiko wengine maafisa wananiambia we umeanza kuchanganyikiwa siku hizi ukilewa..ilikuwa ni aibu.nilimpiga mwanamke ndo ikawa kisa cha kuachana...mwanamke usije kumpa simu yako hawanaga akili mkuu.change password mara kwa mara
 
Usimkataze. Mfanye asione haja ya kupekua simu yako. Kama hauna unavyoficha, why uogope?
Na vipi Kama hiyo Ni simu yenye contacts za wateja? Maana watu Kama wanasheria wana data Na siri kibao ambazo Ni private Na confidential - zinatakiwa kufichwa Kama padri anavyoficha mambo ya waungamaji...
Mimi Mke wangu tangu nimuoe huu ni Mwaka wa 23 hajawahi hata kuishika- siku akiishika siku hiyo anajua itakuwa ndio talaka...achilia mbali simu- hata mifukoni mwa suruari hakagui...Na nimesikia mara nyingi akiwaambia watoto - don’t go to daddy’s pocket... very disrespectful. Na kweli hawaendi...
Omba Mungu akupe Mke bora wa Matamamanio yako Na atakupa...
 
Sasa anakumilikisha sehemu zake za siri aache kukagua simu yako ili ajue ajikinge vipi na gono na uti?.
Mara nyingi, mtu anayehisi kutendewa ubaya Ni yeye huwa anatenda ubaya... ya nini kuhisi mwenzio sio muaniminifu Na kuanza kupekua simu yake Kama kweli wewe huogopi kivuli cha matendo yako?
Na siku akiianza kupekua siku yako pia ndio mwanzo wa ugomvi lakini mwanzisha ugomvi Ni Yule aliyeanzisha hako ka mchezo ka upekuaji... in every action there is equal and opposite reaction ... ndivyo tulivyoambiwa kwenye darasa la physics - form 2-3... Na hii Ina apply kila siku ktk maisha...
 
Na vipi Kama hiyo Ni simu yenye contacts za wateja? Maana watu Kama wanasheria wana data Na siri kibao ambazo Ni private Na confidential - zinatakiwa kufichwa Kama padri anavyoficha mambo ya waungamaji...
Mimi Mke wangu tangu nimuoe huu ni Mwaka wa 23 hajawahi hata kuishika- siku akiishika siku hiyo anajua itakuwa ndio talaka...achilia mbali simu- hata mifukoni mwa suruari hakagui...Na nimesikia mara nyingi akiwaambia watoto - don’t go to daddy’s pocket... very disrespectful. Na kweli hawaendi...
Omba Mungu akupe Mke bora wa Matamamanio yako Na atakupa...
Mkuu, data za siri zinatunzwa kwenye simu? Tena peupe tu ambapo mtu yeyote anaweza access? Data za siri si zingetunzwa kwenye hidden/secret folders au apps ambazo zingehitaji passwords na fingerprints na patterns kuzifungua?
 
Mara nyingi, mtu anayehisi kutendewa ubaya Ni yeye huwa anatenda ubaya... ya nini kuhisi mwenzio sio muaniminifu Na kuanza kupekua simu yake Kama kweli wewe huogopi kivuli cha matendo yako?
Na siku akiianza kupekua siku yako pia ndio mwanzo wa ugomvi lakini mwanzisha ugomvi Ni Yule aliyeanzisha hako ka mchezo ka upekuaji... in every action there is equal and opposite reaction ... ndivyo tulivyoambiwa kwenye darasa la physics - form 2-3... Na hii Ina apply kila siku ktk maisha...

Kuna watu mafundi wa kukagua simu za wanawake kama nyie wanaume?? Nyie mnaonaga mpo na haki ya kukagua simu zetu ila zenu hamtaki zishikwe.

Na kama haufanyi kitu kibaya kwa nini simu yako ikikaguliwa ukasirike?
 
Nilishamkataza kukagua simu yangu.

Kuna faragha hata kama yeye ni mke wangu aruhusiwi kuzijua .

Nilishampa warning since day one.

Anavuka mipaka .

Halfu anataka ndoa kwa mtindo huu
 
Kuna watu mafundi wa kukagua simu za wanawake kama nyie wanaume?? Nyie mnaonaga mpo na haki ya kukagua simu zetu ila zenu hamtaki zishikwe.

Na kama haufanyi kitu kibaya kwa nini simu yako ikikaguliwa ukasirike?
Simu ya mkononi ni ya mtu mmoja sio wengi.

Akisikia naongea na sauti ya kike ananuna.

Nikichart na mwanamke anakasirika.

Ananiingilia faragha zangu hata kama nimemuoa.

Simu yake hata password siijui
 
Back
Top Bottom