Inafaa kufanya nini unapoamua kutafuta mtoto/ mimba? Nini yaweza kuwa kikwazo?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,731
10,033
"Nataka kutumia kilainishi wakati wa sex nitakapohitaji kumpa mpenzi wangu mimba, lakini nitumie ipi"

Swali kama hili wengi hujiuliza inapofika hatma na wakati wa kutafuta mtoto unapowadia. Na kwaufupi vilainishi vipo vingi na vya aina tofautitofauti na vinatofautiana gharama pia kulingana na eneo ulipo.

=> Lakini je, naweza kutumia mate?

Wengi wanapendelea kutumia mate kutokana na urahisi wa upatikanaji wake ambao ni sawa na bure. Lakini je, mate yanaweza fanya wenza kutopata ujauzito?

UKWELI JUU YA UTUMIAJI WA MATE WAKATI WA SEX.

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa utumiaji wa mate unaweza sababisha cell za sperm kujongea kwa shida kutokana na kemikali maalum iliyopo kwenye mate, hivyo kusababishia sperms kutofika kwa wakati katika cell ya kike( ovum).

Wataalamu wa uzazi , wanashauri kutotumia mate ikiwa ;

* Mwanaume anapokuwa na kiwango kidogo cha idadi ya sperm/ sperm zenye afya.

👉Lakini kwa wanaume wenye kiwango na ubora mzuri wa mbegu wanaweza kutumia pale tu inapolazimu na si kutumia mate mengi.

ANGALIZO: epuka kutumia KY kwa wakati huo. Ni hatari kwa sperms. Unaweza tumia lubricant nyingine zilizo salama kama olive oil n.k. Daktari anaweza kukushauri na kilainishi gani kinafaa zaidi.

N.B: Unapotafuta mtoto unashauriwa kudeal sana na fore play ili kutengeneza kilainishi asilia kuliko kutumia hivi vingine.


=>Utajuaje kuwa unakiwango kidogo/hafifu cha mbegu wakati unamwaga mengi wakati wa ngono?

* Si wanawake pekee wanatakiwa kufuatilia afya zao za uzazi bali jinsia zote zinatakiwa kufanya hivyo ili kujiridhisha na afya yako. Specialist wanaweza kukupa ushauri zaidi na nini ufanye.

JE, NI STAILI GANI INASABABISHA MIMBA KWA HARAKA?

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mimba huweza kutungwa mda wowote ule wa hatari kwa mwanamke bila kujali utatumia position style gani wakati wa kungonoka. Hata hivyo missionary style inaweza kuwa njema zaidi kwani inaruhusu muingiliano wa kina( deep penetration) hivyo kurahisisha sperm kuwa karibu na mlango wa kizazi.

=> Je, baada tu ya ejaculation mwanamke akasimama haraka na mbegu zitoke inaweza tokea asipate ujauzito?

* HAPANA. Kumbuka ndani ya muda mchache sana mbegu za kiume zinaweza kusafiri na kulifikia yai la kike kwa urutubishaji.

Hivyo, kama hauhitaji kupata mimba kwa muda huo ni muhimu kutumia kondom au njia nyingine za uzazi wa mpango.

=>Umejaribu miezi kadhaa kutafuta mimba ila ikashindikana?

Jambo hilo ni kawaida na inatokea mara nyingi. Lakini kuna baadhi ya wataalam specialists wa maswala ya uzazi wanaweza kukushauri;

A) Epuka muda mbaya wa kutafuta ujauzito.
👉 Muda wa hatari kwa mwanamke ni sahihi zaidi. Kuliko tofauti na hapo.

B) Jaribu kutoa mapumziko ya kuingiliana na fanya angalau mara 1 kwa kila siku katika siku za hatari.
👉 Ungonokaji usio wa kistaharabu unaweza kupunguza wingi wa mbegu.

====> Ni kawaida sana kusumbuka na upatikanaji wa ujauzito hasa kwa watu wazima zaidi ya miaka 35 na kuendelea. Ikiwa uko chini ya miaka 35 na unapata tatizo hilo kimbia haraka sana ukaonane na madakari specialist wakusaidie.

@Satoh Hirosh
 
Mkuu sijaelewa hapa. Inamaana ukitaka kumpa dem mimba inabidi kilainishi kitumike? Kina saidia nini katika utungaji wa mimba?
 
Back
Top Bottom