Inahitajika task force kudhibiti ubambikaji wa kesi

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
467
Points
250

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
467 250
Mh. Kangi Lugola tunakuomba uunde kikosi kazi ambacho kitazunguka Tanzania nzima ili kubaini askari wanaoonea wananchi na kuwabambikia kesi ili tu wajipatie pesa. Maana limekuwa tatizo ambalo linawanyima raha wananchi.

Hakuna mtu anayependa wahalifu lakini ishu ni watu kupewa makosa ambayo hawakufanya.

Leo gazeti la Mwananchi limeripoti wazi kabisa mfanyabishara aliyeomba rushwa ili asibambikiwe kesi ya utakatishaji pesa huko himo Kilimanjaro.

Huko Mwanza ndio inaonekana ni tatizo sugu. Mtu anakutwa na mali ya wizi ni kosa llakini polisi watampa kesi ya unyag'anyi kwa kutumia silaha, sababu haina dhamana ndugu watauza hata shamba au ng'ombe wamtoe ndugu yao.

Hata Rais Magufuli alijionea kwa macho yake pale Butimba Prison kijana alikuwa anauza mafuta ya dili lakini akapewa kesi ya mauaji.

Kule Igunga ndio aibu kabisa mzee wa miaka 90 polisi walichukuwa milioni nane yake. Namna haya matukio yanavyozidi ni dhahiri kuwa watu wanaonewa sana.

Wewe Waziri mwenye dhamana na Polisi tunakuomba uchukue hatua.
 

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
44,712
Points
2,000

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
44,712 2,000
Wakishajua una biashara na mpunga unao
Hata kama unafanya biashara halali lazima
Kuna kikundi fulani cha askari watakufata kukutingisha!
Utageuzwa atm mpaka utakoma
Mwisho wa siku nchi na dunia utaiona chungu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,389,956
Members 528,062
Posts 34,039,593
Top