dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,476
- 2,087
Kama somo linavyojieleza,
Imekuwa ni kawaida sasa watu wa kada mbalimbali walioko kwenye mahusiano,
Kurusha kero wanazokumbana nazo kutoka kwa wenza wao wa jinsia nyingine,
Mara nyingi kero hizi zinao uhusiano wa karibu juu ya nani anapaswa kumhudumia mwenzake, kumsaidia ama kwa namna gani upande mmoja unapaswa kuchangia kwa kiasi gani kiuchumi kwa upande mwingine.
Bila kujali ni uhusiano wa kawaida (Kimapenzi) au tayari watu hao wapo kwenye ndoa.
Wakati ambapo upande wa wanawake walio wengi wanadhani ni wajibu kwa mwanaume kumhudumia mwanamke na pengine hata baadhi ya wanaumme wakiamini hivyo pia,
Lipo kundi lingine likibaki na msimamo wa kati kuwa pande zote za uhusiano zinapaswa kushiriki kwa sehemu sawa kushiriki katika kuuhudumia uhusiano.
Ikiwa na maana kuwa kama mwanamme atatoa shilingi mbili basi mwanamke nae atoe kiasi hichohicho katika jambo lolote litakalokuwa na tija ya mojakwamoja kwa wahusika walio kwenye uhusiano.
Mkanganyiko huu umepelekea hadi baadhi ya watu kufikia kukejeliana kuwa kama mwanamme hajafanya haya basi,
Si mwanaume timilifu.
Huko wengine wakidai iwapo mwanamke atashadidia ama kulazimisha afanyiwe hili na lile na Mwanaume basi atakuwa 'Mchunaji'-
Hali hii sasa imezaa sintofahamu juu ya lipi ni sahihi na lipi si sahihi hasa ikizingatiwa kuwa wengine msimamo wao upo kiimani ya kidini, ingawa baadhi ya watu wamekuja na hoja kadhaa kuukosoa hata misimamo ya kiimani kuwa zizingatiwe hoja za uhalisia wa kimaisha(Kidunia) Na mabadiliko ya hali ya kimaisha kwa sasa ambapo wengi wanadai kuwa ili mambo yaende sawa basi mume na mke wote wawe na mchango sawa kwenye uhusiano-katika kuchangia uchumi.
Hata hivyo nionavyo mimi,
Na naamini huu ndio ukweli na ukweli mtupu wa hali ilivyo- taka usitake;
MAPENZI YA KWELI NDIO YENYE JIBU SAHIHI KATIKA HILI.
Haihitaji kupenda tu, Ila kupenda kwa dhati, dhati ya moyo na yooote yatafuata.
Kama umempenda kweli utamjali, Utamhudumia, Utampa chochote ulicho nauwezo nacho-Kamwe hutalalama,hutakuwa na hesabu juu ya thamani ya umpatiacho, mara ngapi na pia hutanung'unika.
Tatizo ni kuwa wengi hatujajua thamani ya kupenda kweli.
Mara nyingi tunajikuta tunatamaniana na kuamua kuridhishana huku tukiamini kuwa ndio pendana kumbe bado hatujafikia huko (inahitaji ufahamu kujua unapendwa na namna gani upende pia)
HITIMSHO:
Kama umependa kweli, uwe mwanamke, uwe mwanamme; utahonga,hutamsikiliza mwingine bali umpendae, hutajiuliza marambilimbili na utaridhidhika nae.
Kama bado unakigugumizi juu ya hili usiwe na pupa, Ipo siku Utapenda na yote yatakayosemwa itakuwa bure kwa kuwa utakuwa Umependa, Zile pumba zile "ooo hanifanyii hivi, Siwezi mfanyia hivi bila hiviii, pumbavu zako bado hujajua wewe jua halafu uone, Utachunika, Utahonga na Kwa wale wadada hata ungekuwa unabana vipi zile eti "Sivui Ch.. hadi nione mkwanja",Hakuna kwanza kwani wewe muuza K? -USICHEZEE KUPENDA WEWE ALAA!