Inafaa kuanza biashara mpya kwa sasa au ni bora kusubiri kwanza?

said rashid

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
203
112
Kwa kuangalia jinsi mambo na maisha kwa ujumla ya Tanzania kwa sasa (kwa hii miezi baada ya uchaguzi) naona kama kuna hali ya ugumu katika biashara, mpya na za zamani. Tupo bado hatujui haswa tatizo ni nini na litaisha lini, pia hatujui wapi patabaki salama bila kuathiriwa na ugumu huu wa sasa.
Sasa natamani kuanzisha biashara lakini napata wasiwasi, nianze au nisubiri kidogo ili nione baada ya muda hali itakuwaje?
Wajasiriamali na wafanyabiashara wenzangu naomba ushauri tafadhali
 
Kama fremu ni yako fungua hiyo biashara ili walau hata wateja wawe wanapita na kuiona au hata kuuliza bei, hii itakusaidia walau kutangaza biashara yako ili hali ikiwa nzuri wateja waje kwa urahisi
 
Kwa kuangalia jinsi mambo na maisha kwa ujumla ya Tanzania kwa sasa (kwa hii miezi baada ya uchaguzi) naona kama kuna hali ya ugumu katika biashara, mpya na za zamani. Tupo bado hatujui haswa tatizo ni nini na litaisha lini, pia hatujui wapi patabaki salama bila kuathiriwa na ugumu huu wa sasa.
Sasa natamani kuanzisha biashara lakini napata wasiwasi, nianze au nisubiri kidogo ili nione baada ya muda hali itakuwaje?
Wajasiriamali na wafanyabiashara wenzangu naomba ushauri tafadhali
anza na ya mtaji mdogo
 
Nafikiri kuanza ni bora zaidi ya kusubiri. Kwa maana utapata ujuzi wa aina ya biashara unayoitarajia.
Cha msingi ni kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuuanza
Wasalaaam
 
Inategemea na aina ya biashara na unategemea nani watakuwa wateja wako. Kama unalenga taasisi za umma pengine si wakati muafaka, maana nyingi zinakabiliwa na ukata na mambo ya sintofahamu. Lakini kama ni biashara for general public haina shida.

Cha muhimu ni kwamba ugumu wa maisha wa sasa unatokana na kukatwa kwa mirija ambayo haikuwa halali. Watanzania wengi tulizoea kuishi kwa vipato vya magumashi. Inachotekea sasa ni kwamba watu wengi wataanza kuishi kwa vipato vyao halali. Hii ina maana watu watatumia hela zao kwa makini kwenye vitu muhimu tu.

Kama biashara yako inahusu mahitaji muhimu ya binadamu itaendelea kuwepo, lakini kama biashara yako ni ya vitu vya luxury au ambavyo si vya lazima itazorota. Watu wana cut spending kwenye vitu visivyo vya lazima.

Biashara nyingine ambazo zitaathirika ni za vifaa vya ujenzi, kwani kwa kipato halisi cha watanzanja wengi kujenga ni issue. Watu wengi kama watumishi wa umma wameweza kujenga kwa sababu ya safari hasa za nje ambazo sasa hivi hakuna.

Trend hii haitabadilika hivi karibuni. Tafadhali uasianze biashara bila kufikiria hivi vitu.

Hapa mjini tutaheshimiana sana katika kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom