Sigara Kali
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 3,711
- 8,764
Taarabu ni muziki wa mwambao wenye kushkamana na tamaduni za wageni kutoka bara asia hususani uajemi na nchi nyingine za kiarabu ni muziki ambao hapo awali ulikuwa ukiimbwa na wanaume tu wanawake ilikuwa ngumu kushiriki muziki huo pengine kutokana na tamaduni za jamii za watu wa pwani ambao majority ni waisalamu. Siti binti Saad ndiye mwanamke wa kwanza kuanza kuimba taarabu na kuipeleka anga za kimataifa zaidi. Tangia hapo wanawake wakaanza kujingiza taratibu na hatimaye kuuteka kabisa muziki huo. Taarabu kwa sasa imepoteza maana na uhalisia wake lkn kwa wale manju wa kiswahili na utamaduni wa waswahili wanauthanini sana muziki huo na kwa sasa taarabu asilia imebakia huko Zanzibar, mombasa lkn kwa Dar es salam imepotoka na kumbuka kuwa miaka hyo taarabu ilikuwa ni maarufu sana kwa miji ya Unguja, Tanga, Dsm na Mombasa.Kama mada inavyojieleza
Nauliza inakuaje wewe mwanaume kamili rijali unakaa na kuanza kusikiliza nyimbo za taarabu??
Wakati nimesimama pale mataa ya Buzuruga naskia music mnene wa taarabu kutoka gari la jirani,kuchungulia ndani nawaona masela ndo wanaskiliza tena kwa furaha kweli kweli
Music wa taarabu unapendwa na wambea,wanawake na mashoga sasa wewe dume komavu unapata wapi hisia za kusikiliza nyimbo zilizojaa vijembe na gubu?
Mwanaume sikiliza HIP HOP,Bolingo ndomboro ya solo,hizo taarabu waachie wadada na mashoga.
Buzuruga ni Dar?Wanaume wa Dar!
Washakukosea nini ndg?Wanaume wa Dar!
Wengi wao ukiwaangalia wana chembe chembe za ushogaBinafsi simpendi kabisa Mwanaume anaependa Taarabu.
Na kuna waimba blues pia, wengine mashogaNi namna unavyoichukulia taarabu.
Kuna waimba hip hop ni wala unga, je mtu akisikiliza hip hop naye anatakua mla unga?