Maisha bora kwa kila mtanzania, alafu SISIEM wakienda hapo kijijini wanawaahidi kuwajengea kiwanja cha ndege, Alafu chama kinajisifu barabara nchi nzima, uchumi umepanda, wakati kuna watu mlo mmoja kwa siku mbinde, hakuna ajira wala opportunity za kujiajiri, hakuna soko la mazao wala pembe jeo za uhakika. (kilimo kwanza), elimu imekaa kisaini zaidi (kisiasa) serikali inajisifu imefanikiwa kujenga shule nyingi lakini hakuna vikalio ( simaanishi viti pekee kwakuwa hata mawe ya kukalia hakuna). Darasani watoto 80 mpaka 120 na hakuna vitabu vya ziada wala kiada. Serikali inajisifu idadi ya kufaulu imepanda wakati nusu ya wanaofaulu darasa la saba hawajui hata kuandika majina yao.
KISHA 2015 TUNAICHAGUA TENA SISIEMU. ( LAAAAAAAAANA)